Mkuu usitishe na hiki kijiwe...maana jf siku hizi imeshakuwa kijiwe cha kuchezea bao na draft.....
Ukisoma coment tu ya mdau, utagundua huyu ana gari au hana...
Utagundua huyu amesikia tu maneno ya kijiweni naye akayabeba akilini.
Hakuna gari pasua kichwa ukizingatia masharti yake.
Ubaya wa gari huwa unakuja toka kiwandani kuwa kuna baadhi ya model zinakuwa na shida mfano computer.
kama vile Nissan murano mwanzo zilikuwa na shida ya transmission, baadae Nissan wakafanya marekebisho kwenye model zilizofuata.
Toyota Rav 4 kill time kama sijkosea, nazo zilikija na matatizo ya Computer...computer yake inaonekana ilikiwa na shida ya programming toka kiwandani...ila baadae ilirekebishwa.
Ukikuta gari linatesa watu, hayo ni matatizo yake toka kiwandani kama vile mtoto anavyozaliwa mlemavu...
Sasa watanzania tunapenda bei rahisi.....mtu amezoea kununua wheel bearing ya starlet 3500/-
Akiambiwa ya Nissan ni 140000/- anaanza kusema hizi gari hazifai ni pasua kichwa..
Alafu wanavyoiponda kama wameshawahi kumiliki