The Supreme Conqueror
JF-Expert Member
- Feb 13, 2017
- 609
- 1,584
Maisha yetu yamefichwa katika kesho nyingi tusizozijua wala kuzitarajia.
Una rafiki yako kipenzi unayeamini kuwa ndiye rafiki yako wa dhati? Usiwe mwepesi kumuamini kwa macho, wewe uachie muda nafasi ukudhibitishie yupi ni rafiki wa dhati na yupi ni rafiki wa maslahi na yupi ni adui yako msaliti aliyejificha katika kichaka cha urafiki.
Hatuumizwi na kusalitiwa na maadui zetu, bali tunaumizwa na kusalitiwa na watu tuliowaruhusu kuingia kwenye maisha yetu tukiamini kuwa ni marafiki zetu.
Adui wa mtu ni mtu tena yule wa karibu yako ndiye adui yako. Naam kikulacho ki nguoni mwako ndugu yangu.
Ishi katika uso wa Dunia hii ukijua kuwa hakuna rafiki wa kudumu lakini kuna maslahi ya kudumu.
Rafiki yako wa leo ndiye adui yako wa kesho. Na ukichunguza vizuri, wengi wa maadui wako wakubwa wa leo waliwahi kuwa marafiki zako wakubwa jana.
Unayempambania, kumpigania na kumtia moyo Leo, ndiye atakayepambana kukuangusha, atakayepigana kinyume chako na atakayekuvunja moyo kesho.
Acha kuwa mwepesi kumuamini mtu, upe muda nafasi ukusaidie kufanya kazi hiyo.
Picha hii ni mfano halisi wa maisha yetu dhidi ya marafiki zetu wa jana na leo waliogeuka maadui zetu na wasaliti wa maisha yetu kesho. Picha hii ni mfano halisi wa urafiki na usaliti.
Itunze picha hii na kila mara unapotaka kumuamini mtu au kumpa cheo adhimu cha urafiki itazame picha hii kisha ushauri moyo.
Picha hii ilipigwa mwaka 2018 hapa ni aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakati huo Mrisho Gambo alipomtembelea rafiki yake wa dhati nyumbani kwake aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati huo Paul Makonda kwa minajili ya kumjulia hali.
Leo 2025 sidhani kama wawili hawa kuna anayeweza kudhubutu kunywa maji kwa mwenzake. Ni heri kufa na kiu kuliko kunywa maji malangoni mwa mtesi wako.