>>>>>>EPISODE : 06<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 06
Whatsapp
call/Text:+255687409189
(Audio version ya story coming soon)
*************************************
Previously on GAMBOSHI...
ILIPOISHIA,,,
"Nya- nge-taaaaaa lala chini" ilisikika sauti ya inspecta Dotto huku akipiga risasi,,,,,,
Sehemu ya 06
Sasa endelea,,,,,
kadhaa kuelekea upande wa Kangina( yule mtu mwenye macho mekundu)
Wote waligeuka ghafla na kumuona inspecta Dotto akija mbio huku akiendelea kumimina risasi ambazo zilikua zinadunda tu kwenye mwili wa Kangina na haikuonyesha kuleta madhara yeyote kwenye mwili wake, risasi moja ilidunda vibaya na kumrudia na kumpiga inspecta Dotto kwenye bega la kushoto na kuanguka chini huku damu zikianza kumbubujika, Nyangeta alimfuata mbio na kumshika mkono, huku akijaribu kumkalisha chini
"Dotto umefikaje huku?!?"
"Nilikuona muda unaondoka so nilikuja kama back up yako, ila ... Inaonekana kila kitu umekicontrol!" Aliongea Inspecta Dotto kwa shida huku akitokwa na damu nyingi,
"Nyangeta inabidi twende muda umeisha" aliongea yule msichana huku akichuchumaa alipo inspecta Dotto,
"Siwezi kumuacha hapa akiwa katika hali hii, inabidi aende Hospitali haraka wacha nipigie ambulance" aliongea nyangeta huku akishika simu yake ambayo ilikua kwenye mfuko wa koti lake,
"Nyangeta hawa ni wakina nani?" mbona wanamavazi ya ajabu?" aliuliza Dotto huku akijikongoja kutaka kuamka
"daah, ni story ndefu na yaajabu" alijibu nyangeta huku akimshikilia.
Nyangeta alijaribu kupiga simu yake lakini ilishindikana kutokana na ubovu wa mtandao katika eneo lile,
"Acha mimi nimpeleke hospitali" aliongea yule msichana mdogo.
"Nyangeta ...hawa ni wakina nani?, usiwaamini... wamemuua Dereva Taxi wako...koh ..koh!" Aliongea inspeta Dotto huku akikohoa.
"Nini!?" Aliuliza nyangeta kwa hasira huku akimgeukia yule msichana,
"Ohoo Kumbe, tunatakiwa tuondoke haraka, Minza mpeleke" aliongea yule msichana huku akisimama,
"Ampeleke wapi!!!??? Wauaji wakubwa nyie, !?!" Alihamaki Nyangeta huku akisimama, na kushika bastola yake tena, kabla hajafyatua risasi,
Yule mdada alinyoosha vidole viwili juu na kufanya ishara kama anamuita nyangeta, palepale Nyangeta alijikuta ananyanyuka juu na kuvutwa hewani bila kushikwa na kitu chochote kuelekea alipo yule msichana ambaye kwa sasa alionekana hataki mzaha kwa wakati huo, Nyangeta alikua anapiga kelele kwa nguvu huku hofu ikiwa imemjaa moyoni mwake, akiwa hewani alianza kuishiwa nguvu taratibu na alianza kuona giza na kupoteza fahamu palepale.
******
Nyangeta alifumbua macho na kujikuta amelala kwenye kitanda kikubwa kizuri, aliamka na kuketi kitandani huku akishangaa sehemu aliyokuwepo, ndani ya chumba kile kikubwa kwa pembeni kushoto kulikua na meza yenye kioo kikubwa cha kujitazama, juu ya ile meza kulikuwa na bunduki yake pamoja na waleti yake pembeni ya ile meza kulikuwa na kiti kidogo chakwa mbao, kwa upande mwingine wa chumba kile kulikua na madirisha makubwa yaliyokua yamefunikwa na mapazia meupe ambayo yalipepea taratibu, chumba kile kilirembwa vizuri upande wa juu kwa marumaru za dhahabu na sakafu yake ilikua kama kioo kwa jinsi ilivyokua inang'ara.
Nyangeta alijiangalia na kujiona akiwa kwenye mavazi tofauti na alivyovaa mwanzo, alikua amevalishwa gauni zuri kama la mtoto wa kifalme, gauni hilo la silk likiwa na rangi nyeupe lilikua limedariziwa vizuri kwa vito vya dhahabu, hakika gauni lile lilionekana ni zuri sana na pia lilikua linaonekana ni la gharama kubwa.
Akiendelea kushangaa na kupepesa macho kwenye kile chumba, macho yake yalitua moja kwa moja kwa msichana mrembo ambae alikaa kwenye kiti mbele yake huku akiwa anatabasam.
"Hatimaye umeamka... Pole sana kwa uchovu wa usingizi" aliongea msichana yule akiwa anatabasamu
"Asante, wewe ni nani? Na hapa niko wapi!?" Aliongea nyangeta kwa shauku huku akimuangalia yule msichana kwa wasiwasi,
"Usiogope Nyangeta, uko katika mikono salama kabisa" alijibu msichana yule huku akisimama na kumsogelea Nyangeta.
"Alafu... Nakujua wewe nilishawahi kukuona sehemu" aliongea nyangeta huku akimuangalia kwa makini yule msichana
"Hahahhaha" yule msichana alicheka kidogo kicheko cha kistaarabu,
"Ndio tulionana jana asubuhi"
Aliongezea yule msichana
"Yes nimekumbuka, nilikuona kituoni ulienda kuulizia kuhusu ajali iliyotokea"
"Haswaa tulionana pale mlangoni, na tulisalimiana vizuri sana"
"Ok, bila shaka wewe ndio uliniandikia ule ujumbe, haya naomba uniambie hapa niko wapi? Nimefikaje? Wewe ni nani, na wale walio niteka ni wakina nani.... Alafu! Dotto yuko wapi na anaendeleaje?" Aliuliza nyangeta maswali mengi kwa mfululizo huku akikaa kwenye kitanda
"Sasa nianze kujibu lipi maana dah! maswali mengi!" Alijibu yule msichana huku na yeye akikaa kitandani,
"Dotto yuko wapi?"
"Aliwahishwa hospitali, hali yake ni nzuri na nafikiri ataishi!"
"Wewe ni nani na hapa ni wapi?"
"Mimi naitwa Marietukan Ti Ng'wana Ng'humbu, japo watoto wangu wananiita Mariet au Mama" alijibu yule msichana kwa upole huku akimpa
Mkono Nyangeta
Nyangeta na yeye alimpa mkono kama ishara ya kusalimiana, Mariet aliamka na kusogea dirishani na kusimama
"Samahani watoto wangu walikubeba bila ridhaa yako lakini ni kutokana na muda wa kuwepo kwenye ulimwengu wa binadam wa kawaida uliwaishia na pia hatari ilizidi baada ya wewe kuja na mpenzi wako wakati ujumbe ulisema usije na mtu" aliongea Mariet huku akimgeukia Nyangeta huku akitabasamu kidogo,
"Dotto sio mpe.... Anyway, umesema ulimwengu wa kawaida kwani huku ni wapi?" Aliongea nyangeta kwa kuhamaki na uoga ulianza kumuingia, huku akishuka kitandani na kumsogelea Mariet,
"Haha... Nyangeta ...karibu GAMBOSHI" aliongea Mariet huku akifungua mapazia ya dirisha na kuonyesha taswira ya nje,
Kupitia dirishani pale Nyangeta aliweza kuona mji wa Gamboshi ambao ulikua ni mji mzuri ambao hajawahi kuuona maishani mwake, wakazi wa Gambioshi walionekana kuwa na furaha, barabara nzuri zilizojengeka vizuri za lami juu na chini (Fly Over), watu mbalimbali wakiwa wamepanda fisi wakubwa walipita ikiwa kama moja ya usafiri barabarani, kwa juu angani aliona watu wakiwa wamepanda nyungo za aina tofautitofauti wakipaa, huku wameshikilia singe kama usukani wa kuendeshea nyungo zile. Kwa mbele kidogo aliona magorofa makubwa kama yale yaliopo New york cit marekani, na nyumba nyingi nzuri zilizojengwa vizuri, ama kwa hakika mji ule ulipendeza sana ijapokua mambo mengi yalikua yakistaajabisha.
"Watoto watakupeleka ukatembee baadae " aliongea Mariet kwa ukarimu mkubwa baada ya kumuona nyangeta akiduwaa kuutazama uzuri wa mji ule,
"Oooh no...Nipo kuzimu...!!!" Aliongea nyangeta kwa sautimaana ndogo, huku akiwa anaendelea kuduwaa akiushangaa ule mji
" hahahah... Hapana, Haupo kuzimu Nyangeta, kuzimu ni kulee... barabara ile ndio umeiona? ukiifuata ile barabara ndio inakupeleka huko, japo usije ukaenda kule sio pazuri! ... Hapa ni Gamboshi" aliongea Mariet kwa msisitizo huku akimuonyesha nyangeta barabara iliyopo nje kidogo ya mji,
"Uko tayari nikakutambulishe kwa familia?!?" Aliuliza marieta huku akimgeukia Nyangeta
"Hebu niambie kwa nini nipo hapa?" Aliuliza Nyangeta huku akihamaki
"Hilo tutakueleza ila kwanza inabidi ukutane na familia nzima"
"Ok sawa," alijibu nyangeta huku akitikisa kichwa
Mariet alimshika mkono nyangeta na kuongozana nae, wakatoka nje ya mlango.
Walipotoka kwenye kile chumba Nyangeta akiwa na wasiwasi mkubwa moyoni mwake, walipita kwenye korido kubwa iliyokua imepambwa vizuri, huku kukiwa na milango ya vyumba vingine, walikwenda bila kuongea neno lolote mpaka mwisho wa korido ile, ambapo mwishoni kulikua na ngazi za kisasa zilizokuwa zinaelekea chini ambapo ilionekana kama ni sebule ya nyumba ile ambayo ilikua ni nzuri sana na kubwa sana kama hekalu la kifalme,
Walishuka zile ngazi huku Mariet akimuangalia usoni Nyangeta huku akitabasamu kwa mbali,
"Polepole Nyangeta hizi ngazi huwa zinateleza"
Nyangeta hakujibu kitu na kuendelea kushuka mpaka mwisho wa ngazi na kutokezea kwenye ile sebule ambapo kulikua na watu kama watatu waliokua wamekaa kwenye makochi mazuri makubwa , Nyangeta alisimama kwa kusita sita huku akiwaangalia wale watu ambao kila mmoja alikua Anafanya mambo yake.
"Usiogope Nyangeta" Mariet alimwambia huku akimuangalia usoni kwa ukarimu, akawageukia wale watu waliokaa,
"Jamani mgeni wetu ameamka mje mumsalimie." Aliongea Mariet akiwaambia wale watu huku akienda kwenye yale makochi,
"karibu ukae, mbona unasimama mbali," aliongezea Mariet huku akimuangalia Nyangeta,
Nyangeta kwa taratibu alienda na kukaa kwenye moja ya makochi yale yaliyowekwa kwa utaratibu mzuri,
Nyangeta baada ya kukaa aliwaangalia wale watu na kumtambua mmoja wao ambaye alikua ni yule kijana mkubwa aliyemuona kule kwenye mti wa mbuyu, mwingine alikua ni bibi mzee kikongwe akionekana kama ana umri wa miaka 70 hivi, yule mtu wa tatu alionekana ni mvulana mdogo mwenye umri kati ya miaka 12 mpaka kumi na 14.
"Wengine wako wapi? " Mariet alimuuliza yule kijana mkubwa huku akiketi,
"Minza atakua chumbani kwake, kangina alikua jikoni, ....Kanginaaaa" alijibu yule kijana huku akimuita kwa nguvu Kangina,
"Naaaaam!, namalizia nakuja" ilisikika sauti kutokea kwenye chumba kingine karibu na sebule ile.
Yule kijana mdogo alimuangalia Mariet huku akifanya ishara za mikono kama bubu akimwambia mariet jambo fulani.
"Haaaa kumbe ndio anachofanya!" Aliongea mariet huku akionekana kukasirika,
"Joram hebu muite... Na umwambie aje nacho" Mariet aliongea huku akiwa amekasirika,
Yule kijana alinyanyua vidole viwili akashika kichwa chake na kufumba macho, alionekana kama anawasiliana na mtu kwa kutumia fikra zake (telepathicaly).
Ghafla kwa kasi kama ya risasi alikuja msichana mdogo na kusimama katikati yao huku akiweka mikono nyuma,
Nyangeta alistuka sana akataka kukimbia lakini alijizuia kutikana na hakujua wapi pa kukimbilia, alimuangalia yule binti mdogo na kumkumbuka, wale watu wengine walionekana kuwa hawana wasiwasi huku yule bibi akimuangalia nyangeta bila ya kupepesa macho na kumfanya akose amani,
"Unaficha...!!!?!? Si nilikukataza kushika vitu vya watu?" Aliongea Mariet huku akimuangalia yule msichana
"Haraka rudisha kitu cha watu" aliongea Mariet huku akionekana kukasirika,
Yule msichana akatoa simu ya Nyangeta huku ikiwa inaonyesha alarm ya low betry, aliitoa na kumpa nyangeta huku akiwa na wasiwasi,
"Na uombe msamaha" aliongezea Mariet
"Samahani" aliongea yule binti kwa sauti ya uoga, Nyangeta aliipokea huku akijibu,
"Usijali mwaya....!" Yule msichana aligeuka na kwenda kukaa kwenye kiti, kwa upande ule wa ngazi kwa pembeni kidogo alitokea mvulana mwingine mkubwa akiwa na mwili uliojazia kama anafanya mazoezi ya kutunisha misuli huku akiwa ameshika sahani iliyojaa nyama iliyokua inanukia vizuri, akiwa ameongozana na yule binti ambaye na yeye alikuwako kwenye mti wa mbuyu, yule kijana alimsogezea Nyangeta stuli ndogo na kuiweka ile sahani juu kishana alimkaribisha kwa sauti ya upole na ukarimu,
"Karibu chakula, najua unanjaa, ... Huyu nilimuua mwenyewe na kumchuna mwenyewe, nimekuchagulia mguu alikua na mafuta kwelikweli" aliongea yule kijana akijisifia huku akimsogezea Nyangeta,
"aaah...! Asante sana...!!!" Alijibu huku akirudi nyuma kwa woga,
Watu wote walikua wakimuangalia,
"Haina sumu, si unaona..." Aliongea yule kijana huku akichukua kipande kimoja na kukitia mdomoni.
"Anahisi ni nyama ya mtu ndio maana anaogopa" aliongea Joram yule kijana mwingine
"Ooh...! hapana sio nyama ya mtu, sisi hatuli nyama za watu, hii ni nyama ya ng'ombe na Kangina alikua anampenda kweli huyo ng'ombe wake ila amemtoa kwa ajili yako" aliongea yule binti mkubwa.
"Hebu ngoja kwanza...! Mbona siwaelewi naona mnanifanyia vituko tu... Ukarimu mwingiii ambao sielewi mwisho wake ni nini..! " aliongea nyangeta kwa kuhamaki,
" hebu niambieni nyie ni wakina nani na kwa nini mmenileta huku,,,,,,,ITAENDELEA
USIKOSE EPISODE 07
©Copyright "haki zote zimehifadhiwa"