Gari kuwa na nguvu zaidi ya ile niliyoizoea

Gari kuwa na nguvu zaidi ya ile niliyoizoea

Hii ni experience nzuri sana.
Haya ndiyo mambo yanayotakiwa watu kushare pamoja...

Ukipata tatizo fulani unaelezea namna lilivyotibiwa inasaidia wengine wanaomiliki gari la aina hiyo..

Nachukia sana wale watu wanasema tu...gari fulani majanga...anaishia hapo haelwzi kwa kina matatizo ya gari husika na namna ya kuyatatua
Hahahaha!!!!
Unachosema ni sahihi Mkuu sometimes unakuta mtu anaomba ushauri juu ya gari Fulani lakini kitakachofuata hapo ni kuvunjana moyo
 
Nini kinachangia kupanda silencer ikiwa iddle.

Kuna gari ya jamaa alishusha silencer mpaka 700.

Ila asubuhi akiwasha gari, silencer inapanda yenyewe mpaka 1200 halafu inarudi yenyewe taratibu mpaka 900 na sio 700 iliyowekwa awali.
Mkuu hiyo process ni normal kabisa kwa gari za kisasa. Iko programmed kwenye ECU kuisaidia engine kufanya kazi vizuri immediately hata kwenye cold start. Iki rev juu hivyo engine inapata joto haraka, na mafuta yanaweza kuchanganyikana na hewa upesi. Bila hivyo, utasikia kama gari linasinzia hivi ukitia gia kuondoka. Nyingine huwa zinazima kabisa. Hasa zenye manual transmission.

Kama unakumbuka zamani tulikuwa tunaambiwa ukiwasha gari asubuhi liache kwanza kwa dakika kadhaa mpaka mshale wa temperature upande. Hiyo inasaidia mambo mengi saana kwenye gari. As engine ikipata joto, oil inakuwa nyepesi inazunguka kwa urahisi kulainisha moving parts, na mafuta yakachuwa mvuke, yanachoma haraka.

Kadri gari linavyokuwa zee, au oil iliyochoka, au isiyo standard kwa gari, ndio hiyo rev inachukua muda mrefu kushuka. Ndio maana watu wengi wakitoka kufanya service watakwambia gari lina nguvu au linachanganya haraka.

Pia ni moja ya sababu tunakuwa wakali saana tukisikia fundi kamshauri mtu kutoa themostat ili fan iwake muda wote. Hii inachosha engine. As muda wote inakuwa inapozwa kitu ambacho kinaifanya muda wote ihangahaike kupandisha joto ili kufikia joto linalohitajika kwenye engine ili ifanye kazi kwa ufanisi.
 
Mkuu hiyo process ni normal kabisa kwa gari za kisasa. Iko programmed kwenye ECU kuisaidia engine kufanya kazi vizuri immediately hata kwenye cold start. Iki rev juu hivyo engine inapata joto haraka, na mafuta yanaweza kuchanganyikana na hewa upesi. Bila hivyo, utasikia kama gari linasinzia hivi ukitia gia kuondoka. Nyingine huwa zinazima kabisa. Hasa zenye manual transmission...
Mkuu hapo kwenye fan, fan ipi unayoizungumzua? Hio fan inayowaka muda wote?
 
Kuna magari ya mafeni mawili mengine moja sasa yale yenye moja inakuaje na yenyewe hua mafeni yale yanasimama au?
Yes. Inasimama. Hasa ukiwa highway maana inaingia hewa ya kutosha kupoza coolant/maji ya radiator. Lakini mara nyingi hizi zinakuwa on muda mwingi hasa ukiwasha A/C. Ila gari nyingi za kisasa zina fans mbili. Moja ya radiator, moja ya condensor ya A/C.
 
Mimi gari nalotumia lipo moja na natumiaga A/C muda wote na pia thermostat wameitoa ila nikiendaga umbali mrefu sana lazima temperature ipande hivi kutoa thermostat inaweza kua ni chanzo hicho?
 
Mimi gari nalotumia lipo moja na natumiaga A/C muda wote na pia thermostat wameitoa ila nikiendaga umbali mrefu sana lazima temperature ipande hivi kutoa thermostat inaweza kua ni chanzo hicho?
Karibia Magari yote yanakuwa na feni mbili,moja inakuwa kwaajili ya kupoza rejeta na nyingine kwaajili ya AC na hii feni ya AC huwa inazunguka pale unapowasha AC.

Hiyo gari itakuwa haujachek vizuri sidhani kama feni IPO moja Tu
 
Mimi gari nalotumia lipo moja na natumiaga A/C muda wote na pia thermostat wameitoa ila nikiendaga umbali mrefu sana lazima temperature ipande hivi kutoa thermostat inaweza kua ni chanzo hicho?
Kwa namna fulani inachangia overheating. Labda nikuulize, fan yako imefungwa kwenye engine au inazungushwa na umeme?

Kinachofanya ipate joto ni kwamba engine inakuwa muda wote inafanya kazi ya kujipasha joto, huku at the same time inapozwa constantly. Sasa kama ni zile zilizofungwa kwenye engine, kadri unavyoongeza mwendo ndio fan inapata nguvu zaidi ya kupoza, na engine inahangaika zaidi kujipasha joto ili iweze kufanya kazi vizuri. So hapo unaona inakuwa na mzigo mkubwa. So lazima ichemke.
 
Karibia Magari yote yanakuwa na feni mbili,moja inakuwa kwaajili ya kupoza rejeta na nyingine kwaajili ya AC na hii feni ya AC huwa inazunguka pale unapowasha AC.
Hiyo gari itakuwa haujachek vizuri sidhani kama feni IPO moja Tu
Ni kweli mkuu fan ya AC ni ndogo kimtindo ipo karibu na condenser
 
Kwa namna fulani inachangia overheating. Labda nikuulize, fan yako imefungwa kwenye engine au inazungushwa na umeme?

Kinachofanya ipate joto ni kwamba engine inakuwa muda wote inafanya kazi ya kujipasha joto, huku at the same time inapozwa constantly. Sasa kama ni zile zilizofungwa kwenye engine, kadri unavyoongeza mwendo ndio fan inapata nguvu zaidi ya kupoza, na engine inahangaika zaidi kujipasha joto ili iweze kufanya kazi vizuri. So hapo unaona inakuwa na mzigo mkubwa. So lazima ichemke.
Basi ngoja nifanye mchakato nitafute thermostat niirudishie
 
Subaru zote ziko hivyo ukisafisha throttle Tu engine inakuwa na nguvu mno nakumbuka subaru forester ya jamaa Yangu alisumbuka nayo Sana Kwa mafundi makanjanja mpaka alivyoenda Kinondoni Biafra garage ndipo gari ilitulia,
Tena gari yake ilikuwa inawaka taa ya check engine muda wote....
hii shda nnauo kwenye gar yngu
 
Na nini effect ya sensor za speed kufa au kutofanya kazi sawa sawa?
Kama haipeleki signal kwenye dashboard manake speedometer yako itakuwa haifanyi kazi itakaa zero tu ila ikifa kuwa haifanyi kazi kabisa, hapo utapata misukosuko kwenye gears. Gear zitachelewa kubadilika na huenda ukajikuta umeganda kwenye gear haibadiliki kwenda gear ya juu.

Unaweza kujikuta upo gear ya pili engine RPM inapanda sana gear haibadiliki tu
 
Back
Top Bottom