Wale walioniuzia hilo gari kwa mara ya kwanza walinirembeshea kweli.. yaani, ati ni 'automatic transmission", kwamba "liko fully loaded" na wakanionesha jinsi lilivyo safi kwa nje na ndani! Halafu kunogeshea bei yake! ilikuwa sawa na dezo.. mzee wa watu nikasema nataka nikalijaribu kidogo, jamaa wakanipa nikapiga kona mbili tatu, gari ngurumo utadhani linabembeleza!
Kurudisha moyo umesuuzika, nikasaini mapepa yote kama nina kichaa; nikaondoka mwenyewe na gari yangu na mluzi juu! siku ya kwanza gari linanipa raha, siku ya pili.. mara mwezi likaanza kukongoloka, mara honi hailii, mara breki zinafunga katikati ya safari, mara steering haigeuka liko ka' gogo.. mwisho naona vurugu tu. Nikarudi haraka kwa jamaa
wananionesha pepa moja niliyosaini inasema "SOLD AS IS"!!!!
NIkalowa utadhani nimemwagiga maji mafinga!