Gari langu ni automatic. Nimegundua kuwa ninapokuwa barabarani high speed inachelewa kuchanganya gia, Tatizo hili limeanza kama wiki mbili sasa, na mara ya mwisho nilitoka Dar kuja mkoani, nikiwa high way nilikoswa koswa na fuso kwenye overtaking mpaka sasa siamini. Nimezoea ninavyoijua gari yangu huwa iko fasta sana, sasa nilikadiria umbali wa kuovertake lori lililo mbele yangu nikaingia nikakanyaga wese kwa nguvu zote mara naona gari halichanganyi nikapress O/D nayo ikachanganya kwa shida na ilipochange gear ilibadili kwa namna kama ya kushtuka ndo nikaiwahi lori nyingine iliyokuwa inakuja.
Nilipofika home hata sikumwambia mtu lile tukio maana linanijia kichwani kwa mshtuko. Nikapaki gari na bahati mbaya nikashikwa na homa kwa hiyo sijaiendesha tena. Sasa nimepata nafuu nataka niende kwa fundi lakini nawaza fundi asije akaniingiza mjini na usawa huu wa vyuma kukaza asije akanibambika kitu kingine kabisa. Hebu nipeni uzoefu wenu tatizo hili possibly inasababishwa na nini?