Gari la Diamond Lamchefua Wema

Gari la Diamond Lamchefua Wema

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
LILE ndinga aina ya Nissan Murano alilozawadiwa supastaa Wema Sepetu na aliyekuwa mchumba wake , Nasibu Abdul ' Diamond ' , limeanza kumchefua mrembo huyo kiasi cha kulisusa.

Tukio hilo lilijidhihirisha wazi mbele ya paparazi wetu juzikati nyumbani kwa staa huyo, Kijitonyama jijini Dar, ambapo Wema alitamka hadharani kuwa kwa sasa analichukia kupita maelezo gari hilo alilozawadiwa na Diamond kwenye sherehe yake ya kuzaliwa.

Wema Sepetu akitafakari jambo. "Bwana acha nitumie hili gari lingine kwenda airport hilo Murano sitaki hata kulisikia , sijui najisikiaje hata nikiliona , " alisikika Wema.

Paparazi wetu baada ya kusikia Wema akionesha wazi kuwa analichukia gari hilo, alimuuliza sababu inayomfanya alichukie ambapo alisema hajui ni kwa nini analichukia ingawa ni mali yake. "Siku hizi sipendi kutumia hili Murano tena nalichukia kweli , inafikia kipindi nakosa raha nikiliona lakini ukiniuliza sababu ya kulichukia kiasi hicho hata sina sijui nimezoea sana kutumia BMW, ndiyo maana najikuta nalichukia gari hili, " alisema Wema.

Kwenye bethidei yake iliyofanyika Septemba mwaka huu, Wema alizawadiwa magari mawili . La kwanza lilikuwa ni BMW 545i ( Sh. Milioni 56 ) ambalo liliibua utata juu ya mtu aliyemzawadia na la pili ni Nissan Murano (Sh . milioni 36 ) alilopewa na Diamond .
 
Attachments

  • 1419056114202.jpg
    1419056114202.jpg
    54.8 KB · Views: 3,790
  • 1419056123719.jpg
    1419056123719.jpg
    67.2 KB · Views: 3,757
Mimi pia nilimsikia akisema kwenye show yake ya in my shoes....
Kama halitaki si aliuze tu jamani?yanini kujikosesha raha mwenyewe?
 
cyo auze apeleke kwenye vituo vya yatima watumie. cjui kwa nn hakuikataa cku ileile.
 
cyo auze apeleke kwenye vituo vya yatima watumie. cjui kwa nn hakuikataa cku ileile.

Ile siku alivyopewa alijishaua hadi kulilalia...angekua halipendi asingefanya vile...
 
warumi kwenye ubora wake aiseee ulikuwa kimya sana vipi ulipigwa ban nini binamu
 
Ile siku alivyopewa alijishaua hadi kulilalia...angekua halipendi asingefanya vile...

kuachwa kubaya, eeh nimesikia umbeya binamu eti akina chege walimfuma zari kwa ivan yule mume wa zari mbona patamu na ndomo kashapewa umbea tayar, nasikia chakubimbi kapeleka umbea
 
kuachwa kubaya, eeh nimesikia umbeya binamu eti akina chege walimfuma zari kwa ivan yule mume wa zari mbona patamu na ndomo kashapewa umbea tayar, nasikia chakubimbi kapeleka umbea

Mimi nasikia bado wanakutanaga kukumbushia enzi....
Mtalaka hatongozwi binamu,yetu macho.
Chege naye yumo eeh?
 
kuachwa kubaya, eeh nimesikia umbeya binamu eti akina chege walimfuma zari kwa ivan yule mume wa zari mbona patamu na ndomo kashapewa umbea tayar, nasikia chakubimbi kapeleka umbea

hivi unafanya kazi gani inayokuingizia kipato
 
Back
Top Bottom