kwa Mtazao wake eti Wachina wameleta maendeleo Afrika kwa Kujenga Viwanja vya Mpira 'akasema "Football grounds" Labda akimaanisha kiwanja kile cha TEMEKE (UWANJA WA TAIFA MPYA). Hakuwa hata na takwimu za kuthibitisha mahala pengine katika Afrika ambapo Wachina wamejenga Uwanja wa mpira wa miguu kama angeulizwa hilo.
Amezungumzia Afrika haiwezi kuishi bila China na kubainisha kuwa "milioni of exports to China from Tanzania especially cotton, sisal, coffee " etc na Kuhoji kwa kiingereza eti "... and if not China, where we could sent our products???> Hajui hata maana ya bishara za kimataifa zinafanyikaji na hakuweza kufahamu ni kiasi gani cha thamani za bidhaa za mazao ya Kilimo ambazo Tanzania imeuza nchini China.
Alipoulizwa kuhusu changamoto za ushirikiana ulipo kati ya Afrika na China alisema "Problem is technology for example machine, how to operate machine is difficult in Africa....." khaaaa..
Mwendesha mada akaingia kati na kumkatiza " oh yes, I get your point...."
Labda TBC waliamua kumtuma yeye kwa kuwa kwa sasa anashikilia lile dawati ambalo Clement Mshana alikuwa akishikilia wakati wa TIDO.