Gabrieli Jesu, huyu Dogo ndo mrithi wa Ronaldinho pale Brazil

mbona chenga za gaucho ni kopi ya chenga za ronaldo de lima,ambazo lima nae alikopi kwa 'wazee' waliotangulia kasoro chenga moja tu,anachofanya gaucho ni kuongeza madoido
Acha uongo, gaucho hafanani hata kidogo na ronaldo lima, gaucho anafanana kimchezo na okocha wa nigeria. Kumbuka okocha ndiye aliye msimamia gaucho pale PSG ufaransa wakati wakicheza timu moja.
 
itachukua muda kupata mtu sahihi wa kumrithi gaucho yule alikuwa wa sayari nyingine kabisa. huyo dogo bado hajafikia hata nusu ya gaucho ila anaonekana ana kitu fulani anacho na bado umri unamruhusu tumpe muda kwa sababu mpira unachezwa hadharani tutamuona tu.
 
Gaucho kama okocha kila kitu kwa tuliozaliwa mapema tafuta chenga za okocha utamjua nani
 
Gaucho was one of the most talented players and he played football with style. It was a delight to watch him dancing his way past world class defenders and scoring seemingly impossible goals with a smile on his face.
 
mbona chenga za gaucho ni kopi ya chenga za ronaldo de lima,ambazo lima nae alikopi kwa 'wazee' waliotangulia kasoro chenga moja tu,anachofanya gaucho ni kuongeza madoido
Ni kweli kuwa baadhi ya chenga za Gaucho zilifanana sana na za Ronaldo "el phenomena" De Lima ambaye naye ni moja ya wafungaji magoli hodari zaidi kuwahi kutokea. Lakini tofauti na Ronaldo, Gaucho alikuwa anacheza mpira wa kuvutia zaidi na kwa umahiri ambao hakuna mchezaji ambaye ameweza kufikia kiwango change mpaka sasa.
 
 
Nimemuangalia dogo ana kipaji kwa kweli, ila wachezaji wa kuandikwa andikwa na kutabiriwa huwa hawafanyi vizuri, ila wanapata soko..

Mi nakumbuka Ronaldinho akutabiliwa wala kufananishwa na yoyote, kombe la Dunia 2002 ndio lilimtangaza
 
Mmmh! Gaucho si rahisi hivyo.... Hao wachezaji wa kuwaangalia kwenye YouTube hovyo kabisa... Hakuna kama Gaucho ulimwengu huu na itakaa mda mrefu kumpata Gaucho mwingine... .
 
mbna hako kadogo sura yake inaonesha wazi kuwa kakikupigwa buti katakua kanarudishia, gaucho alikua arudishii
 
Acha uongo, gaucho hafanani hata kidogo na ronaldo lima, gaucho anafanana kimchezo na okocha wa nigeria. Kumbuka okocha ndiye aliye msimamia gaucho pale PSG ufaransa wakati wakicheza timu moja.
nenda google,katafute ulinganifu wa gaucho na de lima kwa video,ronaldinho maana yake Ronaldo mdogo,umeanza kuangalia mpira jana unatuita wazee wazima waongo,ronaldinho kapiga chenga gani ya okocha!?
 
Huyo dogo Gabriel anafanania na Robinho au Naymar mchezo wake, Gaucho ni mashine nyingine, waulize waingereza watakwambia akicho wafanyia hata kabla hajatua barca
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…