Kabla ya yote mara nyingi inatokea kulingana na upangiliaji wa gia. Ukikosea kupanga gia lazima itadai. Kila mwendo unagia yake. Ikiwa wewe uko mwendo wa 50 KPH ni dhahiri kabisa lazima injini idai gia. Kwa kawaida kama unajua unasafari ndefu hiyo speed 50 unatakiwa uwe namba 3 na pindi ukifika 80 uwe umefika namba 4. Pia inagetemea na injini. Kama imeshaanza kuchoka itakuwa inavuma kama inahitaji gia lakini haichanganyi. Ukiwa na upangiliaji mzuri wa gia na gari ambayo iko imara unaweza kwenda hadi 110+ kwa namba 4 halafu ukamalizia dashboard yako kwa namba 5 iliyobaki.
Vilevile kama gari umeizoesha mwendo wa speed -80 kufika 100+ huwa ngumu na matokeo yake ni injini kuvuma