Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapa tatizo ni lugha mkuu. kuna jamaa alinieleza kuwa baadhi ya majina ya kijapani ktk nchi nyingine ni matusi. kulikuwa na email (spam) ikielezea kuwa Tanzania imemkataa mmoja wa wateule aliyekuwa awe balozi sababu ya jina lake.
hivyo hivyo kwa magari ya kijapani ktk baadhi ya nchi ni matusi kabisa au yana maana tata ndo maana wanabadili majina ingawa muundo na na mwonekano ni mirror image ya jingine. Soma hili hapa chini: The Legend of the Chevy Nova That Wouldn't Go
Isipokuwa huku kwetu ni bora gari tu ilimradi linanitoa point A to point B hayo mengine hatuna haja nayo
Mi huwa natatizwa na Cami vs Terrious. Mmoja ni Toyota na mwingine Daihatsu lakini kwa kuyaangalia sioni tofauti zake.
Sijakuelewa mkuu, unamaanisha nini kusema Toyota Ulaya na Toyota Japan??
Tena mkuu hii haimuzi sana kichwa sababu Toyota na Daihatsu ni kampuni tofauti ila jaribu kuangalia gari nilizotaja hapo mfano Toyota Ipsum na Toyota Avensis Verso!! Kila kitu ni kile kile but majina tofauti, why??
sa si ndo vizuri kwani hata spea zitaingiliana ,tena hiyo passo na daihatsu boon ndo hatari, ukiangalia hata injini zake kila kitu mulemule hadi raha,mjanja ka mie nanunua boon kwa kuwa mara nyingi bei zake zipo chini kiaina kuliko passo,angalizo,DAIHATSU MOTOR CORPORATION na TOYOTA MOTOR ni dugu moja kabisa na ndio maana baadhi ya brand zao zinafanana kabisa ingawaje majina ni tofauti
Terrios amenunuliwa na Toyota.
Pia mfano mwingine ni Toyota Harrier ambayo Marekani huitwa Rexus.
Hizo gari zina tofauti kadhaa japo kimsingi ndio hizo hizo na zinafanana sana. Kwa mfano Toyota Harrier ni kwa ajili ya soko la Japan na nchi nyingine. Rexus ni kwa ajili ya soko la Marekani. Tofauti hizo mara nyingi huja ili kukidhi viwango vya Marekani na Ulaya katika mambo fulani fulani ndani ya gari. Mfano, unene wa bati katika gari aina ya Toyata RAV4 ni tofauti. Ulaya na Marekani wanataka bati nene zaidi. Hizo tofauti unaweza kuziona haya magari yakiwa Dar - moja la Japan na lingine la Ulaya. La Ulaya body haiozi kirahisi kufuatana na unene wa bati lake. Tofauti nyingine zinaweza kuwa kwenye engine
Nakumbuka kuna wakati walitaka gari zote za Toyota Land Cruiser VX yaliyokuwa yameuzwa Ulaya na Marekani yarudishwe kiwandani! Hii haikuhusu yaliyokuwa yameuzwa Africa?
Mara nyingi huwa ni sababu za kibiashara au tamaduni. Mfano, Toyota Highlander ni gari lile lile la Toyota Kluger. Wajapani hawawezi kutamka Highlander kwa ufasaha hivyo Highlander inauzwa Marekani na Kluger inauzwa Japani lakini ni gari ile ile. Ni kama tu toyota Harrier na Lexus RX 300. Lexus RX 300 iko kwa ajili ya Soko la Marekani na Harrier ni soko la japani lakini ni gari ile ile.
Pia Daihasu Motor Corporation ni subsidiary company ya Toyota ndo maana magari yao yanafanana kwa vile Daihatsu ni mtoto wa Toyota. Subsidiary nyingine y a Toyota ni Lexus (Luxurious Car division of Toyota) na Hino
Za UK/US zipo Confotable kuliko za Japan!! Hata speed ni tofauti, kazi ipo....!! Kitambo sana hata hivyomkuu,hizi gari za japan na uk/usa ni tofauti kabisa ingawa zina muonekano ulio sawa
1.lexus rx300 inaonekana kama harrier lakini mashine na gadgets ndani ni tofauti,lexus rx300 iko superior hata speed rx300 ina up to 240km harrier mwisho ni 180kph
2.lexus 1s200 na altezza hata ukisikiliza engine ni tofauti kabisa....is200 ina speed 240+ wakati altezza ina 180
ukifanikiwa kuendesha zote mbili utanielewa
ukija kwenye rav4 za japan na uk ni tofauti kabisa kuanzia comfortability hadi mbio....kuna reason kwa nini rav4 za uk zina max speed 220+ na za japan ni 180kph sio bure kuna sababu.
Kula like mkuu, umegundua hili!! Then hata fuel consumption ni tofauti sana fanya uchunguzi tena! Nilikuwa nafuatilia hii Toyota Ipsum kwao wanaita Toyota Avensis Verso, hizi Ipsum za Africa zina CC2300 ila za Avensis Verso toka UK na Ulaya zina CC2000.
Vivo hivyo gari za Land Rover tunazonunua kutoka makampuni ya Japan ya CC kubwa sana mfano Range Rover zinakuwa na CC4400 na ziko hovyo hovyo wakati za Ulaya zina CC3000 na ni very comfortable.
Inawezeka Africa bado ni sehemu yao ya kupatia faida kubwa
Mbona umetaja kampuni 4 tofauti?Kweli mkuu mfano toyota PASSO ndo hiyo hiyo DAIHATSU BOON mazda bongo ndo hiyo hiyo Nissan Vanette mwee !!
Kasome BRANDING kwa undani zaidi utaelewaHabari wana JF??
Katika pita pita zangu kwenye mitandao hasa kwenye kuangalia zaidi magari, nimegundua kitu kimoja na kimekuwa kikinitatiza sana. Gari linakuwa limetengenezwa na kampuni moja, Pia ni brand moja (aina), zimetengenezwa mwaka mmoja lakini kwa sababu tu yanauzwa mabara tofauti basi yanakuwa na majina tofauti.
Kwa mfano: Toyota Ipsum ukienda Ulaya na Amerika linaitwa Toyota Avensis Verso
Toyota Vitz hali kadhalika kwa wenzetu linajulikana kama Toyota Yaris
Mitsubishi Pajero IO GDI wao wanaliita Mitsubishi Shogun Pinin
Nissan March wao wanaita Nissan Micra
Hayo ni mfano tu wa magari machache yanayotofautiana majina kutoka bara moja na jingine.
Mwenzenu nimekuwa nikijiuliza maana au athari za kufanya hivi ni nini?? Ni mbinu za kibiashara?? Njia hii wanayoifanya haiwezi kuwa ndiyo chanzo cha kutengeneza magari yenye kiwango cha chini kwenda Afrika na magari imara kwenda Ulaya na Amerika, mfano wakasema Nissan Micra zote zirudishwe kiwandani si imekula kwa Waafrika hapo??
Wataalamu wa haya mambo tunaomba mtujuze jamani.
Nawasilisha