Kama utakuwa unaendesha mwenyewe itakulipa lakini kama utampa mtu akuletee hesabu jiandae na maumivu, sbb kwa wiki uber hesabu kwa boss ni 150,000 kwa mwezi ni 600,000 kwa mwaka ni 7,200,000 bado hapo unadaiwa karibia milioni tano ili ifike 12m, ukiendesha mwenyewe kwa siku unaweza kuingiza hadi laki moja kwa hesabu ya haraka kwa wiki unaingiza laki tano kwa mwezi 2m kwa mwaka ina maana 24m yaani pesa yako inarudi na unanunuwa ist nyingine. Akili kichwani mwako.
HII BIASHARA HAILIPI (kulaza 100,000 kwa siku ni ngumu sana)
Nianze na UBER. Uber wanalipa kila kilomita sh. 450 na kila dakika sh. 80.
Tuchukulia kinadharia nimeamua ku “ request” Uber nikazunguka nayo masaa 12 na kutembea Dar kilomita 300.
Nakokotoa hesabu
Km 300 x shs. 450 = 135,000
Dakika 12x60x shs. 80 = 57,600
JUMLA NI 192,600
Kilomita 300 kwa Gari kama IST inatumia lita 33-37 inategemea na uendeshaji wa dereva
Tuchukulie lita 35x bei ya petrol sasa 2,123 = 74,305
UBER wanakata chao asilimia 25%
Kwa hiyo (25% x 192,600) - mafuta 74,305 = 70,145
Kwa hiyo dereva anabakiwa 70,145 kama gari ni yako, kama ana boss atoe hiyo t.shs 25,000 au 30,000.
Kuna malipo ya latra , insuarence, parking tickets(unaweza kuona ndogo lakini ziki accumulate ni nyingi.) Gari itahitaji service mara kwa mara maana inatembea km nyingi kwa siku
Uhalisia ni kwamba huwezi pata Request kila muda, kupata 70,000 kwa siku ni kazi kubwa sana
HASARA YA BIASHARA HII
1. Mteja aki “request” ukaenda kumchukua haulipwi kwa km ulizotembea kumfuata, malipo yanaanza pale tu mteja akiingia kwenye gari. Hiyo ni hasara kwa dereva.
2. Kuna maeneo mengi Dar ukimpeleka mteja unarudi kapa. Na hujui abiria unampeleka wapi mpaka aingie kwenye gari.
3. Dar njia nyingi ni mbovu ni kuichosha gari tu.
4. Wateja hawajui kutumia app vizuri, location alipo na alipo “pin” kwenye map ni vitu viwili tofauti. Unahangaika kumtafuta ukimuudhi ana cancel
5. App ya Uber ikikaa masaa 12 mfulizo inajizima, inakulazimisha upumzike angalau masaa 6 ndio inarudi
6. Traffic wameshaijua hii biashara usumbufu wao lazima uache “5,000”
FAIDA labda upate “tips” na kwa wageni, (wabongo hawatoi, wanalaalamika tu kwamba unaendesha taratibu ili hela iongozeke au uawapitisha kwenye foleni.) WABONGO BANA.
Kuna muda UBER wanatoa bonus au kuna mida hela inaongezeka kidogo kipindi kuanzia saa 9 alasiri au kama kuna demand kubwa ya gari
Wateja wakikuzoea wanakuwa wanakupigia simu direct, unakwepa 25% ya UBER
BOLT WANALIPA 400km na t.sh. 72 kwa dakika kama nakumbuka vizuri