Gadafi bwana.
Ninaposoma habari hiyo hapo juu ninakumbuka mambo kibao. Ninajaribu kukumbuka hali ilivyokuwa wakat wa chama kimoja.
Kwamfano, dk. Slaa angekuwa bungeni leo hii? Au watu wa sampuli ya dk. Slaa wangekuwa wapo mle bungeni? Watu ambao si watu wa yes SIR. Hoja anazowakilisha leo bungen na wabunge wenzie wa upinzan zingewasilishwa bungen? Hapa unaweza sema mbona wapo akina anne malecela na wengineo kutoka ccm lakin mi naamin hao wanakuwa na nguvu zaid kunapokuwa na upinzan. Wengi katka ccm utakuta ni kina ndio mkuu ili next bunge wawemo ndani. Vyama vingi ni njia mbadala ya watu wanaofaa kwenda kutusemea tusio na saut huku vijijin na mijin.
Wapinzan wamekuwa mbele hapa tz kupinga ufisad. angalau kweli bunge linaichangamsha serikali. Na naamin bila upinzan kusingekuwa na vita hii (kali?) ya ufisad inayoongozwa na mjeshi kikwete. Wapinzan huiamsha serikali. Tz ni mfano
Libya huenda haina ufisad au uzembe kama ule uliowadondosha kina lowasa au kama ule wa kununua rada au kama ule wa umeme wa iptl, lakin tz upo. Ni watu kutoka vyama vya upinzan ndo wanatakiwa kuibana serikali kuhusu kadhia hiyo. Wale wa ccm ama wamelala, au wako bize kujikomba wapate uwazir na nk, au wanaona sio vizur kuiuliza serikal ambayo ni ya chama atokacho. Kwa hiyo wanabak kuuliza tuswali tudogotudogo ambato tungeweza ulizwa penginepo. Halaf wepes wa kuunga mkono kila kitu wasijeonekana wanaibana serikal ‘yao'. Na wakiibana sana utakuta wanaitwa kwenye vikao vya chama na kuwa ‘displined'.
Naam, kwa tz, vyama vingi viendelee.
Kuna gharama kubwa ya kuendesha chaguz na kuvihudumia vyama vyote lakin kwa Tanzania tukifanya cost benefit analysis mi na come up with more benefits than costs.
Wengine katka upinzan wanajikomba ccm au hawawajibiki ipasavyo, lakin sio rahis kukosa defects popote