Futari nyumbani kwa Hamza Aziz siku aliyowaeleza wageni wake kisa chake akiwa Inspector Geneal Of Police ( IGP) alipokataa kutii amri kutoka juu

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
View attachment 1117048

Kuna rafiki zangu watu maarufu katika duru za Kiislam waliniomba niwapeleke kwa Hamza Aziz na ilikuwa katikati ya miaka ya 2000.

Nilimpigia simu na akatukaribisha nyumbani kwake nyumba ambayo kwangu mimi sikuwa mgeni.

Siku hii kwa kuwa nilikuwa nimekwenda na wageni Hamza Aziz hakutukaribisha kwenye kibanda chake cha makuti cha kupunga upepo, kibanda kinachoangalia Bahari ya Hindi.

Hiki kibanda kilikuwa Majlis yetu sisi wawili.

Siku hiyo tulikuwa katika ukumbi wake ndani ya nyumba yake nzuri ya gorofa moja Msasani unaelekea Kawe.

Ulikuwa Mfungo wa Ramadhani.

Baada ya wale rafiki zangu kumaliza kile kilichowaleta tukawa tunafanya mazungumzo ya hili na lile.

Ghafla Hamza Aziz akaniuliza, ‘’Mohamed nimekualikeni futari?’’

Mimi nikamjibu kuwa hakutualika futari miadi ilikuwa ni mimi kuwaleta kwake wale rafiki zangu kwa lile walilotaka kuzungumzanae.

Pale pale Hamza Aziz akasema, ‘’Basi nakualikeni futari leo msiondoke.’’

Kadri tulivyojaribu kumkatalia hakukubali akasema mshafika nyumbani kwangu leo tufuturu pamoja.

Basi ikawa sasa ule wasiwasi wa kuondoka kwenda majumbani kwetu kuwahi kufuturu umeondoka tukawa sasa tumekaa tumetulia tukifaidi upepo mwanana wa Bahari ya Hindi uliokuwa ukiingia kupitia madirisha yale makubwa na huku tukiiangalia bahari yenyewe iliyokuwa na rangi ya bluu ya kupendeza.

View attachment 1117049

Sasa mimi nakijua kisa cha Hamza Aziz ambacho alinihadithia mwenyewe alivyokataa kutii amri kutoka juu ya kumkamata Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir akituhumiwa kuwa alikuwa katika mipango ya kupindua serikali ya Tanzania.

Hamza Aziz alimkatalia Waziri wa Mambo ya Ndani Said Ali Maswanya aliyemfikishia amri ile kuwa hawezi kamwe kumkamata Sheikh Hassan bin Ameir kwa sababu za uongo.

Basi nikamchokoza Hamza Aziz nkamwambia, ‘’Baba hebu tueleze kile kisa cha Sheikh Hassan bin Ameir.’’

Mimi nilifanya hivyo kwa kutaka na wale ndugu zangu wasikie kisa kile kutoka kwenye mdomo wa farasi mwenyewe.

Waingereza wanasema, ‘’From the horse’s mouth.’’

Nilitaka na wao wawe shahidi wa historia ile muhimu sana katika historia ya Tanganyika baada ya uhuru wake mwaka wa 1961.

Hamza Aziz aliwageukia wageni wake akasema huku akicheka, ‘’Huyu Mohamed ni mchokozi sana.’’

Hamza Aziz alianza kueleza kisa kile akianza na mgogoro uliokuwapo wakati ule wa East African Muslim Welfare Society (EAMWS) serikali ikitaka ivunjwe ili ipatikane nafasi ya kuuunda BAKWATA.

Ukumbi ghafla ulikuwa kimya na sauti iliyokuwa ikisikika ilikuwa ya Hamza Aziz akieleza mkasa ule na upepo uliokuwa ukivuma na kutikisa matawi ya miti iliyokuwa nje jirani na nyumba yake.

Hamza Aziz alimaliza kwa kusema maneno haya: ‘’Siku zote namshukuru Allah kwa kuniongoza kufanya uamuzi ule kwani laiti mimi ningelitoa amri ya polisi kumkamata Sheikh Hassan bin Ameir leo ningeliwatazamaje Waislam?’’

Maghrib iliingia tukapiga adhana, tukafungua kwa tende na vinono vilivyokuwapo tukaswali ukumbini kwake, tukafuturu pamoja kisha tukaagana.

Picha hapo juu Hamza Aziz akiwa askari kijana na picha nyingine ni Sheikh Hassan bin Ameir na viongozi wakuu wa serikali ya Tanzania..
 
Sheikh Mohamed kwanini hii mada umeipost mida ya wachawi na walozi? Saa tisa usiku sheikh! Au ndio mida yako ya kula daku?
 
sheikh mohamed kwanini hii mada umeipost mida ya wachawi na walozi?. saa tisa usiku sheikh!!. au ndio mida yako ya kula daku?.
Smarte,
Nilikuwa nimerudi nyumbani kutoka msikitini kwa ajili ya Kiyam Layl, yaani Kisimamo cha Usiku.

Huo kama ni muda wa wanga ni bahati mbaya sana kwani katika Uislam huo ni muda Allah anaoupenda watu waamke na kusali.

Wakati nasubiri kula daku nikaona nimwandike rafiki yangu Hamza
Aziz.
 
Somo zuri Mzee Mohamed Said. Zama hizi sijui ni vigogo wangapi wenye uwezo wa kukataa amri zenye utata toka juu .
Bagamoyo,
Hamza Aziz
alifanya uamuzi wa kishujaa sana.

Hamza Aziz alipata kunieleza kuwa katika miaka ya 1960 alikuwa akiishi nyumbani kwao Mtoni na alikuwa na kawaida ya asubuhi kufanya mazoezi ya kukimbia kutoka Mtoni hadi Kituo Cha Polisi cha Kilwa Road na kurudi Mtoni.

Siku moja wakati anatoka nyumbani kutaka kuanza mbio zake Sheikh Yahya Hussein akawa amefika akamwambia kuwa anaitwa na SheikhHassan bin Ameir.

Pale pale wakaongozana hadi kwa sheikh.

Sheikh Hassan bin Ameir akamwambia kuwa amemwita kwa kuwa anataka kumuombea dua kwa Allah.

Hamza Aziz ananihadithia anasema, ''Sheikh Hassan bin Ameir alinyanyua mikono yake juu akaniombea dua ndefu sana kisha akaniruhusu kuondoka.''

Hamza Aziz anasema miaka mingi ikapita na yeye akawa kasahau ile dua aliyoombewa na Sheikh Hassan bin Ameir hadi siku ilipomfikia amri kutoka juu akamkamate Sheikh Hassan na alipouliza kosa la Mufti ni lipi na kujibiwa kuwa alikuwa anafanya mipango ya kupindua serikali, pale pale alijibu kuwa huo ni uongo.

Hamza Aziz akakataa kupeleka askari kumkamata Sheikh Hassan bin
Ameir.
 
Ukweli katika uongo ni sawa na mafuta yaliyopo kwenye maji. Ukweli wake Bwana Aziz uliwatenganisha wakweli na wafitini. Hapa tunapata funzo jinsi viongozi wa kiislamu wanavyotakiwa kuutetea uislamu hasa pale wanapojua kuna maagizo ya kinafiki na uongo yanayotaka kuwaangamiza wale wasio na hatia.

Tujiulize hivi leo kuna muislamu anayeweza kuyafanya yaliyotendwa na Hamza Aziz?
 
Kisa kizuri hiki cha Hamza Aziz, huyu ni miongoni mwa Watanzania wachache sio tuu waadilifu, bali pia, wanaojua haki zao.

Akiwa IGP, aliwahi kugonga mtu, akaua, hakuripoti on time, Nyerere akakasirika, akamtimua kazi kwa summary dismisal, unakosa haki zako zote.

Huyu jamaa akafungua kesi kuishitaki serikali, mtu huwezi kufutwa kazi kwa traffic ofence, akashinda, serikali ikaamriwa kumlipa haki zake zote na fidia, akavuta fungu la maana, akawa tajiri.

Mwalimu Nyerere aliogopwa kama Mungu na serikali pia iliogopwa, who would dare challenge him?. Hamza Aziz did.

P
 
Kitendo cha kugonga mtu na kushindwa kuripoti on time tena akiwa askari anayejua sheria kinamuondolea sifa ya uadilifu.
 
Kwezisho,
Muda utasema.
 
hivi askari anaweza kukataa amri toka juu na bado akawepo kazini tuanzie hapo
Rodrick...
Hilo saula la askari kutii amri hata ikiwa ni batili lilizungumzwa sana katika Nuremberg Trials baada ya WWII pale askari wa Kijeruamani waliopandishwa kizimbani kwa ajili ya vitendo vya mauaji ya Wayahudi na watu wengine.

Kutii amri kutoka juu kama kinga mahakamani haikuwasaidia.

Washitakiwa walikuwa wakijitetea kuwa walo walikuwa wanatii amri kutoka juu.

Haikuwasaidia hata chembe walionekana wauaji tu na kutiwa hatiani. Wengi wao walinyongwa.
 
Aliendesha gari la serikali akiwa kalewa mbwiii! Islam mlevi. Uliwahi kuusikia wimbo wa Makongoro kumhusu dereva mlevi wa gongo?!
 
Angefanya kipindi hiki cha JPM afu tuone angeshinda hyo kesi!!!
 
"Dereva kalewa pombe, akaja kugonga mtu"
"Sawa hiyoo?"
"Hataa, Hiyo si sawa dereva acha vituko"

P
Kwa comments hizi na zingine kwenye nyuzi za Mzee Mohamed Said unaweza kugundua upande uliojificha wa Pascal Mayalla na hisia zake juu ya imani nyingine.

Take in easy Pascal.. Mzee anajaribu kutufahamisha yale yaliyojificha toka kwenye kitovu halisi cha historia ya Tanganyika na baadae Tanzania (Dar es salaam) watu wake, mila, zake, utamaduni wake na mchango wake mkubwa katika kubadilisha na kurudisha uhuru wa Tanganyika toka kwa udhamini na mikono ya Waingereza na wale kabla yake.

Ni mtu aliyekulia katika mazingira hayo na watu waliokuwa wapambanaji ni sehemu ya mazingira yake.
(Sina hakika kipindi hiko kama ulikuwa tayari umeshazaliwa au uko wapi)

Najua kwamba tafiti na historia za Mzee Said Abdallah ni religious influenced but behind it kuna logic reasons na ushahidi ambao haujapambanuliwa dhahiri na wana historia wetu. (Amini mimi na wewe na wengine ni mazao ya hizo historia na sababu zake).

Why are you Always try to discredit him?
 
Mkuu darcity , kwanza namheshimu sana Mkuu Maalim Mohammed Said, pili nakitambua kipaji chake, uwezo wake wa kusimulia visa na kikubwa zaidi, naifahamu power zake alizonazo ambazo ana zi impart kwenye maandishi yake.

Tatizo langu mimi ni mkweli daima, toka ndani ya nafsi yangu, hivyo nikikutana na hoja yoyote iliyovikwa urongo, kazi yangu sio kum discredit, bali kazi yangu ni kusema tuu kuwa jambo hili ni urongo.

Mfano wa juzi kati, harakati za zilinashibishwa na dini fulani na kuelezwa kuwa watu wa dini fulani ndio waanzilishi, niliwawekea humu kuanzia mwanzilishi wa AA, TAA na TANU, hakuna hao watu wa dini hiyo.

Pia nimemsikia akisema ndani ya Bunge la JMT, wabunge Waislamu ni only 6%, kitu ambacho ni urongo wa mchana kweupe, kwasababu wabunge wote wa Zanzibar ni Waislamu, hao tuu wenyewe ni over and above hiyo 6%. Uwongo kama huo sio wa bahati mbaya, ni planned for some specific motives behind, Maalim anaijua, na sisi wasomaji wa in between the lines, unaweza ukasoma kitu halafu ukaijua the state of mind ya mwandishi alidhamiria nini ili apate nini!.

I don't discredit the writer, namheshimu sana, I discredit the contents that contains the lies, that are smartly mixed with the facts, by pointing specifically to such lies.

P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…