Gardner Habash: Natumia laki 1 kwa siku

jaman tuache kujikweza, laki kwa siku ni kubwa acheni masihara......inamaana mshahara wa 3m kwa mwezi tena hiyo ni take home huna serving yoyote unayofanya zaidi ya matumizi ya kawaida??? seriously???....sasa kibanda chako utajenga lini?? maana hapo hana familia anatumia laki ukiwa na familia ya watoto 2 mpaka 3, wife, house girl si ndo atatumia laki 3 kwa siku??
 
Umeona eeh. Eti mtangazaji wa radio anatumia laki kwa siku. Kwa asset gani alizonazo?
 
Aombe radhi kwanza ndio atumie hiyo laki yake kwa siku.
 


Duh! Kuwa gentleman kidogo Kama jina lako.
 


Duh watu mna manenoo, jana nilisikiliza Jahazi, hiyo laki alisema kama mfano tu, sio kwamba ndio matumizi yake kwa siku ..........................................
 
Duh watu mna manenoo, jana nilisikiliza Jahazi, hiyo laki alisema kama mfano tu, sio kwamba ndio matumizi yake kwa siku ..........................................
Siyo mfano. Alisema uhalisia. Tena alisema ikitokea hana yupo tayari kupiga mzinga kwa washkaji zake. Na pale alikuwa ameshatoka kupiga mzinga kwa mtu na kamtumia laki 1 lakini akawa abashindwa kuitoa Airtel money.
 
Watanzania bwana kila MTU anaweza kuongea bila vidhibitisho ilimradi tu aonekane wa maana. OK Mimi natumia lakini tano kwa siku.
 
Hizo ni fix kwa mahesabu ya 3m take home. Ina maana basic ni zaidi ya 4m. Huo ni uongo.
Kuna siku akiwa Efm akiwa na kina Mpoki n Seth alikuwa anajinadi anakunywa kinywaji fulani jina limenitoka ambacho chupa ni 200k mpoki akamuuliza anajimudu akadai kuna wadhamini. Kwa mtu mwenye mshahara wa 4m kuchoka 200k kwa chupa moja kawaida tu. Si jambo la kutoa macho.
 
Mimi sipingi wala sikubali kwa kuwa siyajui maisha yake kwa ujumla zaidi ya kumsikia redioni tu na si zaidi ya hivo. Ila niwape ushauri wale wanaopinga na wanaomtetea wasituambie kuwa wanapinga/kukubali kwa kuwa wanamsikia tu redioni kama mimi/sisi ila iwe wanamjua kiundani wa maisha yake kwa maana ya mshahara anaolipwa(na posho kama zipo) au kama anavitega uchumi alivyonavyo au kama wanajua namna nyingine yake ya kumuingizia kipato.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…