NGUVU YA UMMA TUNASUBIRI TU MAELEKEZO YA LUGHA YA MWILI WA KIKWETE, MAKINDA NA CCM YAKE JUU YA MUSWADA WA KATIBA MARA BAADA YA 'PUBLIC HEARING' NA HATIMAYE MCHANGO WA WABUNGE NDANI YA BUNGE DODOMA!!!
Kama mtu atakua anayakodolea tu macho huo mkutana wa Mhe Lema na Machalii wa Makao Makuu ya mabadiliko (Arusha) nchini na kutafuta kunusanusa kwamba kumeongeleka nini basi ni kupoteza to muda.
Mikutano karibu yote muhimu na washikadau nchini kote nchini tayari yamekamilika kiaina, mijini na vijijini na ujumbe wa mabadiliko bado yanasambaa huko kama moto wa kiangazi porini.
Kinachosubiriwa sasa hivi tu ni mwelekeo gani huo Muswada wa CCM juu ya katiba utachukua mara baada ya kilichoitwa 'Public Hearing' na hatimaye mchango wa bunge juu ya hili; hasa wabunge wa CCM na endapo kwao Maslahi ya Umma ndi yatatangulizwa au ya CCM.
Yaani hadi hatua ya hivi sasa ni kwamba serikali ya Kikwete ndio itakayotuelekeza nini cha kufanya, kutokana na matendo yake ndani ya kipindi kifupi kijacho ndani ya mwezi April, sisi kama Nguvu ya Umma kote ncini kulinda haki na maslahii yetu.
Haki mbeeeele kama tai katika wananchi kushika ushukani kuamua na kusimamia mwelekeo mzima wa mchakato wa Katiba Mpya nchini. Kila kijana Tanzania Bara na Visiwani, muda wa Ukombozi u jirani leo kuliko hapo jana na hivyo sote tukae mkao wa ushindi juu ya mchakato wa katiba nchini kumalizana salama na MAFISADI nchini.
Huu uvumilivu wetu wote ni kwa ajili ya kutopenda kusikia kisingizio chochote hapo baadaye mtu akitulalamikia vijana kwa hatua zitakazofuatia katika ukombozi wa taifa letu tuipendayo kwa njia ya amani.