Gadafi anafaa kuiongoza afrika kweli?

Hivi cha muhimu zaid nin kwa nchi? Demokrasia, dini au maendeleo ya nchi?
Nasikia demokrasia iko ndogo libya. Jamaa kang'ang'ania madaraka hataki kutoka. Naamin wananchi wa kule pia wanabanwabanwa kiainaaina japo nje hatusikii sana kelele (sina uhakika na hili). Hata hivyo kiujumla demokrasia kule ni ndogo
Jamaa ni mdini na naamin ingekuwa ndani ya uwezo wake akina sisi sote angetaka tuwe waislamu. Du.
Wakat huohuo tunasikia shida kule ni kidogo. Naweza kuongea kiujumla kuwa nchi ile ina hali nzur kiuchumi kuliko nchi nyingi hapa afrika. Na kama hili ni kweli hatuwez kuunganisha mafanikio ya libya na uongoz wa gadaf mwenyewe personally.

Waafrika tunataka zaid nin kwanza? Demokrasia au maendeleo? Ni kweli pasipo na demokrasia hakuna maendeleo? Unasemaje kuhusu china? Ni kweli pasipo na uchaguz wa kila baada ya miaka 4 au 5 hamna maendeleo? Mi naona hapana. Zaidzaid hiz chaguz za mara kwa mara zinatulostisha na kutufanya tuwe too dependent on misaada ya nje. Hebu fikiria, kila baada ya miaka mitano mabilion yanatumika kwenye uchaguz. Hizo hela zingetosha kujenga vyuo vingap vya ufundi? Na zingejenga vituo vingap vya afya?
Najua kuna faida ya hiz chaguz za mara kwa mara. Akili mbovu au ya ufisad inatoka na inaingia akili yenye uzalendo na yenye uwezo mzur zaid wa kutatia matatizo yetu. Lakin je, ndivyo inavyokuwa? Uzoefu wetu unaonyesha hivyo hapa afrika? Wapi! Hamna kitu kama hicho. Inakuja timu hii, inatimua timua na kuja ingine kwa gharama kubwa zaid. Nayo inatimiuatimua kabla haijaja ingine. Ndo mtindo wa maisha yetu.
Hii ni demokrasia aghali sana. Inatufanya tuwe alosto na tegemez zaid na zaid

Tatizo letu ni kukopi. Matokeo tunakopi hata visivyo kopika halafu vinatutokea puani

Gadaf anamapunguf yake huenda mengi tu, lakin kama haui raia/wapinzan wake, sion kama ni kiongoz asiyefaa kias hicho

Afrika kila kitu kipo. Afrika inachohitaj ni kiongoz/viongoz wenye nia na uwezo wa kutumia vilivyopo katka nchi zao kuendeleza jamii zao. Nasikia gadaf hilo ameliweza kwa kiwango kikubwa
 
Can't wait for Kagame to take over, the man seems to be a doer, despite his adventure in DRC
 
Kiongozi yeyote asiyetaka kuruhusu mabadiliko ya juu katika uongozi wa nchi yake ni dikteta. Mu7 na Ghadaffi wote ni madikteta ambao hawataki kuachia madaraka. Viongozi kama hawa ni waroho wa madaraka.

Dah, kumbe udikteta unamaana hiyooo?

mimi sina tatizo mtu akikaa madarakani hata miaka mia, muhimu nchi iwe mbele kimaendeleo. hii fikra ya kimagharibi kwamba mtu akikaa madarakani miaka mingi hafai si fikra nzuri kuichukua, japo hupendeza kupokezana madaraka. kuna nchi kibao zinaongozwa kifalme na ufalme hauna kikomo hadi kifo, wao hatusikii malalamiko ya mtu kukaa madarakani muda mrefu habu tuacheni hizo double standards.
 

Mkuu uko sahihi kwa asilimia 101%, mpaka sasa sioni sababu ya kumfanya Gadafi ashindwe kuwa mwenyekiti wa Afrika. So saf ndio kiongozi pekee anayepigania umoja wa Afrika nzima, wengine wanamkwamisha kutokana na uchu wa madaraka. Hata hivyo angalia Blair amekaa madarakani kwa miaka mingapi? Helmut Kohl alikaa kwa miaka mingapi, Masire alikaa ka miaka mingapi? Walikuwa madikteta?? Mbona Bush amekaa kwa miaka 8 tu lakini alikuwa dikteta wa kutisha. Naona tatizo laGadafi kwa wengine ni uarabu wake. So far ukiangalia kati ya wenyeviti wote wa OAU/AU utaona kuwa aliyefanya kazi nzuri kuliko wote ni Idi Amin, kwa hiyo isse ni kudeliver sio style ya kazi
 

Mkuu Bongolander taratibu,mifano unayotoa ya kina Helmut Kohl,Tony Blar ni tofauti kabisa na hali halisi iliyoko Libya.Kwa Mheshimiwa col Gadafi hakuna uchaguzi na kwataarifa yako jamaa anamuandaa mtoto wake kuchukua mikoba yake.Nadhani hili ni tatizo la karibu nchi zote za kiarabu.
Uchumi wa Libya ni mzuri kwasababu ya mafuta na si kwasababu Col Gadafi ni kiongozi bora.
 
.................................................... au sijui kuna kiongozi mwingine anayeweza kufaa hapo??

Kwani Gadaffi ndiye Rais anayefaa kuiongoza Africa kuliko wengine wote?
 
Gaddafi defends Somali pirates!

Addis Ababa, Thursday

AU chairman Muammar Gaddafi has said that his priority will be to claim colonial compensation and to limit the power of Western nations

The Libyan leader further said he believed that piracy was a way of counter defence against the greedy Western nations.

Col Gaddafi expressed the sentiments Thursday morning when he paid his first day official visit to African Union head quarter in Addis Ababa. He addressed AU officials and staff.

Col Gaddafi wore a colourful shirt decorated with Africa Union founding fathers portraits including Tanzanian Julius Nyerere, Ethiopian Haile Selassie, Kenyan Jomo Kenyatta, and Ghanaian Kwame Nkrumah.

During the inaugural tour, Col Gaddafi revealed his plan for the next seasons, saying he doesn’t believe that Somalia piracy was a crime.

“It is a response to greedy Western nations, who invade and exploit Somalia’s water resources illegally,’’ he said.

“It is not a piracy, it is self defence. It is defending the Somalia children’s food,” Col Gaddafi argued.

He pointed out that some countries, particularly Western nations, were penetrating into a Somalia’s sovereign water territory, against the international law .

European, the US and China fleets are entering in the sovereign Somalia territory, because Africa doesn’t have strong and modern defence to push them back, Col Gaddafi said.

Nowadays, Somalis are reacting for justice and trying to defend their country against the unfair exploitation of resources, but Western countries have labelled it as piracy, Gaddafi explained.

The long-serving Libyan leader said he planned to convince other African leaders to claim compensation from colonial masters for their crimes and exploitation during the colonial era.

He disclosed that Libya will this week be claiming quarter billion dollars per year for the next 20 years compensation from Italy.

He said it was a time to ask Western world to pay for Africa’s past suffering and exploitation.

Italian parliament has agreed to pay the money to Libya, he said

Col Gaddafi has refused any invitation from Italy for official visit for the past 40 years as part of his protest and claim.

During my term in AU, I will initiate an organised compensation claim for Africa and I will fight for a greater voice for Africa in the United Nations Security Council.

“If they (Western nations) do not want to live with us fairly, it is our planet and they can go to other planet,” Gaddafi added.

Earlier Col Gaddafi asked for the support and ‘wisdom’ of Tanzanian president Jakaya Mrisho Kikwete, his predecessor, on how to handle the 53-member group’s day-to- day affairs.

Col Gaddafi, who was elected on Monday as a chairman of AU for the next one year, said as the group’s 12th summit ended: “I need the support of my son Kikwete from his wide experience on how to handle AU issues.’’

President Kikwete, who retired from the chairmanship of the AU on Monday, headed the group at one of the most turbulent times during which he played a key role in mediating an end to the post-election violence in Kenya and the election dispute in Zimbabwe.

Had been picked

At the same time, Colonel Gaddafi said he would also seek the advice of former Nigerian President Olusegun Obasanjo on how to deal with the continent’s matters. Col Gaddafi said that Obasanjo was in Addis to meet him.

Earlier, AU chairman Jean Ping said former South African president Thabo Mbeki had been picked by the AU to coordinate its legal matters like the threatened ICC indictment against Sudanese President Omar al-Bashir.

At the press conference, Mr Ping was asked by journalists about his impression about the capability of Col Gaddafi, who took power through a coup close to 40 years ago, to lead a continent where coups are rampant.

Mr Ping said Col Gaddafi was “Elected democratically representing North Africa and it’s a decision of the assembly” .



......ni mwehu lakini sometimes anamake sense,hizo meli nasikia zinaingia Somalia coast either kumwaga garbage iliyojaa sumu au kuiba kwa uvuvi haramu maana inajulikana somalian coast ina samaki na shrimp wengi sana na quality ya juu,western media haisemi ukweli kuhusu hizo meli,na ndio coast ya kushushia silaha na bangi,unga...yaani ni umafia mtupu!
 


Mkuu hauko mbali na ukweli. Demokrasia ya Kimagharibi mara nyingi hazifai kwenye chi za kiarabu demokrasia hhuwa inayumbisha sana nchi za kiarabu mfano mzuri uko Palestina, nchi nyingine ukiangalia kama Jordan, Syria, Lebanon, Saudia nk na hivi karibuni kama ulivyosema Gadafi, na mwingine Mubarak, madaraka wanarithishana, hakuna demokrasia ya kimagharibi lakini kuna stability fulani. naonekana kama ni tatizo lakini ndio political life style ya waarabu
Unajua Nigeria ina mafut kuliko hata Libya, lakini angaliajinsi inavyohangaika na umaskini. Kwa hiyo kuna uwezekano kuwa umaskini unaondoka kutokana na aliyemadarakani anayo-allocate raslimali zilizopo
 
tatizo la africa ni kwamba tumeshapoteza mwelekeo, hakuna fikra sahihi kutoka ndani ya waafrica wenyewe, fikra zote za kiafrika zinatoka Magharibi
madhumuni ya OAU yalikuwa ni ya wazi tu (kulikomboa Bara la Africa) na kweli wale viongozi walikuwa Commited na walifanikisha hilo, tatizo lilikuja pale afrika walipoamua kulibadilisha OAU na kuwa AU, kwa kweli mabadiliko yalikuwa ni ya makaratasi na jina lakini hakukuwa na viongozi commited katika AU kanma walivyokuwa katika OAU, ni viongozi ambao hawana misimamo binafsi acha ya pamoja kama jumuiya,
hivi kweli waafrika wa nigeria wanakufa na umaskini na ni nchi ya kwanza afrika kwa kutoa mafuta lakini kwenye AU hakuna hata kiongozi mmoja anayelizungumzia hilo na hakuna action ya pamoja kama AU kulitatua hilo, wakati wa OAU kama wakiamua wanataka kuikomboa Zimbabwe basi africa nzima ingeunga mkono na kweli Uhuiru ungepatikana, lakini AU inashindwaje kuweka malengo kama hayo ya kuwakomboa watu kiuchumi,lakini ukija kuangalia utakuta viongozi wote wa africa wanafanana issue ya Nigeria ipo Ghana(dhahabu), Congo, DRC, Liberia, Siera leone, TANZANIA, Zambia,Zim almost nchi zote za kiafrica matatizo yanafanana kwa sababu viongozi waliowote wanachukua fikra kutoka upande mmoja(Magharibi)
Gadaffi anaweza kuwa kiongozi mzuri lakini si kwa waafrika wote(labda nchi yake na watu wenye itikadi kama yake) na tatizo kubwa yeye japokuwa yupo africa lakini hayupo tayari kukubali mchanganyiko wa kiafrica, ni kitu cha ajabu kiongozi mkubwa kusimama mbele ya watu tena kwanye nchi ya itikadi tofauti na yake na kutamka kwamba itikadi yake ni bora na itikati zingine zote ni za uongo, ukweli ni kwamba kwa africa vitu ambavyo viko sensitive sana ni DINI na UKABILA, sasa kama wewe ni kiongozi na unaanza kubagua watu kwa itikadi zao inakuwa ni vigumu sana kuwaongoza kwa sababbu hata adui inakuwa ni rahisi kugawa watu
 
Gaddafi ni mmoja katika viongozi wachache wenye uchu ya kuiona Afrika ikiendelea na lakini ubinafsi wa viongozi wengi wa Afrika unafanya wampinge na suala la kufaa au kutofaa hakusema yeye lazima awe rais wa hiyo United States of Afrika.
 

Dikteta si kwa kukaa madarakani muda mrefu, bali ni kwa kukandamiza (suppression) mchakato wa kidemokrasia ambao unaongeza ushindani ktk kuchagua kiongozi mkuu wa kitaifa. Sidhani kama hili lina mjadala.
 
Hakuna mantiki yoyote ya mawazo ya Gadafi kama Gadafi kktk kuleta umoja kwa waafrika. Dhambi yake ni kubwa kiasi kwamba hakuna mtu mwenye akili timamu anayeweza kuyakubali mawazo yake.
Je, ni kweli watanzania wa leo wamesahau jinsi Gadafi alivyomsaidia Idi Amini katika kutaka kuitawala Tanzania?

Ni kiongozi gani anayeweza kuongoza jumuiya hii ya Afrika hali akipuuza hadhari imani za wengine?

Ni lini anaweza kuleta muungano wa kweli hali rohoni akiwa na matabaka tayari?
 
Dikteta si kwa kukaa madarakani muda mrefu, bali ni kwa kukandamiza (suppression) mchakato wa kidemokrasia ambao unaongeza ushindani ktk kuchagua kiongozi mkuu wa kitaifa. Sidhani kama hili lina mjadala.

Mtindio pole sana na huo mtindio unaokunyima uelewa, ukisoma post yangu utaiona ikiwa na paragrafu mbili moja ni yenye mshangao na yapili ni maelezo.

Dah, kumbe udikteta unamaana hiyooo?

mimi sina tatizo mtu akikaa madarakani hata miaka mia, muhimu nchi iwe mbele kimaendeleo. hii fikra ya kimagharibi kwamba mtu akikaa madarakani miaka mingi hafai si fikra nzuri kuichukua, japo hupendeza kupokezana madaraka. kuna nchi kibao zinaongozwa kifalme na ufalme hauna kikomo hadi kifo, wao hatusikii malalamiko ya mtu kukaa madarakani muda mrefu habu tuacheni hizo double standards.
 

Hivi ni NANI mwenye mtindio baina ya mimi na wewe? Kamuulize mtoto wa Ghadafi mwenyewe anayempinga baba yake mzazi kwa udikteta wake.

Najua huna facts unasukumwa na ushabiki ..hivyo endelea maana hivyo ndivyo inavyowafaa watu wenye upeo njiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…