Ligogoma
JF-Expert Member
- Aug 27, 2010
- 3,503
- 6,415
Habari wana JF??
Katika pita pita zangu kwenye mitandao hasa kwenye kuangalia zaidi magari, nimegundua kitu kimoja na kimekuwa kikinitatiza sana. Gari linakuwa limetengenezwa na kampuni moja, Pia ni brand moja (aina), zimetengenezwa mwaka mmoja lakini kwa sababu tu yanauzwa mabara tofauti basi yanakuwa na majina tofauti.
Kwa mfano: Toyota Ipsum ukienda Ulaya na Amerika linaitwa Toyota Avensis Verso
Toyota Vitz hali kadhalika kwa wenzetu linajulikana kama Toyota Yaris
Mitsubishi Pajero IO GDI wao wanaliita Mitsubishi Shogun Pinin
Nissan March wao wanaita Nissan Micra
Hayo ni mfano tu wa magari machache yanayotofautiana majina kutoka bara moja na jingine.
Mwenzenu nimekuwa nikijiuliza maana au athari za kufanya hivi ni nini?? Ni mbinu za kibiashara?? Njia hii wanayoifanya haiwezi kuwa ndiyo chanzo cha kutengeneza magari yenye kiwango cha chini kwenda Afrika na magari imara kwenda Ulaya na Amerika, mfano wakasema Nissan Micra zote zirudishwe kiwandani si imekula kwa Waafrika hapo??
Wataalamu wa haya mambo tunaomba mtujuze jamani.
Nawasilisha