Gari aina ya Cresta Gx 100

chief2021

New Member
Joined
Mar 3, 2021
Posts
1
Reaction score
56
Namiliki gari aina ya cresta gx 100 yenye injini ya 1G kavu.

Hii gari wakuuu Mjapani hapa alicheza kama pele gari iko na starehe kama yote wakati unadrive.

Kama ni mzee wa myendoo basi hapa ndiopake.

Uvumilivu wa hizi gari ni wa kiwango cha juu sana.

Safari popote utakapo unafika kwa wakati.

Ushauri wangu vijana wenzangu ambao bado tunaungaunga na life tusiogope CC kabisaaaa mafuta inakula kawaida sanaaaaaa.

Tunakosa vitu vizuri kisa tunatishwa na CC hatimaye tunakimbiliaaa kwenye Vitz, ist na porte
 
Yameshuka bei sana mtaani kutokana na kuwa na engine kubwa hali inayopelekea kunywa mafuta tofauti na gari nyingi za watu wa hali ya chini, upande wa mwendo na kutulia barabarani hapo ndio mwake...nimeshamiliki hiyo kitu yenye Vvti.
 
Ulaji wenyewe wa mafuta sio mkubwa kama mnavyosema. Zingatia service kwa wakati utalifurahia, hutaonekana gereji mara kwa mara, naweza sema ina immune kubwa ya kuhimili magonjwa ila .... service ni muhimu. Ni gari ya safari sasa kama wewe unaitumia kuendea gengeni na saloon lazima uichukie. Ikiwa barabarani (long safari) inatulia sana, ni nzito haiyumbi, imeshibaaa. Kuuzwa bei rahisi sio kwa sababu ya ubovu ni kwa sababu mengi yalinunuliwa miaka 10 iliyopita hivyo kwa sasa lazima yauzwe chini. Ukiagiza bado bei yake iko juu na wengi kwa sasa hawayaagizi kwa uoga wa maneno ya kuogopa mafuta!
 
Tatizo sio kutunza inshu ipo kwenye mkojo wa mwarabu yananyonya kama jini
Inategemea na uliyochukua, kama ni six (6 Cylinders) hiyo consumption hua juu maana ina speed zaidi.

Ila four (4 Cylinders) hua consumption yake ni ya kawaida sana.

All in all, yale magari ni mzuri aisee , Nimelipark tu, kama backup car.

Nzuri sana.
 
Wakuu mie naulizia Mark ii gx 110 nataka nikamate hii nitoke kwenye IST wese sio ishu, naomba kujua changamoto na faida zake
Cc;
Extrovert mng'ato
 
Re-Sale value iko chini hayashikilii thamani yake kwa muda mrefu, unaweza ukalivusha maji toka Japan kwa 11M ila baada ya miezi 6 tu ukitafta mteja wanakuja wa 5M ama chini sio kama IST unanunua leo 13M ukija kuliuza mwakani kipindi kama hichi unauza 10.5M.

Pia kuna msemo unasema kwamba ukitaka kumuua mbwa muite jina baya😂 huo msemo umejidhihirisha kupitia hili gari kuwa ni "jini mnyonya wese" wakati gari inaitwa chaser yani mkimbizi ila mtu anaendesha speed 30 af anategemea awe rafiki na gauge ya mafuta. Huwezi kuendesha gari na gear 1&2 af utegemee isile mafuta. Hizi gari ni rafiki kwenye less traffic areas kama mikoani ila dar litakutesa. Linataka service kwa wakati na speed ili u attain fuel economy nzuri.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…