Gari jipya la rais wa Marekani (Beast) laonekana wakati wa ziara ya Trump kwenye mji wa New York

Gari jipya la rais wa Marekani (Beast) laonekana wakati wa ziara ya Trump kwenye mji wa New York

RugambwaYT

JF-Expert Member
Joined
Jan 11, 2014
Posts
1,397
Reaction score
1,899

Gari hilo maarufu lililopewa jina la BEAST (mnyama mkali) kutokana na kusheheni mifumo mbalimbali ya kujilinda dhidi ya jaribio la mashambulizi kwenye msafara wa rais wa Marekani, limeonekama likipita Manhattan na viunga vya mji wa New York wakati rais Trump akihudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliohudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali duniani.

beb8351b-t1.jpg

Awali rais huyo alikuwa akitumia gari lililokumwa likitumiwa na rais Obama, amabalo halijabadilishwa tangu lilipoundwa mwaka 2009 wakati Rais Obama akiingia madarakani. Gari hilo lenye nembo ya Cadillac la mwaka 2018 ni moja kati ya magari kadhaa ya aina hiyo yanayotarajiwa kuundwa na kampuni ya General Motors kwa gharama ya takribani dola za kimarekani millioni 15.8.
Gari hilo lenye muonekano wa kisasa zaidi kuliko lile lililotumiwa na rais Obama, limezinduliwa majuma machache baada ya gari jipya la rais Putin wa Urusi na lile la rais Xi Jiping wa China kuonekana hadharani.

limos-.jpg

Taarifa kuhusu mifumo ya gari hilo bado ni siri kubwa, japo linasemekana kuwa na uwezo wa kujikinga dhidi ya mashambulizi mbalimbali ya risasi na makombora, pia lina vifaa vya huduma ya afya kwa rais ikiwemo machine ya hewa ya oxygen na damu ya rais. Picha hapo chini iliyowekwa na afisa wa habari wa Ikulu ya White House kwenye mtandao wa Twitter inaonesha mlango wa nyuma wa gari lilo wenye upana wa karibu futi moja.

66355359-t5.jpg
 
Huu wote ni ukwamu tu,yaani mbwembwe zisizo na lolote,wala hatuonagi hayo mashambulizi yoyote kwa kiongozi huyo laakini mambo ni meeeengi mbwembwe tu
 
Huu wote ni ukwamu tu,yaani mbwembwe zisizo na lolote,wala hatuonagi hayo mashambulizi yoyote kwa kiongozi huyo laakini mambo ni meeeengi mbwembwe tu
Hehehee. Tangu ashambuliwe JFK wamekuwa makini saana hao watu.
 
Huu wote ni ukwamu tu,yaani mbwembwe zisizo na lolote,wala hatuonagi hayo mashambulizi yoyote kwa kiongozi huyo laakini mambo ni meeeengi mbwembwe tu
Marekani ndio nchi inayoongoza kwa maraisi wake kushambuliwa kwa silaha wakiwa kwenye magari! Ongeza hii kwenye fikra zako.
 
Back
Top Bottom