Gambling and betting addiction

Hongera kwa kufikia haya maamuzi. Mimi mwenyewe nataka kuachana na huu ushetani. Uteja wa kamari ni mbaya sana zaidi ya hata ya uteja wa drugs , sex na alcohol. Kamari ni pepo la umaskini na sonona.Zamani kabla sijajua huu ushetani nlikuwa nikiwaona wanaobeti kama wamepungukiwa na akili (which is right tbh), siku moja nilikaa mawazo tu ya kishetani yalinijia akilini kunambia beti kwa ajili ya kutafiti. Nliweka pesa nyingi nikabeti , mkeka ukatiki, nikajisemea kumbe naweza kukaa tu home nikaingiza pesa kimasihara....dah kilichofuata ni kuzama ndani ya lindi la uteja. Sijutii pesa nlizopoteza ila najutia sana nafsi yangu kwa kuiingiza kwenye huu uovu. Namuomba sana Mungu anisaidie niweze kuachana na huu uovu.
 
Mkuu wewe ni kiongozi kabisa kwenye hiyo raha jipe mwenyewe,ila acha nyeto mzee ,je ulisha wahi kujichunguza ni kitu gani kinacho sababisha ushindwe kuacha?
 
Betting ruined my mental health to an extent napata depression, anxiety,insomnia etc.

Upande wa kiroho na kiimani pia naiona athari yake sana tena sana.Spiritually i feel empty, tukija katika upande wa kijamii the same, sina muda wa kusocialize na watu wangu wa karibu ...muda wote na concentrate na smartphone yangu tu. Economically, ndio staki hata kuelezea.


Guys ni hivi, ubaya wa gambling ni kuwa umefungua mlango wa tamaa ndani ya nafsi yako.Tusidanganyane kuwa mtu ana bet for fun. Hakuna mwanadamu anaependa kupoteza pesa zake hapa ulimwenguni. Ukweli ni kuwa unabet ili upate pesa zaidi ya ulizonazo. Ili kuacha uovu huu inabidi uwe karibu sana na Mungu,maana tayari shetani ameshakita mizizi ya tamaa ndani ya nafsi yako. Hivyo inahitaji kwanza Will power na pia msaada wa Mungu.

Mungu habadilishi mambo ya mja wake kama huyo mja hayupo tayari kubadilika. Kila la heri kwa wote tulioazimia kuachana na huu utumwa. Pesa unazozipoteza kwenye vambling kama ungelikuwa unazitolea sadaka kwa yatima, wajane wazee,walemavu n.k hakika maisha yako yangelikuwa ya baraka na amani tele.
 
Nimeshakutana na Ex-drug addicts na kubonga nao mara kwa mara.

Wengi huwa wanaeda hospitali kumeza dose ya methadone ambayo kiuhalisia ni kama madawa ya kulevya maana wakimeza ikifika muda huwa wanasinzia kama wamekula unga tu, wengi katikati huwa wanashindwa na kurelapse kwenye matumizi ya drugs.

Ila nikakutana kama na watu wawili hivi ambao nao walikuwa ni drug addicts nikawauliza waliwezaje kuacha.Mmoja alinambia kuwa alipoamua kuwa anaacha alidhamiria moyoni kuwa anaacha moja kwa moja bila ya methadone . Alikubali kupitia maumivu machungu ya kuacha madawa (withdrawal syndrome/arosto). Haikuwa rahisi mwanzoni maana aliumwa sana ila alipiga moyo konde na kuvumilia kama mwaka hivi akaweza kuacha moja kwa moja! Pia alijitahidi kujiweka karibu na Mungu akaanza kufanya ibada na Mungu alimfanyia wepesi kuweza kuacha mpaka hivi leo.

Hapa duniani kwa wale wenye imani wanaamini uwepo wa Mungu, wanajua kuwa kuna pande mbili.Pande ya kulia ni Mungu ambapo anafungamana na matendo mema na upande wa kushoto yupo shetani anaefungamana na matendo yote maovu.

Kazi ya shetani ni kuupamba uovu uonekane mzuri machoni na ndani ya nafsi ya mwanadamu. Hivyo anaipamba hii betting ionekane ni nzuri na kutupa ahadi nyingi za uongo kuwa tutatusua na kuwa matajiri kitu ambacho sio kweli. Wachache sana wamefanikiwa kupitia betting....na kama amefanikiwa kiuchumi basi ukija kuchunguza maisha yake kwa upande wa kiroho na kijamii utakuta ni mabovu sana ndio huyo dada binti kiziwi amesema kuwa huyo jamaa licha ya kuwa na maisha mazuri ila hana hata familia anayokaaa nayo karibu.

Watu wanaobeti hawawezi kufurahia maisha ya ndoa au mahusiano na wake au wanawake zao.Haiwezekani upigwe milioni moja na muhindi halafu urudi nyumbani mood yako iwe sawa.Ni lazima utakuwa tu na hasira za kupoteza na huenda ukahamisha hasira hizo kwa watu wa karibu yako kama mke na watoto.
 
Mungu akutie nguvu kwenye maamuzi haya, naamini ni sahihi kabisa.

Betting/Gambling ya aina yoyote ile ni Uovu kwa Mungu ukiifanya lazima itakuathiri kwa namna moja au nyingine.

Wanaokataa suala lako hawajafikia level za kusema wako addicted, kuwa ns Gambling Disorder ni level ya juu na ndio uliyonayo wewe mkuu.

Nina bet ila sio kama ww mkuu ila nikiri kuna vitu haviko sawa kwangu.
1. Niko busy na simu balaa,niwe home au kazini.
2. Akili yangu ni kama imefungwa kufikiri fursa zaidi za kuwekeza.
3.Siwezi budgeting ya pesa ninazopata.
4.Emotionally na naweza kasirikia nyumba kumbe nimepigwa.

Kiufupi kama hii mambo inakuletea shida ni kuomba kuiepuka kabla hali haijawa mbaya.
 
Wenzio tunabet kutafuta pesa ww pesa unazo mshahara unatema unataka nini tena acha upigwe
 
binafsi sina cha kusema kuhusu betting but mungu anisaidie ni toka 2019 mpaka hii leo nimechakazwa vibaya mmno but tusidanganyane kuacha kamari ni shughuri pevu inahitaji nguvu ya ziada koz nimejiapiza nimeshindwa liapa tarehe 30 december mwisho but ndani ya ya siku kumi nikacheza na nimepoteza si chin ya laki tatu binafsi nimeamua nitengeneze stage za kuacha pili nimejikubali mm nimefeli
 
Mkuu vipi juve amekuacha salama vibibi vya torini
 
Kwani ukiandika kwa lugha moja kuna tatizo gani?

Kama unaandika kiswahili andika kiswahili na kama umeamua kuandika kingereza andika mwanzo mwisho na sio huo utoto ulioandika hapo
 
I just want to say that I can relate to what you're going through, as I've been there. But believe me, it is possible to get out! Just be strong, and everything will be fine.

Thanks for the positive comment, 8+ months and counting. I’m in a better place honestly niko proud with myself kwa hii step.
 
Kwani ukiandika kwa lugha moja kuna tatizo gani?

Kama unaandika kiswahili andika kiswahili na kama umeamua kuandika kingereza andika mwanzo mwisho na sio huo utoto ulioandika hapo

Sawa.
 
Wiki hii nmebet 1500 nimeliwa yote,sitasahau🥲🥲🥲🥲🥲
 
Avoid,the so called get rich quick schemes(SHERIA YA PILI YA FEDHA KWENYE KITABU CHA RICHEST MAN IN BABYLON KAMA SIKOSEI
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…