Nyeri, Kenya
Naibu Rais ameachilia kombora la utani kwa wanaume wa eneo la Kati, akidai wameshindwa na majukumu muhimu ya ndoa kwa sababu ya kutekwa na ulevi.
Bw Gachagua alisema wanaume wa Mlima Kenya wamekuwa mateka wa pombe, hasa ile haramu.
Alisema athari za pombe zimewalemea kiasi cha kushindwa na majukumu ya kindoa.
“Vijana wetu wameisha. Kwa kitanda, badala ya kulala juu wanalala chini. Kina mama ndio wanalala juu peke yao,” Naibu Rais alisema.
Alitoa kauli hiyo Ijumaa, baada ya kufanya mkutano na wakuu wa usalama eneo la Kati, shabaha ikiwa kuweka na kuainisha mikakati dhidi ya pombe haramu.
Alisema kero ya mvinyo haramu katika ngome yake, imezidi unga kiasi cha viungo vya siri vya wanaume kukosa nguvu za kiume.
Gachagua aidha alilalamikia viwanda vya pombe na wagemaji pombe haramu kutumia kemikali katika kuunda vileo.
“Ethanol (kiungo kinachotumika kutengeneza pombe) inakuja kama imechanganywa na kemikali, inamaliza viungo vyote na nguvu za uzazi za vijana wetu.
“Betri zote ziko chini, hata ikiwekwa chaji haitachukua. Wanawake wetu wanalia, na huo ndio ukweli
Watu wengi hawataki kuongea ukweli, na mimi ni mtu mkweli. Husema ukweli,” alielezea.
Naibu wa Rais aliamuru wasimamizi wa vituo vya polisi (OCS) kufanya msako mkali katika maeneo na mazingira yao ya mabaa, vilabu, vituo vya burudani na kujivinjari na viwanda vinavyounda pombe haramu na ile hatari.
Aidha, alitoa onyo kwa maafisa hao wakuu wa askari kwamba yeyote atakayepatikana akichukua hongo kuruhusu utengenezaji, ugemaji au uuzaji wa pombe haramu hatakuwa na budi ila kumtimua kazini.
“Hali ni mbaya na haitaendelea hivyo.”
Alitumia mfano wa shule za chekechea, kuonyesha jinsi wanaume eneo la Kati transfoma zao zimezima kwa kushindwa kutungisha bibi zao ujauzito.
“Ukienda shule zetu zote, madarasa hayana wanafunzi. Hata hizi pesa za ECDE magavana wanaweka ni upuuzi tu. Hakuna watoto,” alilalamika.
Mlima Kenya ni miongoni mwa maeneo yaliyotajwa kuathirika pakubwa na kero ya unywaji pombe, hasa ile hatari na haramu.
Mkutano wa Bw Gachagua na wakuu wa usalama eneo hilo, pia ulihudhuriwa na magavana, wabunge na viongozi wa kisiasa.

'OUR WOMEN ARE CRYING, WANAUME HAWAFANYI KITU KWA KITANDA!' DP GACHAGUA ON ILLICT BREW!!