Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Weka stori yako katika uzi mmoja na si kila kipande unakianzishia uzi.Asante sana kwa kusapoti kazi hii, utangulizi upi huo hebu nifahamishe
Je, unapata shida yoyote kwenye utafutaji wa episode za story hii,? Ningependa kukujulisha kuwa story hii itapatikana kila siku kwenye jukwaa kuu la "entertainment" kama unapata changamoto kwenye utafutaji wa episode nijulishe kwa msaada zaidiWeka stori yako katika uzi mmoja na si kila kipande unakianzishia uzi.
JINA LA STORY: GAMBOSHI>>>>>>>EPISODE : 05<<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI>>>>>>EPISODE : 06<<<<<<<<
JINA LA STORY: GAMBOSHI>>>>>>EPISODE : 07<<<<<<<<<
Mbona haiendelei??JINA LA STORY: GAMBOSHI
(Malkia wa wachawi)
MTUNZI: MOSSES AGREY
SEASON : 01
EPISODE: 07
ILIPOISHIA,,,,,,,,,,
" aliongea yule kijana akijisifia huku akimsogezea Nyangeta,
"aaah...! Asante sana...!!!" Alijibu huku akirudi nyuma kwa woga,
Watu wote walikua wakimuangalia,
"Haina sumu, si unaona..." Aliongea yule kijana huku akichukua kipande kimoja na kukitia mdomoni.
"Anahisi ni nyama ya mtu ndio maana anaogopa" aliongea Joram yule kijana mwingine
"Ooh...! hapana sio nyama ya mtu, sisi hatuli nyama za watu, hii ni nyama ya ng'ombe na Kangina alikua anampenda kweli huyo ng'ombe wake ila amemtoa kwa ajili yako" aliongea yule binti mkubwa.
"Hebu ngoja kwanza...! Mbona siwaelewi naona mnanifanyia vituko tu... Ukarimu mwingiii ambao sielewi mwisho wake ni nini..! " aliongea nyangeta kwa kuhamaki,
" hebu niambieni nyie ni wakina nani na kwa nini mmenileta huku"
SASA ENDELEA,,,,,
Nyangeta aliongea huku akijipapasa kiunoni na kugundua bunduki yake aliiacha chumbani,
"Usiogope nyangeta" aliongea Mariet huku akiwaonyesha ishara ya kwenda kukaa Wale waliosimama,
" uko katika mikono salama kabisa," aliongezea Mariet huku akikaa vizuri na wote wakiwa wameketi wakimuangalia Nyangeta.
"Mimi kama nilivyojitambulisha awali, ninaitwa Marietukan, na huyu ni Mama yangu, Ng'humbulian, au unaweza ukamuita Nyanya," aliongea Mariet huku akimuonyeshea kidole yule bibi mzee,
"Yani wewe ni mzuri kama mama yako, masikini aliondoka mapema sana"aliongea yule bibi mzee kwa huzuni huku akipigapiga kofi chini kwenye sakafu kwa mkono wake wa kulia na wakushoto akiuweka kifuani, Na wote walifanya hivyo,
Nyangeta alimuangalia yule bibi huku akishangaa
"huyu ndio binti yangu mkubwa anaitwa Pagilian.." Aliongea mariet huku akimuonyesha yule binti mkubwa,
"Samahani kwa kukuchukua bila ridhaa yako sikua na njia nyingine" aliongea yule binti,
Nyangeta alitikisa kichwa ishara ya kukubali,
"Na huyu ni Kangina ndio mpishi wetu hapa ndani, najua ulikutana nae kabla akiwa katika ile hali yake nyingine" aliongea Mariet akimuangalia yule mvulana aliyekua anamkaribisha chakula Nyangeta,
"Karibu sana japo umegoma kula chakula changu" aliongea Kangina,
Kwa kutabasamu, Nyangeta aliangalia ile sahani ya nyama na kuchukua kipande kimoja na kuanza kukitafuna, hakika nyama ile ilikua tamu ajabu,
"Mmh, mbona tamu sana unajua kupika!" Aliongea nyangeta,
"Asante sana..." Alijibu kangina huku akiinamisha kichwa chake ishara ya kukubali pongezi zile,
"Haya tuendelee, huyu anaitwa Joram, anawafuatia hawa wawili, halafu hawa wawili ni mapacha huyu Anaitwa Minza na huyu anaitwa Mbitian, nae pia ulikutana nae japo kwa hali tofauti... Huyu ni Bubu hana uwezo wa kuongea hivyo anaongea kwa ishara" aliongea Mariet huku akiwaonyesha kwa vidole , Joram na Minza walinyanyua mikono na kumpungia Nyangeta huku wakitabasamu,
Mbitian alinyoosha mikono yake na kufanya ishara fulani, wote wanaangua kicheko kasoro yule bibi mzee ambae muda wote alimkodolea macho Nyangeta.
"Mbona mnanicheka..!" Aliuliza nyangeta akiwa haelewi kinachoendelea,
"Hahaha, Mbiti anasema wewe ni mzuri na anataka kukuoa!" Aliongea Mariet huku akiendelea kucheka,
Nyangeta alimgeukia Mbiti na kutabasam.
"Ngoja kwanza, uliniambia hapa ni mji wa wachawi kwa hiyo nyie wote ni wachawi!?!" Aliuliza nyangeta kwa ujasiri, huku akiwa na wasiwasi moyoni mwake,
"Ndio, huu mji haingii mtu yoyote kama sio mchawi au hana chimbuko la kichawi.. Sisi wote ni wachawi" alijibu Mariet huku akimuangalia usoni,
"Sisi ni wachawi lakini wote tuna uwezo tofauti, sisi ni wachawi wa asili kabisa yani uchawi tumezaliwa nao ni tofauti kabisa na wachawi unaowafahamu wewe au uliowahi kuwasikia, uwezo nilio nao mimi ni tofauti na wengine yani kila mmoja anauwezo wake ambao haufanani na mwingine
Kwa mfano,
Mbitian anauwezo wa kubadilika kuwa kiumbe chochote ambacho kina uhai, na ndio maana ulipomuona alikua kwenye umbo la fisi, anapenda sana umbo hilo" aliongea huku akimuonyesha kidole Mbitian ambae ghafla alibadilika na kugeuka kuwa Fisi mkubwa, kisha alirudi tena kua binadamu.
"Minza uchawi wake yeye ni anauwezo wa kukimbia kwa kasi sana na bila kuchoka, ndio alimpeleka mpenzi wako hospitali," aliongezea mariet huku akimuangalia minza ambae aliondoka kwa kasi ya ajabu, kama sekunde mbili alikua amerudi na kumkabidhi nyangeta bunduki yake ambayo aliiacha chumbani, nyangeta alipigwa na butwaa mdomo ukiwa wazi,
"Sio mpenzi wangu"aliongea Nyangeta
"Joram anauwezo wa kujua mawazo yako yani anaona unachokifikiria pia ana uwezo wa kukuamrisha ufanye kitu bila ridhaa yako na ukafanya kwa kutumia mawazo yake"Mariet aliongezea huku akimuonyesha Joram ambaye alishika kichwa chake kwa vidole viwili na kufumba macho, hapohapo mkono wa Nyangeta ulinyanyuka ukiwa umeshika ile bunduki na kuelekezea kwenye kichwa chake, Nyangeta alijaribu kuurudisha lakini hakuaa na mamlaka kwenye mkono wake.
" hey joram tafadhali.... Basi nimeshajua uwezo wako" aliongea Nyangeta huku akitoa macho na kutetemeka kwa hofu, ghafla mkono wake ulirudi chini.
"Hahaha, haya na huyu Kangina yeye nafikiri unajua uwezo wake anabadilika kuwa kama ulivyomuona na pia ananguvu za ajabu sana" aliongezea Mariet huku akimkazia macho kangina, ambaye ghafla macho yake yaligeuka kuwa mekundu yanayowaka kama taa alafu yakarudi kuwa kawaida,
"pia anauwezo wa kuongezeka umbo na kuwa futi kama kumi na nane au ishirini hivi" aliongezea Mariet,
"Pagiliana anauwezo wa kuongoza kila kitu, na pia anauwezo wa kuwa zaidi ya mtu mmoja...ya..." kabla hajamaliza alitokea pagilian mwingine akishuka kutoka kwenye ngazi huku akiwa na walet ya Nyangeta ambayo nayo aliiacha chumbani, yule pagilian alikuja na kumletea ile walet Nyangeta na kumpa mkononi kisha akaenda akasimama kando na kupotea kama hewa.
"Wewe je !?" Aliuliza nyangeta huku akimuangalia Mariet
"Subiri mbona unaharaka" aliongea mariet huku akinyoosha mkono wake wa kushoto kuelekea jikoni, ambapo mkono ule ulirefuka moja kwa moja na kwenda mpaka jikoni, ulibeba jagi la maji na mkono ule ukarudi ukiwa na jagi mkononi., nyangeta alifumba macho huku akistaajabu aliyoyaona,
"Na mama yangu yeye pia uwezo wake ni kuona hatari zote ambazo zinakuja yani anaweza kuona jambo kabla halijatokea. Pia anaweza kukuonyesha mambo yaliyopita na pia yajayo. Na pia anauwezo wa kukuonyesha kitu chochote anachotaka yeye," aliongeza Mariet,
Yule bibi alinyanyua mkono wake huku akitetemeka kwa uzee huku akumuonyesha Nyangeta,
"Nenda ukajaribu anataka kukuonyesha kitu" aliongea Mariet,
Nyangeta aliamka na kwenda kumshika mkono yule bibi.
Alipo mshika hakuna kitu chochote kilichotokea, wote walikaa vizuri Na kushangaa,
"Nini kimetokea?" Aliuliza Kangina kwa mshangao,
"Mama uko sawa!?" Aliuliza Mariet huku akisimama na kwenda kumshika mabegani yule bibi,
"Yuko sawa ila kuna kitu kina mzuia kufanya uchawi wake kwenye mwili wa Nyangeta" aliongea Joram
"Kweli kuna kitu kina nizuia, kuna kitu umevaa shingoni" aliongea bibi Ng'humbulian, huku akimuangalia Nyangeta kifuani,
Nyangeta alibaki ameduwaa, mariet alimfunua kidogo maana ile nguo aliyovaa ilimfunika mpaka shingoni,
Nyangeta alikua amevaa rozali ambayo yeye alikua anaona ni rozali ya kawaida lakini kwa upande wa wale wachawi ilikua inang'aa kama jua na ilikua inawachoma macho,
" hili ni nini!?!" Aliongea Mariet huku akiangali pembeni,
"Ni Rozali" alijibu nyangeta huku akiiangalia,
Mariet alimsogelea huku akijikaza alitaka kuishika na kuitoa shingoni mwa Nyangeta, ilimuunguza kwa moto mkali sana na kumuachia Jeraha kubwa sana, aliiachia na kuanguka chini.
Wote walimkimbilia mama yao huku wakimsogeza Nyangeta pembeni,
"Mama..."
"Mama..."
"Mariet..." ,,,,,,,ITAENDELEA
SIKOSE SEHEMU YA 08
[emoji2398]Copyright "haki zote zimehifadhiwa"
View attachment 2868880