Gamondi, Nabi hawana uwezo ila tunaojua soka la bongo tunajua nguvu za giza zinavyotumika kuwafanya waonekane bora

Leonel Ateba Mbinda

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2023
Posts
644
Reaction score
2,695
Hakuna cha ubora wa nini, iweje Bangala na Feitoto waonekane wachezaji wa kawaida tu wakiwa azam wakati walipokuwa Yanga walikuwa mastaa na walikuwa wanaupiga mwingi.

Leo Feitoto na Bangala wanaonekana wazito na hawana mvuto, ilhali Gamondi anaonekana mtaalamu kuliko Nabi.

Huyo huyo Gamondi mpeleke akafundishe JKT Ruvu halafu Kocha wa Ruvu aende Yanga bado Yanga itashinda tu.

Kuna nyota wanatembelea Yanga ambayo haihusiani na masuala ya kiufundi, ndio maana juzi wakati wanacheza na ADT ya Djibouti walisema ni xku ya Max Nzengeli ya kuchomekea, siku ile wajanja tulijua kuwa nyota ya ushindi kapewa yeye, ni rahisi sana kutabiri matukio ya Yanga kutokana na mipango yao nje ya uwanja.

Hakuna cha Gamondi wala nini, ni mipango nje ya uwanja inafanya kazi.
 
Hakuna cha ubora wa nini, iweje Bangala na Feitoto waonekane wachezaji wa kawaida tu wakiwa azam wakati walipokuwa Yanga walikuwa mastaa na walikuwa wanaupiga mwingi...
Nyie mmezuiwa kuifanya iyo mipango ya nje ya uwanja? Kama ndio ivyo basi fungeni mabakuri yenu kila mtu atakula alikopeleka mboga, uwezi kusajili kina boko alafu ukaanza kulalamika eti wenzako wanatembelea nyota! Iyo nyota wewe auna? Utumbo kama huu ni aibu kuupost hapa na unakuta ni baba mzima na akili zake timamu!
 
Wewe ni kolowizad namba moja hapo kolofc aka mbumbumbufc
 
Mlichoma Hadi moto uwanjani ,mkapigwa faini ya Dola 10000 na bado mkabakwa na Wazuru ila umekomaa na ushirikina
Kutwa kurogana wenyewe Kwa wenyewe,kila siku Kramo anaumwa tumbo la kuhara kama bata,halisikii Tetracycline wala Doxycycline
Kuna watu wachawi kama makolo ila bado mnabanduliwa robo robo shenzi taip
 
Mkuu tunawasubiri klabu bingwa[emoji1787][emoji1787]wakienda hata makundi tu niiteni mbwaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…