Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua, amesema eneo la Mlima Kenya litakuwa na mgombea wa urais katika uchaguzi mkuu wa 2027, hata kama yeye mwenyewe atazuiwa kuwania nafasi hiyo.
Akizungumza katika mahojiano Jumatano usiku, Julai 22, Gachagua alisema amekuwa akiwalea na kuwaandaa viongozi vijana ambao wanaweza kuwania urais iwapo hataruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Gachagua, ambaye anaongoza chama cha Democracy for the Citizens Party (DCP), alisema eneo hilo litakubaliana na kumchagua mmoja wa viongozi hao kuwa mgombea wake wa urais. Alieleza kuwa viongozi hao vijana wana nguvu na uwezo wa kisiasa, akidai kuwa baadhi yao wanaweza kufanya vizuri zaidi kuliko yeye katika kinyang'anyiro cha urais.
Kauli hiyo inakuja wakati Gachagua akiendelea kukabiliana na changamoto za kisheria zinazohusiana na kuondolewa kwake madarakani. Mahakama Kuu ilithibitisha uamuzi wa Seneti wa kumuondoa katika nafasi ya Naibu Rais, ingawa iliamua kuwa hakutendewa haki wakati wa mchakato wa kusikilizwa kwa kesi yake na kumpa fidia ya KSh50 milioni. Gachagua amekata rufaa dhidi ya uamuzi huo katika Mahakama ya Rufaa.