Katika mchezo wa soka kuna kujifunga ''own goal''. Katika tennis kuna 'unforced error'' kwamba mchezaji anafanya makosa bila shinikizo la mpinzani wake. Halafu kuna goli la mkono la Nape
Unforced error inatokana na udhaifu wa mchezaji kujipanga kukabiliana na mashambulizi
Own goal hutokea kwa nia njema, kwamba, lengo ni kuokoa mwisho wake ni kujifunga
Goli la mkono ni kulazimisha kufunga kwa njia za haramu
Bunge lilitaka goli la mkono,kwamba, kumsusia CAG kwa neno dhaifu kungemlazimisha ajiuzulu
CAG Prof Assad akaling'amua hilo, hakujiuzulu
Bunge likifanya unforced error kwa kutafuta 'kiroja' na kukifanya hoja. Hakuna aliyeshinikiza hilo
Taarifa ya CAG ipo hadharani na kuondoa shaka juu ya kauli yake. Bunge limeithibitisha kauli hiyo kwa mtindo wa ''own goal''. Nia ya Bunge ilikuwa ''njema' CAG aondoke. Wamejifunga