Gari aina ya IST inawezaje kunirudishia faida

Hapa Dar na nishawahi kujaribu kama wiki moja baada ya kuona dereva wangu ananiletea pesa pungufu na visingizo vingi
Ku generalize matokeo ya income ya wiki moja ku project overall income ya majuma 52 ni makosa makubwa.Hiyo sample yako ni too insignificant kukupa uhalisia,What if week uliyoichagua ndo ilikuwa kwenye peak season? Utajuaje pengine kulikuwa na major event kwenye hyo week ikapelekea excessive demand?
 
Nilijiunga uber na bolt kwa wakati mmoja ss hapo utakosa vp abiria na location niliyokuwepo ilikuwa ya kishua, inafika kipindi nazima data ili angalau nipumzike maana unakuta wakati mwingine inaingia sms niko na abiria
 
Mdanganye tu mwenzako nmefanya uber na bolt kwa mwezi mzima nilichoambulia ni laki 1 tu kuna sku unafanya kazi unaambulia mpka elf 10 ukitoa ya mafuta na commision yao hyo ni biashara ya kujipatia tu hela ya kula laki 3 anaweza pata kwa mwezi kma atakuwa anakesha ila hyo hyo aitoe hela ya service nk

Sent from my SM-M315F using JamiiForums mobile app
 
Kama location yako ilikuwa maporini au uswazi hiyo laki utaipata vipi? Ww unafikiri hata hizi bajaj na bodaboda za hapa mjini mahesabu ni sawa?
 


HII BIASHARA HAILIPI (kulaza 100,000 kwa siku ni ngumu sana)

Nianze na UBER. Uber wanalipa kila kilomita sh. 450 na kila dakika sh. 80.

Tuchukulia kinadharia nimeamua ku “ request” Uber nikazunguka nayo masaa 12 na kutembea Dar kilomita 300.

Nakokotoa hesabu

Km 300 x shs. 450 = 135,000
Dakika 12x60x shs. 80 = 57,600

JUMLA NI 192,600

Kilomita 300 kwa Gari kama IST inatumia lita 33-37 inategemea na uendeshaji wa dereva

Tuchukulie lita 35x bei ya petrol sasa 2,123 = 74,305

UBER wanakata chao asilimia 25%
Kwa hiyo (25% x 192,600) - mafuta 74,305 = 70,145

Kwa hiyo dereva anabakiwa 70,145 kama gari ni yako, kama ana boss atoe hiyo t.shs 25,000 au 30,000.

Kuna malipo ya latra , insuarence, parking tickets(unaweza kuona ndogo lakini ziki accumulate ni nyingi.) Gari itahitaji service mara kwa mara maana inatembea km nyingi kwa siku

Uhalisia ni kwamba huwezi pata Request kila muda, kupata 70,000 kwa siku ni kazi kubwa sana

HASARA YA BIASHARA HII
1. Mteja aki “request” ukaenda kumchukua haulipwi kwa km ulizotembea kumfuata, malipo yanaanza pale tu mteja akiingia kwenye gari. Hiyo ni hasara kwa dereva.
2. Kuna maeneo mengi Dar ukimpeleka mteja unarudi kapa. Na hujui abiria unampeleka wapi mpaka aingie kwenye gari.
3. Dar njia nyingi ni mbovu ni kuichosha gari tu.
4. Wateja hawajui kutumia app vizuri, location alipo na alipo “pin” kwenye map ni vitu viwili tofauti. Unahangaika kumtafuta ukimuudhi ana cancel
5. App ya Uber ikikaa masaa 12 mfulizo inajizima, inakulazimisha upumzike angalau masaa 6 ndio inarudi
6. Traffic wameshaijua hii biashara usumbufu wao lazima uache “5,000”

FAIDA labda upate “tips” na kwa wageni, (wabongo hawatoi, wanalaalamika tu kwamba unaendesha taratibu ili hela iongozeke au uawapitisha kwenye foleni.) WABONGO BANA.

Kuna muda UBER wanatoa bonus au kuna mida hela inaongezeka kidogo kipindi kuanzia saa 9 alasiri au kama kuna demand kubwa ya gari

Wateja wakikuzoea wanakuwa wanakupigia simu direct, unakwepa 25% ya UBER

BOLT WANALIPA 400km na t.sh. 72 kwa dakika kama nakumbuka vizuri
 
Hypothetical
 
Point
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…