Gari aina moja, majina tofauti, nini athari zake?

Ligogoma

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2010
Posts
3,503
Reaction score
6,415
Habari wana JF??

Katika pita pita zangu kwenye mitandao hasa kwenye kuangalia zaidi magari, nimegundua kitu kimoja na kimekuwa kikinitatiza sana. Gari linakuwa limetengenezwa na kampuni moja, Pia ni brand moja (aina), zimetengenezwa mwaka mmoja lakini kwa sababu tu yanauzwa mabara tofauti basi yanakuwa na majina tofauti.

Kwa mfano: Toyota Ipsum ukienda Ulaya na Amerika linaitwa Toyota Avensis Verso
Toyota Vitz hali kadhalika kwa wenzetu linajulikana kama Toyota Yaris
Mitsubishi Pajero IO GDI wao wanaliita Mitsubishi Shogun Pinin
Nissan March wao wanaita Nissan Micra

Hayo ni mfano tu wa magari machache yanayotofautiana majina kutoka bara moja na jingine.

Mwenzenu nimekuwa nikijiuliza maana au athari za kufanya hivi ni nini?? Ni mbinu za kibiashara?? Njia hii wanayoifanya haiwezi kuwa ndiyo chanzo cha kutengeneza magari yenye kiwango cha chini kwenda Afrika na magari imara kwenda Ulaya na Amerika, mfano wakasema Nissan Micra zote zirudishwe kiwandani si imekula kwa Waafrika hapo??

Wataalamu wa haya mambo tunaomba mtujuze jamani.
Nawasilisha
 

Moja toyota ulaya jingine toyota japan
 
Kweli mkuu mfano toyota PASSO ndo hiyo hiyo DAIHATSU BOON mazda bongo ndo hiyo hiyo Nissan Vanette mwee !!

Tena mkuu hii haimuzi sana kichwa sababu Toyota na Daihatsu ni kampuni tofauti ila jaribu kuangalia gari nilizotaja hapo mfano Toyota Ipsum na Toyota Avensis Verso!! Kila kitu ni kile kile but majina tofauti, why??
 
Mi huwa natatizwa na Cami vs Terrious. Mmoja ni Toyota na mwingine Daihatsu lakini kwa kuyaangalia sioni tofauti zake.

Daihatsu na Toyota nahisi wana lao moja, angalia na Toyota BB na Daihatsu Materia huwezi kutoa tofauti hata kidogo. Kuna na mdau (@Mwamunu)hapo kataja Toyota Passo na Daihatsu Boon
 
Kweli mkuu mfano toyota PASSO ndo hiyo hiyo DAIHATSU BOON mazda bongo ndo hiyo hiyo Nissan Vanette mwee !!

Mkuu.....mbona hapa kuna kampuni kama 4 hivi tofauti kama sijakosea......
Halafu Rav4 J au V kule zimepewa majina ya Rav4 GX au VX....
 
sa si ndo vizuri kwani hata spea zitaingiliana ,tena hiyo passo na daihatsu boon ndo hatari, ukiangalia hata injini zake kila kitu mulemule hadi raha,mjanja ka mie nanunua boon kwa kuwa mara nyingi bei zake zipo chini kiaina kuliko passo,angalizo,DAIHATSU MOTOR CORPORATION na TOYOTA MOTOR ni dugu moja kabisa na ndio maana baadhi ya brand zao zinafanana kabisa ingawaje majina ni tofauti
 

Hapa tatizo ni lugha mkuu. kuna jamaa alinieleza kuwa baadhi ya majina ya kijapani ktk nchi nyingine ni matusi. kulikuwa na email (spam) ikielezea kuwa Tanzania imemkataa mmoja wa wateule aliyekuwa awe balozi sababu ya jina lake.

hivyo hivyo kwa magari ya kijapani ktk baadhi ya nchi ni matusi kabisa au yana maana tata ndo maana wanabadili majina ingawa muundo na na mwonekano ni mirror image ya jingine. Soma hili hapa chini: The Legend of the Chevy Nova That Wouldn't Go

Isipokuwa huku kwetu ni bora gari tu ilimradi linanitoa point A to point B hayo mengine hatuna haja nayo
 

Mara nyingi huwa ni sababu za kibiashara au tamaduni. Mfano, Toyota Highlander ni gari lile lile la Toyota Kluger. Wajapani hawawezi kutamka Highlander kwa ufasaha hivyo Highlander inauzwa Marekani na Kluger inauzwa Japani lakini ni gari ile ile. Ni kama tu toyota Harrier na Lexus RX 300. Lexus RX 300 iko kwa ajili ya Soko la Marekani na Harrier ni soko la japani lakini ni gari ile ile.

Pia Daihasu Motor Corporation ni subsidiary company ya Toyota ndo maana magari yao yanafanana kwa vile Daihatsu ni mtoto wa Toyota. Subsidiary nyingine y a Toyota ni Lexus (Luxurious Car division of Toyota) na Hino
 
ukinunua RAV 4 used toka England unaona tofauti, iko more comfortable ndani kuliko zile zinazoletwa Africa moja kwa moja, dark continent

Kula like mkuu, umegundua hili!! Then hata fuel consumption ni tofauti sana fanya uchunguzi tena! Nilikuwa nafuatilia hii Toyota Ipsum kwao wanaita Toyota Avensis Verso, hizi Ipsum za Africa zina CC2300 ila za Avensis Verso toka UK na Ulaya zina CC2000.

Vivo hivyo gari za Land Rover tunazonunua kutoka makampuni ya Japan ya CC kubwa sana mfano Range Rover zinakuwa na CC4400 na ziko hovyo hovyo wakati za Ulaya zina CC3000 na ni very comfortable.

Inawezeka Africa bado ni sehemu yao ya kupatia faida kubwa
 
cheverlette cruize ni sawa na suzuki swift kama ilivyo toyota cami na dahaitsu terrios
 
Toyota Tundra = Hilux
Toyota Highlander = Kruger
Lexus G740 = Toyota Prado
Lexus Rx64 = Toyota Harrier
Toyota 4Runner = Surf
Lexus Lseries = Toyota Alteeza
Nissan Maxima = mna jina lenu nimesahau
Nissan Altima = mna jina lenu nimesahau
 
As far as I know makampuni mengi ya magari huwa yananunuana na wakti mwingine kuungana ili kupunguza gharama hasa katika Research and development. Hii tabia iko dunia nzima.

Volkswagen group ina karibu magari nane chini yake Na mengine wan share nyingi sana. Lamborghini, Porsche, Bentley, Buggati, Skoda hadi malori ya Scania na MAN. So sometimes unakuta braking system technology inakuwa developed kwa ajili Porsche 911, then itaenda kutumika kwenye Golf etc etc. Inapunguza gharama, na haya mambo yapo dunia nzima, Renault wapo na Nissan, Ford na Mazda na Hyundai. Daihatsu + Toyota + Hino = family moja.

Sometimes inatokana pia na mahitaji ya soko. In America, Lexus inauza sana and it is perceived ti be more luxurious tha Toyota and they are actually made better than normal Toyota, likewise Nisaan is sold as Infinity, Honda as Acura.... ni presentation tu chakula kile kile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…