Gari kuchelewa kuchanganya

Gari kuchelewa kuchanganya

SIPIYU30

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Posts
1,751
Reaction score
2,437
Gari langu ni automatic. Nimegundua kuwa ninapokuwa barabarani high speed inachelewa kuchanganya gia, Tatizo hili limeanza kama wiki mbili sasa, na mara ya mwisho nilitoka Dar kuja mkoani, nikiwa high way nilikoswa koswa na fuso kwenye overtaking mpaka sasa siamini. Nimezoea ninavyoijua gari yangu huwa iko fasta sana, sasa nilikadiria umbali wa kuovertake lori lililo mbele yangu nikaingia nikakanyaga wese kwa nguvu zote mara naona gari halichanganyi nikapress O/D nayo ikachanganya kwa shida na ilipochange gear ilibadili kwa namna kama ya kushtuka ndo nikaiwahi lori nyingine iliyokuwa inakuja.

Nilipofika home hata sikumwambia mtu lile tukio maana linanijia kichwani kwa mshtuko. Nikapaki gari na bahati mbaya nikashikwa na homa kwa hiyo sijaiendesha tena. Sasa nimepata nafuu nataka niende kwa fundi lakini nawaza fundi asije akaniingiza mjini na usawa huu wa vyuma kukaza asije akanibambika kitu kingine kabisa. Hebu nipeni uzoefu wenu tatizo hili possibly inasababishwa na nini?
 
Kuzeeka kwa gari,kuchelewa kufanya service,leakage kwenye exhause pipe,plug hazichomi sawa sawa,matatizo kwenye mfumo wa hewa,gearbox kuwa na tatizo,mengine watajazia...
 
Mkuu asante kwa ushauri, ila miongoni mwa hoja zako naweza kupokea hizo nilizobold red japo ni mpaka fundi ahakikishe.
Kuhusu kuzeeka kwa gari au service nakataa kabisa. Huwa sichelewi service hovyo hovyo. Mara nyingi nikichelewa sana kufanya service haizidi km 150. Mara nyingi ni chini ya hapo. Pia kuhusu gearbox bado sikubaliani.

All in all nashukuru kwa ushauri wako, nikifika kwa fundi nitakuwa na pa kuanzia
 
Gear box nafanya service kwa mujibu wa utaratibu mubashara, kwa mfano, last service ya gearbox oil nilichange nikaweka ile original kabisa ambayo nembo yake imewekwa kwenye ile stika ya kupimia. Tena ni ghali kuliko hizi za kawaida, na Tangu nimeweka haijafika hata km 4000, wakati ile oil unaambiwa inaenda mpaka 8000km au zaidi.
 
Gear box inaelekea kuaga hio, aliyekwambia ubadilishe gear box oil ya automatic ( ATF ) ni nani ? Huwa inabadilishwa inapobadilika rangi toka nyekundu kuwa nyeusi , na inachukua hata miaka 6 au 100,000 kms . Tatizo sio kubadilisha tu bali kuipata original iliyokuwa recommended type.
 
ukiumwa nenda hospital kafanyiwe vipimo mkuu..

kama mafundi wako wa mtaani huwaamini chukua gari yako peleka toyota pugu road.. au nissan au mistubishi kutegemea na aina ya gari yako wakuangalizie tatizo nini wao na wakuhudumie...

gari ununue milion 8 au 10 au 20 uone ubahili checkup isiyozidi laki 5... tena sio kila siku ni mara moja tu
 
kabla ya kwenda hospital unaweza pia kuutaja ugonjwa wako unaohisi unakusumbua! anyway, hapo tatizo ni gearbox
 
Mkuu asante kwa ushauri, ila miongoni mwa hoja zako naweza kupokea hizo nilizobold red japo ni mpaka fundi ahakikishe.
Kuhusu kuzeeka kwa gari au service nakataa kabisa. Huwa sichelewi service hovyo hovyo. Mara nyingi nikichelewa sana kufanya service haizidi km 150. Mara nyingi ni chini ya hapo. Pia kuhusu gearbox bado sikubaliani.

All in all nashukuru kwa ushauri wako, nikifika kwa fundi nitakuwa na pa kuanzia
shida si kufanya service shida unafanya service wap na wap .. unaweza ukawa unafanya every week kumbe unafanyia vitu vya kawaida
 
huyu jamaa anachekesha sana amesikia mambo ya gearbox na pesa inapiga chenga ameamua abishe hatak ujinga kabisa
 
Gari langu ni automatic. Nimegundua kuwa ninapokuwa barabarani high speed inachelewa kuchanganya gia, Tatizo hili limeanza kama wiki mbili sasa, na mara ya mwisho nilitoka Dar kuja mkoani, nikiwa high way nilikoswa koswa na fuso kwenye overtaking mpaka sasa siamini. Nimezoea ninavyoijua gari yangu huwa iko fasta sana, sasa nilikadiria umbali wa kuovertake lori lililo mbele yangu nikaingia nikakanyaga wese kwa nguvu zote mara naona gari halichanganyi nikapress O/D nayo ikachanganya kwa shida na ilipochange gear ilibadili kwa namna kama ya kushtuka ndo nikaiwahi lori nyingine iliyokuwa inakuja.

Nilipofika home hata sikumwambia mtu lile tukio maana linanijia kichwani kwa mshtuko. Nikapaki gari na bahati mbaya nikashikwa na homa kwa hiyo sijaiendesha tena. Sasa nimepata nafuu nataka niende kwa fundi lakini nawaza fundi asije akaniingiza mjini na usawa huu wa vyuma kukaza asije akanibambika kitu kingine kabisa. Hebu nipeni uzoefu wenu tatizo hili possibly inasababishwa na nini?
Mkuu kwa tatizo hlo cha kwanza ni kuangalia fuel and power system. Yaaan kuanzia kwenye Usafi wa fuel tank lako kama lipo safi. Nenda kwenye Fuel pump nayo inachangia sana gari kupoteza nguvu kama haifanyi kaz yake vizur. Kwa mfano unakuta Fuel pump haivuti mafuta kwa kiwango kinachotakiwa. 3. Angalia ignation coil pamoja na firing order kama zpo vzur. 4 Angalia kama Spark plug zinachoma vizur. 5. Aina ya Petroli unayotumia. Maana kuna aina 3 za petroli nazo n Super ,Unlead na Premium. Hapo inw tegemea na Fuel Station ipi ww unajaza Mafuta. Lakn nnakushauri uwe unaweka TOTAL. 6 Weka Gear box Oil ambayo inashauriwa na manual ya Gar lako co kuweka ATF(AUTOMATIC TRANSMISSION FLUID) maana hzo fluid kila moja ipo na viscovity yake. 7 Angalia Gear box sensors kama zinafanya kazi vizuri. Ramadhani Kareem
 
Kuna comments zingine humu ni genuine na inafikirisha akili, yaani ni constructive criticisms maana pia zinaongeza uelewa wa mambo. Na ndo lengo la kutumia majukwaa haya ya social media kupeana uzoefu.
Lakini comments zingine ni just commedy (Mfano, Eminentia). Hivi unajua kipato changu wewe? Unarukia mambo yasiyo na tija broo. Najua hujui kipato changu, anyway hongera umeongeza idadi ya posts.
 
Back
Top Bottom