Gari aina moja, majina tofauti, nini athari zake?

Hakuna magari ya Africa bali bei ndio inayoamua kipi kiuzwe wapi kuhusu kubadilika majina si kwenye magari tu bali vitu vingine vyote
Angalia coke cola wanadai formula yao ni moja dunia nzima lakini kila nchi inatofautiana chupa kutokana na mahitaji ya nchi husika
Vilevile hata kama gari ni brand moja lakini kuna vitu huongezwa au kupunguzwa kutokana na hali ya hewa ya nchi husika
 

Kweli kabisa! Fiat 'Pinto' Latin America inaitwa Fiat 'Uno'. Pinto kihispaniola ni uume mdogo!
 
Mi huwa natatizwa na Cami vs Terrious. Mmoja ni Toyota na mwingine Daihatsu lakini kwa kuyaangalia sioni tofauti zake.

Terrios amenunuliwa na Toyota.

Pia mfano mwingine ni Toyota Harrier ambayo Marekani huitwa Lexus.

Hizo gari zina tofauti kadhaa japo kimsingi ndio hizo hizo na zinafanana sana. Kwa mfano Toyota Harrier ni kwa ajili ya soko la Japan na nchi nyingine. Rexus ni kwa ajili ya soko la Marekani. Tofauti hizo mara nyingi huja ili kukidhi viwango vya Marekani na Ulaya katika mambo fulani fulani ndani ya gari. Mfano, unene wa bati katika gari aina ya Toyata RAV4 ni tofauti. Ulaya na Marekani wanataka bati nene zaidi. Hizo tofauti unaweza kuziona haya magari yakiwa Dar - moja la Japan na lingine la Ulaya. La Ulaya body haiozi kirahisi kufuatana na unene wa bati lake. Tofauti nyingine zinaweza kuwa kwenye engine
 
Sijakuelewa mkuu, unamaanisha nini kusema Toyota Ulaya na Toyota Japan??

Tena mkuu hii haimuzi sana kichwa sababu Toyota na Daihatsu ni kampuni tofauti ila jaribu kuangalia gari nilizotaja hapo mfano Toyota Ipsum na Toyota Avensis Verso!! Kila kitu ni kile kile but majina tofauti, why??



  1. Kwa uelewa wangu mdogo kwenye hii ndustry ya magari ni kwamba: kuna wakati hizi kampuni huwa zinafanya kazi ya kutenganisha masoko ya magari yao (market segmentation) na kutengeneza tofauti ndogo ndogo sana kwenye bidhaa zao, ili kuleta ladha "tofauti". Mfano, Toyota L/cruiser kwa huku Afrika tuna VX, ilhali Toyota hiyo hiyo kwa kule Uingereza ni Amazon. Kwa USA, Toyota hiyo ni Lexus (kama ile ya marehemu Kanumba). Injini, bodi na mambo mengine almost ni vilevile. Hali ni hiyo hiyo kwa Toyota Harier na Lexus LX series.
  2. Kutokana na ugumu wa kupenyeza bidhaa sokoni (kwa sababu za kiushindani), kuna wakati inabidi baadhi ya kampuni za magari zinunue hisa kwenye kampuni nyingine na kuwekeza hizo brands zao huko. Ukitazama Nissan Civilian (hizi new model), haina tofauti na Isuzu Journey (new model, sio ile ya zamani). Bodi, injini na kila kitu vinafanana. Kuna model ya Benz, sikumbuki jina, ina components zile zile kama Toyota Mark X
  3. Suala la mwisho ni wizi wa teknolojia. Ukiangalia malori ya FAW (new model) ni sawia kabisa na Mitsubishi Fuso (model ya zamani, zilizotoka 1989 na 1990). Yaani ni copy and paste. 'Inasemekana' Mchina ali hack servers za Mitsubishi na kuiba michoro. Hizo ni hearsays ambazo unapaswa kuzipotezea
 

Hili ulilolisema hapo mkuu ndilo nililouliza kule juu, athari za utofauti huu ni nini naona tunakwenda sawa sasa!! Umesema la Ulaya haliozi kirahisi, kwa maana nyingine nchi zetu hizi zisizokuwa makini tunaletewa magari yasiyo na ubora na tunapokea tu!!

Nakumbuka kuna wakati walitaka gari zote za Toyota Land Cruiser VX yaliyokuwa yameuzwa Ulaya na Marekani yarudishwe kiwandani! Hii haikuhusu yaliyokuwa yameuzwa Africa?
 
Nakumbuka kuna wakati walitaka gari zote za Toyota Land Cruiser VX yaliyokuwa yameuzwa Ulaya na Marekani yarudishwe kiwandani! Hii haikuhusu yaliyokuwa yameuzwa Africa?

Nikiweka msisitizo hapo kwenye bold, naweza kujibu kama hivi:
  1. Inawezekana batch ya magari hayo iliyouzwa Afrika kutoka kwenye viwanda hivyo haikuwa na hitilafu hiyo
  2. Huenda model hiyo hiyo ilitengenezwa ktk kiwanda cha Afrika Kusini (kuna kiwanda cha Toyota pale). Toyota Hilux D4D na hardtop nyingi siku hizi zinatoka Afrika Kusini.
 
Ni kweli alivyoandika Idimi. Ila Daihatsu inamilikiwa na Toyota. Kuna baadhi ya makampuni pia wanashirikiana katika kutoa model k.m. Honda, Nissan, Vauxhaul na Isuzu wote wametoa gari moja majina tofauti - Isuzu Wizard, model moja ya Terrano na Vauxhaul Frontera na Honda Jazz (Kuna fit jazz na SUV)

Mazda, Ford na Nissan wameshirikiana ; Nissan Vannette, Mazda bongo na Ford Frieda.

Suzuki Swift na Chevrolet Cruze.

Suzuki Vitara/Escudo na Mazda Proceed levante
 

mkuu,hizi gari za japan na uk/usa ni tofauti kabisa ingawa zina muonekano ulio sawa

1.lexus rx300 inaonekana kama harrier lakini mashine na gadgets ndani ni tofauti,lexus rx300 iko superior hata speed rx300 ina up to 240km harrier mwisho ni 180kph
2.lexus 1s200 na altezza hata ukisikiliza engine ni tofauti kabisa....is200 ina speed 240+ wakati altezza ina 180
ukifanikiwa kuendesha zote mbili utanielewa

ukija kwenye rav4 za japan na uk ni tofauti kabisa kuanzia comfortability hadi mbio....kuna reason kwa nini rav4 za uk zina max speed 220+ na za japan ni 180kph sio bure kuna sababu.
 
Za UK/US zipo Confotable kuliko za Japan!! Hata speed ni tofauti, kazi ipo....!! Kitambo sana hata hivyo
 
Kwa uzoefu wangu magari hata kama yamefanana namna gani kwa macho. Kwa upande wa spare parts zinatofautiana kwa baadhi ya vitu. Spare za magari ya kijapan zipo tele na bei ya chini lakini magari ya UK na US upatikanaji wa spare ni mgumu na bei juu.
 


Mkuu,toyota ipsum ulaya ni toyota picnic na sio hiyo ulioitaja wewe
 
Hayo majina ni division tu za hayo makampuni kibiashara ila hayo magar yanakua tofaut tofaut kwa baadhi ya mambo kulingana nakule yalikokusudiwa yauzwe.Hii inafanyika ili kukidhi mahitaj yakila pembe ya dunia na watumiaji tofauti tofauti.Wakat hapa kwetu barabara na sheria hairuhusu kumaliza speed meter 180 iliyoko kwenye magar mengi yanayotumika hapa nchini wenzetu nchi nyingine wanamaliza 240 km/hr.Wakati hapa kwetu Vx V8 ni anasa wenzetu nikawaida.Wakat hapa barabara zimejaa humps wenzetu ni full mkeka.Wakat hapa unatembelea kushoto kuna mwingine anatumia kulia.Sasa kwa hali iyo lazima kuwe na matoleo tofaut tofaut ili kuonyesha ayo niliyosema hapo juu.Na hiyo iko ata kwenye vitu vingine kama cm,computer n.k.Hata sis serikal ya viwanda ikikamilisha kazi yake tutakua na hizo division kwenye bidhaa zetu.
 
This is called Rebadging or badge engineering, is the application of a different brand to an existing product. This practice is done to reduce high cost of designing and engineering a new model or establishing a brand
 
Kasome BRANDING kwa undani zaidi utaelewa
 
Kuna Brand na kuna manufacturer .
kama Cocacola......ya Tanzania na ya Kenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…