Gambling and betting addiction

Gambling and betting addiction

I’m an addict, yes leo nimekubali kuwa mimi ni addict wa michezo ya kamari. Sikuwa tayari ku accept hili swala na kila siku nilikua najipa moyo nita acha au huenda I will make through gambling and online sports betting.

Nilianza kamari back in 2014 and I blame myself for the addiction to get the best of me. Nimeishi sometimes maisha magumu sana chuoni kwa sababu ya betting which was a sign for me to quit but I didn’t.

Nakumbuka on my university graduation I just wanted that extra cash nika bet budget nzima nilopewa na my parents. I woke up the next morning with 40k with no new clothes or shoes plus a girlfriend to please and take care of for the next three days of the graduation hype, I made it through lakini sito sahau msoto nilopitia.

Fast foward namaliza uni napata kazi nzuri somewhere, I up my stakes to the mounts of 500k-1M. Unajikuta in a weekend unatoa 1M mpaka 3M then next week unatoka from 500k to (-3M) just chasing the losses . The adrenaline was more than that of alcohol or drugs I just wanted to continue sikutaka kuacha hata kidogo.

Had savings somewhere ikanibidi kuvunja account just to keep up with the lifestyle!, that account ilitoka kwenye some Ms mpaka sasa iko na 70k. To keep it short I have made losses, huge losses.

Una deposit 100k ijumaa jioni una bet na ku gamble online vya kutosha unafikisha let’s say 700k. Your mind tells you to withdraw ila una jiambia one last bet, unatafuta live play dakika ya 83 game ni 1-0 unasema hapa ni under 2.5 una stake one last bet of the night the whole 700k, guess what it’s the 94th minute na game imeisha 3-1. Unasema ngoja ni deposit 500k to chase the loss, guess what inaenda pia!!! The cycle continues all month!

Naweza sema I lost myself not my cash in all this facade!! Najiona nimepotea mimi hizi pesa zita tafutwa ila kwa namna kubwa kamari imeniharibia mipango yangu mingi sana.

But I give up now, I call it quits. I have learned my lesson now, ni muda wa ku fight hii addiction.

Day 0 of not placing a bet, here we go.
Hongera kwa kufikia haya maamuzi. Mimi mwenyewe nataka kuachana na huu ushetani. Uteja wa kamari ni mbaya sana zaidi ya hata ya uteja wa drugs , sex na alcohol. Kamari ni pepo la umaskini na sonona.Zamani kabla sijajua huu ushetani nlikuwa nikiwaona wanaobeti kama wamepungukiwa na akili (which is right tbh), siku moja nilikaa mawazo tu ya kishetani yalinijia akilini kunambia beti kwa ajili ya kutafiti. Nliweka pesa nyingi nikabeti , mkeka ukatiki, nikajisemea kumbe naweza kukaa tu home nikaingiza pesa kimasihara....dah kilichofuata ni kuzama ndani ya lindi la uteja. Sijutii pesa nlizopoteza ila najutia sana nafsi yangu kwa kuiingiza kwenye huu uovu. Namuomba sana Mungu anisaidie niweze kuachana na huu uovu.
 
Dah.!
Kwenye nyeto umenigusa mkuu nimeanza kunyetuka tangu 1994 mpaka leo naendelea kila siku nasema nipige cha mwisho niache then najikuta naendelea [emoji1787]
Kuna kipindi nilijikeep busy sana nikafanikiwa kutoboa mwezi ila kilichofuata nilirudi chamani kwa kasi ya 5G
Mkuu wewe ni kiongozi kabisa kwenye hiyo raha jipe mwenyewe,ila acha nyeto mzee ,je ulisha wahi kujichunguza ni kitu gani kinacho sababisha ushindwe kuacha?
 
Vyote hivo nimefanya, ila on a bigger picture hata pale unapo recover loss kwa formula ile ile ambayo unatumia always na bado matokeo yana enda kinyume ina kupa picha gani? Betting matokeo yake hayako pre-planned hivo at any time yanaweza kukuendea kombo.

Una weza kuendelea na betting endapo haiku athiri your mental state na everyday life ila it was different for me that’s why I called it quits.
Betting ruined my mental health to an extent napata depression, anxiety,insomnia etc.

Upande wa kiroho na kiimani pia naiona athari yake sana tena sana.Spiritually i feel empty, tukija katika upande wa kijamii the same, sina muda wa kusocialize na watu wangu wa karibu ...muda wote na concentrate na smartphone yangu tu. Economically, ndio staki hata kuelezea.


Guys ni hivi, ubaya wa gambling ni kuwa umefungua mlango wa tamaa ndani ya nafsi yako.Tusidanganyane kuwa mtu ana bet for fun. Hakuna mwanadamu anaependa kupoteza pesa zake hapa ulimwenguni. Ukweli ni kuwa unabet ili upate pesa zaidi ya ulizonazo. Ili kuacha uovu huu inabidi uwe karibu sana na Mungu,maana tayari shetani ameshakita mizizi ya tamaa ndani ya nafsi yako. Hivyo inahitaji kwanza Will power na pia msaada wa Mungu.

Mungu habadilishi mambo ya mja wake kama huyo mja hayupo tayari kubadilika. Kila la heri kwa wote tulioazimia kuachana na huu utumwa. Pesa unazozipoteza kwenye vambling kama ungelikuwa unazitolea sadaka kwa yatima, wajane wazee,walemavu n.k hakika maisha yako yangelikuwa ya baraka na amani tele.
 
Nimeshakutana na Ex-drug addicts na kubonga nao mara kwa mara.

Wengi huwa wanaeda hospitali kumeza dose ya methadone ambayo kiuhalisia ni kama madawa ya kulevya maana wakimeza ikifika muda huwa wanasinzia kama wamekula unga tu, wengi katikati huwa wanashindwa na kurelapse kwenye matumizi ya drugs.

Ila nikakutana kama na watu wawili hivi ambao nao walikuwa ni drug addicts nikawauliza waliwezaje kuacha.Mmoja alinambia kuwa alipoamua kuwa anaacha alidhamiria moyoni kuwa anaacha moja kwa moja bila ya methadone . Alikubali kupitia maumivu machungu ya kuacha madawa (withdrawal syndrome/arosto). Haikuwa rahisi mwanzoni maana aliumwa sana ila alipiga moyo konde na kuvumilia kama mwaka hivi akaweza kuacha moja kwa moja! Pia alijitahidi kujiweka karibu na Mungu akaanza kufanya ibada na Mungu alimfanyia wepesi kuweza kuacha mpaka hivi leo.

Hapa duniani kwa wale wenye imani wanaamini uwepo wa Mungu, wanajua kuwa kuna pande mbili.Pande ya kulia ni Mungu ambapo anafungamana na matendo mema na upande wa kushoto yupo shetani anaefungamana na matendo yote maovu.

Kazi ya shetani ni kuupamba uovu uonekane mzuri machoni na ndani ya nafsi ya mwanadamu. Hivyo anaipamba hii betting ionekane ni nzuri na kutupa ahadi nyingi za uongo kuwa tutatusua na kuwa matajiri kitu ambacho sio kweli. Wachache sana wamefanikiwa kupitia betting....na kama amefanikiwa kiuchumi basi ukija kuchunguza maisha yake kwa upande wa kiroho na kijamii utakuta ni mabovu sana ndio huyo dada binti kiziwi amesema kuwa huyo jamaa licha ya kuwa na maisha mazuri ila hana hata familia anayokaaa nayo karibu.

Watu wanaobeti hawawezi kufurahia maisha ya ndoa au mahusiano na wake au wanawake zao.Haiwezekani upigwe milioni moja na muhindi halafu urudi nyumbani mood yako iwe sawa.Ni lazima utakuwa tu na hasira za kupoteza na huenda ukahamisha hasira hizo kwa watu wa karibu yako kama mke na watoto.
 
Mungu akutie nguvu kwenye maamuzi haya, naamini ni sahihi kabisa.

Betting/Gambling ya aina yoyote ile ni Uovu kwa Mungu ukiifanya lazima itakuathiri kwa namna moja au nyingine.

Wanaokataa suala lako hawajafikia level za kusema wako addicted, kuwa ns Gambling Disorder ni level ya juu na ndio uliyonayo wewe mkuu.

Nina bet ila sio kama ww mkuu ila nikiri kuna vitu haviko sawa kwangu.
1. Niko busy na simu balaa,niwe home au kazini.
2. Akili yangu ni kama imefungwa kufikiri fursa zaidi za kuwekeza.
3.Siwezi budgeting ya pesa ninazopata.
4.Emotionally na naweza kasirikia nyumba kumbe nimepigwa.

Kiufupi kama hii mambo inakuletea shida ni kuomba kuiepuka kabla hali haijawa mbaya.
 
Wenzio tunabet kutafuta pesa ww pesa unazo mshahara unatema unataka nini tena acha upigwe
 
binafsi sina cha kusema kuhusu betting but mungu anisaidie ni toka 2019 mpaka hii leo nimechakazwa vibaya mmno but tusidanganyane kuacha kamari ni shughuri pevu inahitaji nguvu ya ziada koz nimejiapiza nimeshindwa liapa tarehe 30 december mwisho but ndani ya ya siku kumi nikacheza na nimepoteza si chin ya laki tatu binafsi nimeamua nitengeneze stage za kuacha pili nimejikubali mm nimefeli
 
binafsi sina cha kusema kuhusu betting but mungu anisaidie ni toka 2019 mpaka hii leo nimechakazwa vibaya mmno but tusidanganyane kuacha kamari ni shughuri pevu inahitaji nguvu ya ziada koz nimejiapiza nimeshindwa liapa tarehe 30 december mwisho but ndani ya ya siku kumi nikacheza na nimepoteza si chin ya laki tatu binafsi nimeamua nitengeneze stage za kuacha pili nimejikubali mm nimefeli
Mkuu vipi juve amekuacha salama vibibi vya torini
 
Kwani ukiandika kwa lugha moja kuna tatizo gani?

Kama unaandika kiswahili andika kiswahili na kama umeamua kuandika kingereza andika mwanzo mwisho na sio huo utoto ulioandika hapo
 
I just want to say that I can relate to what you're going through, as I've been there. But believe me, it is possible to get out! Just be strong, and everything will be fine.

Thanks for the positive comment, 8+ months and counting. I’m in a better place honestly niko proud with myself kwa hii step.
 
Kwani ukiandika kwa lugha moja kuna tatizo gani?

Kama unaandika kiswahili andika kiswahili na kama umeamua kuandika kingereza andika mwanzo mwisho na sio huo utoto ulioandika hapo

Sawa.
 
Wiki hii nmebet 1500 nimeliwa yote,sitasahau🥲🥲🥲🥲🥲
 
Avoid,the so called get rich quick schemes(SHERIA YA PILI YA FEDHA KWENYE KITABU CHA RICHEST MAN IN BABYLON KAMA SIKOSEI
 
Back
Top Bottom