SI KWELI Gari hili la MONUSCO lilipinduka Congo, 2018 lilikuwa limebeba madini

SI KWELI Gari hili la MONUSCO lilipinduka Congo, 2018 lilikuwa limebeba madini

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
This United Nations (UN) vehicle in the Democratic Republic of Congo overturned only for the residents to discover that it was carrying looted minerals.

Gari la UN Temp.jpg
 
Tunachokijua
Katika mitandao mbalimbali ya kijamii kumekuwa na picha inayosambaa ikionesha gari la UN limepinduka huko katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo na kueleezwa kuwa lilikuwa likisafirisha madini ya wizi. Tazama hapa, hapa na hapa

Uhalisia: Potoshi

Ufuatiliaji umebaini kuwa picha hiyo imekuwa ikisambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii ikiambatana na madai hayo ya gari hiyo kuwa na madini.

Tukio hilo lilitokea Oktoba 7, 2018 ambapo tovuti mbalimbali za uhakiki wa taarifa zimebainisha kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli na badala yake gari hiyo ilikuwa imebeba mchanga kwa ajili ya matumizi ya kijeshi.

Msemaji wa vikosi vya MONUSCO Florence Marchal baada ya kuhojiwa na Congo Check alieleza kuwa;

“Tumeona kwa hakika kuwa tukio hili limezua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari vya jadi. Kuhusu mifuko inayodaiwa kuwa imejaa madini, ningependa kufafanua kwamba jeshi hutumia mifuko ya mchanga kwa ajili ya ulinzi wakati wa operesheni.”
Machapisho kadhaa yanayosambaa kwenye mtandao wa Facebook yanadai kwamba lori la Umoja wa Mataifa lililopinduka katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo lilikuwa limebeba madini asilia yaliyoibiwa.

Hata hivyo, madai hayo si ya kweli. Taarifa zilizothibitishwa zinaonyesha kuwa lori hilo lilikuwa likisafirisha mifuko ya mchanga.
Uchunguzi wa ukweli umebaini kuwa ajali inayodaiwa kwenye machapisho hayo ilitokea tarehe 7 Oktoba 2018.

Kwa mujibu wa shirika la ukaguzi wa taarifa la Congo Check, lori hilo lilikuwa limebeba mifuko ya mchanga iliyokusudiwa kwa matumizi ya kijeshi.

Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Beni, ulioko katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Back
Top Bottom