Futballplanet: Guardiola na prof Nabi wagombea tleble tofauti duniani

Futballplanet: Guardiola na prof Nabi wagombea tleble tofauti duniani

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
Josep ‘Pep’ Gurdiola na Nasreddine Nabi ‘Prof Nabi’ ni makocha 2 maarufu sana ambao wanakimbizia rekodi zinazofanana katika maeneo tofauti.

Pep kocha maarufu Duniani kote anakimbizia rekodi ya Sir Alex Ferguson aliyoiweka mwaka 1999 akiwa na Manchester United ya kutwaa makombe 3 (treble) alipochukua FA CUP, EPL na CHAMPIONS LEAGUE, leo Pep Ana hiyo nafasi kwani yuko Fainali ya FA, anaongoza Epl na yuko fainali ya Champions League hivyo uwezekano ni mkubwa.

Prof Nabi anakuwa kocha wa kwanza kutoka klabu ya Tanzania kuonekana yuko kwenye uwezekano mkubwa wa kutwaa makombe 3 tena 1 likiwa la mashindano ya vilabu Afrika.

Kocha huyu maarufu zaidi nchini kwa sasa ameziongezea sifa barani Afrika alipoifikisha Yanga SC fainali ya Kombe la Shirikisho. Tayari ana NBC PL , yuko nusu fainali ya FA CUP na yuko fainali ya CAFCC.

Source: futball planet

NB: Kwa mliokimbia shule

Tleble is achieved when a club team wins three trophies in a single season.
1684491137952.jpg
 
Back
Top Bottom