Gari kutetemeka ukiwa speed 70-80

richardmtavi

Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
8
Reaction score
6
Habari wadau nina gari ya suzuki jimny, ni manual transmission,
Kawaida ukiwa unaendesha na ukifika kati ya speed 70-80 huwa inatetemeka. Ila ukipita 80 na zaidi inatulia na kuwa kawaida, kwa wataalamu mnaweza kujua tatizo ni nini? Au kama mtu yoyote ameshawahi kukumbana na tatizo hili, msaada tutani.
 
Mimi nimekumbana nalo msaada please
 

Mmmhhhh kwel suzuki jimny ipite 80 si utakufa[emoji23][emoji23][emoji23]
We sema ukikarbia 80 inahama barabara, hyo gar ndo ilivyo maana ni nyepesi au ndefu, aerodynamic yake ni ya ajab

Sema inalamba mafta vzr na kamuonekano kake ka nje ni kazr
 
Kama ni gari ya kuazima, yawezekana kua mwenye nalo kalifunga Speed gavana.

Au mmiliki wa zamani aljisahau akaliuza likiwa limefungwa speed gavana.
 
Na taili zikiwa zimeisha huwa gari inatetemeka
 
Nilishawahi kukutana na tatizo exactly kama hilo, nilihangaika sana kumbe shida ilikuwa ni tairi moja ya nyuma ilikuwa imepinda pinda kwa kuvimba vimba manundu, nilivyobadili tu tatizo likaisha. Awali nilipoteza pesa nyingi kubadili joints na bush za miguu ya mbele nikiamini zina duggy, ambayo poa huwa inasababisha hali kama hiyo; hivyo cheki joints na bush zote za miguu kama hazina duggy, then cheki tairi kama zimenyooka vizuri na uzifanyie wheel balance na alignment
 
Cheki tairi kama hazijavimba pia angalia bush za wishbone. Zikiisha sana huwa zinakuwa na play flani
 
Unapita nayo rough road au

Maana hiyo gari haipo confortable kwenye rough road.

barabara za vumbi inataka uindeshe kwa speed km ya mwali...

Ukiwa lami 140 unaona kama inataka kupeperuka hivi...
 
Kwa mvua hizi litaachaje kutetemeka mkuu.. Jaribu kulitembeza kwenye mikoa yenye joto kisha unote kama tatizo litajirudia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…