Gari aina ya Toyota Noah imezima ghafla haitaki kuwaka

Gari aina ya Toyota Noah imezima ghafla haitaki kuwaka

Patandi

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
420
Reaction score
397
Wanajamvi,

Gari yangu aina ya Toyota Noah, enine yake ni 1AZ, baada ya kukagua maji na oil niliiendesha mita kama 50 hivi nikasimama ili niingie dukani, kabla sijaizima ikazima yenyewe. Baada ya hapo imegoma kuwaka kabisa. Wakati nikiiendesha mpaka inazima haikuonesha tahadhali yoyote kwenye dash board. Kwa wajuzi tatizo itakuwa nini? Naomba mnijuze tafadhali.
 
Ok twambie dash bord inaonesha ukiweka switch on. Tuazie hapo au je engine inazunguka lkn haidaki moto
 
Check Terminal za bettry labda kuna kaboni, je ukiweka funguo taa zinawaka na soma kinachoonekana kwa Dashbord
 
Terminal ziko vizuri. Ukiwasha dashdoard haina tahadhari yoyote. Uikipiga inazungusha lakini haiwaki. Mafuta yako 3/4 ya tank.
Patandi kashindwa jibu maswali naona simu yake imekataa kuwaka nayo.
 
Terminal ziko vizuri. Ukiwasha dashdoard haina tahadhari yoyote. Uikipiga inazungusha lakini haiwaki. Mafuta yako 3/4 ya tank.
Kama ulinunua kwa mtu chek nae huenda aliweka tracking device huwa sometimes zinazingua. Nilifungaga kwangu kuna wakati najisahau mpaka namuita fundi kumbe ishu ni hiyo gadget
 
Terminal ziko vizuri. Ukiwasha dashdoard haina tahadhari yoyote. Uikipiga inazungusha lakini haiwaki. Mafuta yako 3/4 ya tank.
Unamaanisha nini unasema gari haiwaki wakati huo unasema kuwa dashboard ina display vizuri? je unamaanisha kuwa gari hai start? manaa kuwaka kwa gari na kustart ni vitu viwili tofauti. Unaposha gari hatua ya kwanza gari linakwenda on hapa ni kuwa mifumo yote inayotumia umeme inakuwa powered on, kisha inafuata kustart gari,
 
Kama ulinunua kwa mtu chek nae huenda aliweka tracking device huwa sometimes zinazingua. Nilifungaga kwangu kuna wakati najisahau mpaka namuita fundi kumbe ishu ni hiyo gadget
Nashukuru nitacheck nae.
 
Nina maana hai-start ingawa dashboard haionyeshi kama kuna faulty yeyote.
Unamaanisha nini unasema gari haiwaki wakati huo unasema kuwa dashboard ina display vizuri? je unamaanisha kiuwa gari hai start? manaa kuwaka kwa gari na kustart ni vitu viwili tofauti. Unaposha gari hatua ya kwanza gari linakwenda on hapa ni kuwa mifumo yote inayotumia umeme inakuwa powered on, kisha inafuata kustart gari,
 
Wanajamvi,

Gari yangu aina ya Toyota Noah, enine yake ni 1AZ, baada ya kukagua maji na oil niliiendesha mita kama 50 hivi nikasimama ili niingie dukani, kabla sijaizima ikazima yenyewe. Baada ya hapo imegoma kuwaka kabisa. Wakati nikiiendesha mpaka inazima haikuonesha tahadhali yoyote kwenye dash board. Kwa wajuzi tatizo itakuwa nini? Naomba mnijuze tafadhali.

Nadhan itakuwa imekata timing belt,, check timing belt mkuu utuletee na mrejesho shida ilikuwa ni nini
 
Wakuu na mimi nina toyota noah sr40 shida yake haina nguvu yaani hata kimlima kidooooogo inashindwa kupanda, nimesha badili engine oil na plag zote nne lakini bado tatizo lipo, msaada wenu wakuu
 
Wakuu na mimi nina toyota noah sr40 shida yake haina nguvu yaani hata kimlima kidooooogo inashindwa kupanda, nimesha badili engine oil na plag zote nne lakini bado tatizo lipo, msaada wenu wakuu
Fuel pump
 
msaada wakubwa kwa wadogo. mwenye Noah new model ao Carina Ti aniuziye kwa mkopo. Nina shida kati ya izo gari mbili. ni Pm kama umenielewa. zamana nitalipa % kodogo. than badae nije kumalizia deni.
 
Back
Top Bottom