GANNIBAL: Kutokea mtumwa hadi mtawala

GANNIBAL: Kutokea mtumwa hadi mtawala

zitto junior

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2013
Posts
20,537
Reaction score
31,729
Wakuu habari za asubuhi kama kawaida na mada zangu za kuongelea waafrika waliosahaulika katika historia leo ningependa tujikumbushe kuhusu Abraham petrovich Gannibal.
unnamed (5).jpg


Nguli huyu alizaliwa logon cameroon mwaka 1696 na kufariki urusi mwaka 1781.Alipokuwa miaka 8 akauzwa kwenda utumwani na kabila hasimu hivyo walipotokea wafanyabiashara wa kituruki basi akabebwa hadi constantinople yaani uturuki ya sasa ila licha ya kukulia kwenye umaskini na utumwa kijana huyu alijikuta akisogezwa kwenye hatima njema ya maisha yake bila kufahamu kiufupi waliomuuza walikuwa wanampiga chura mateke.

KUKUTANA NA MFALME PETER 1
Aliuzwa utumwani urusi na huko akapelekwa kwenye ikulu ya Czar (mfalme) Peter 1 aka Peter the great ambaye kihistoria ndio aliifanya Russia iwe hapa ilipo yaani taifa kubwa. Kukutana naye kukawa muujiza katika maisha ya Gannibal maana alimuasili na hivyo alipata fursa zote ambazo zingeweza kuonyesha uwezo wake mtumwa huyu. Alifika ikulu hapo kama mbeba silaha na mavazi wa Czar Peter 1 akiwa vitani.

Muda haukupita akapelekwa kusoma nchini ufaransa ambako alisomea Uhandisi na mafunzo ya kijeshi na akafaulu sana na kugraduate 1723 il ufaransa wakambakisha kama commander mmojawapo ili awasaidie jeshini kwao hasa kwenye vita dhidi ya Hispania ila baadae urusi walimrudisha ili akatumike.

KIFO CHA CZAR PETER 1
Kinyume na alivyotarajia kuwa sasa amemaliza mafunzo arudi kutumika kwa Czar Peter!! akakutana na msiba wa mfalme huyo mwaka 1725 ambaye alikuwa kama baba yake hivyo alifadhaika sana maana aliona ndoto zake zote zimefia hapo... Na kweli kama alivyohisi kiongozi aliyerithi madaraka ya ufalme yaani Prince Menhikov alimuona gannibal kama tishio sababu ya elimu na ushawishi wake hivyo akampeleka siberia ili azekee huko mbali na mji yaani ni sawa na magufuli ampeleke majaliwa kuwa mkuu wa wilaya ya buchosa!!!

Ila kama wasemavyo waswahili kuwa Mungu si Athuman ibrahim gannibal nyota yake bado iling'ara na miaka michache baadae uongozi mpya ulimuita arudi moscow na haraka alipanda madaraja hadi kufikia kuwa Jenerali wa jeshi la urusi na akawa mtawala ilihali alikuja kama mtumwa na chini ya utawala wake alifanya mambo makubwa ya kimaendeleo kiasi anakumbukwa mpaka leo na taifa la urusi.

HITIMISHO
Story ya Ibrahim Gannibal iwe fundisho kwa sisi watu weusi kuwa hatupo inferior kwa watu weupe na ndio maana licha ya kuwa mtumwa ila aliweza kuwa mtawala wa wazungu waliomtumikisha mwanzoni, hivyo ni vizuri historia za mashujaa hawa waliotangaza vyema Afrika zifundishwe mashuleni kuliko kufundishwa kwamba watu weusi huwa hatuwezi kujitawala mpaka aje mzungu atukoloni ndio maendeleo yaje...!! Kama Malcom Lumumba alivyopata kusema ''Mabadiliko ya kifikra ndio yatatutoa hapa tulipo''.

AFRIKA TUAMKE

naomba kuwasilisha.... Wenye maoni,wajuvi wa historia mtiririke mengine mnayoyafahamu kuhusu mtu huyu ili tuzidi kujifunza
Петровское._Бюст_А.П._Ганнибала.jpg
 
Ila urusi sionagi maniga sana km ilivyo amerika!ingawa amerika utasema nchi ya maniga
 
Ila urusi sionagi maniga sana km ilivyo amerika!ingawa amerika utasema nchi ya maniga
Marekani si biashara ya utumwa ilibeba maelfu ila sidhani kama urusi ilikuwa ina inflow ya watumwa wengi kihivyo kutoka afrika kiasi hadi manigga wawe kibao kma US
 
Inatia hamasa na moyo kwenye maisha yetu ya leo, Don't give up keep fighting.
Kanikumbusha Uprising ya Spartacus na watumwa wenzake, kutoka kua watumwa hadi kufikia hatua ya kua tishio kwa utawala wa Rumi. Japo alikua mzungu alitoka kua mtumwa anayepiganishwa/Gladiator hadi kuwa kiongozi nakupelekea vita Third Servile War 73 - 72 BC mwisho wa siku waliishia kutundikwa msalabani na Warumi
 
Back
Top Bottom