Wadau hebu nisaidieni, gari yangu ya IST ya mwaka moja tu toka niagize inatoa mlio kama lori huku moshi ukiwa una harufu kama Petroli mbichi.
Kuna baadhi ya watu wameniambia huenda wajanja wameniibia platinum ambayo ni aina ya madini ambayo hupatikana katika kiungio ambacho huwa kinachakata mafuta yanapotoka kwenye engine.
Mwenye ujuzi anisaidie
Pole mkuu
Tatizo linaweza kuwa kama ifuatavyo kutokana na kama gari yako itakuwa inafanya kama ninavyodhani
(Kama gari inatetemeka na mlio unakuwa kama wa kumiss n unasikia harufu ya petrol kutoka kwenye exhaust)
Kama ni hivo tatizo linaweza kuwa moja katika vitu viwili..
1: ignition coil ( coil spark kibongo)
2: spark plug
1
Ignition coil ikifa huwa cylinder ambayo inahusika na kuchomwa na hiyo coil spark huwa haichomi kiwango cha mafuta na hupelekea yale mafuta kutoka moja kwa moja kwenye exhaust ( ndio maana unasikia harufu ya pure petrol kwenye exhaust)
Solution ni kutambua ni coil spark ipi imekufa kwa kuchomoa connector moja moja gari ikiwa imewaka, ukiona gari kama inataka kuzima ujue hiyo ni nzima, chomeka hamia nyingine mpaka uone ukichomoa connector gari haibadili mlio wala mtetemo hiyo itakuwa ndio coil mbovu.
2
Unaweza dhani ni coil ila ikawa ni spark plug ya hiyo cylinder ndio mbovu,
Chomoa na spark plug ikague kama ni nzima au kama huna ujuzi ihamishie kwenye cylinder iliyoonesha kuwa coil yake ni nzima, kama isipobadili hali basi spark plug ni nzima na coil ulipoitoa spark plug mwanzo ndio mbovu
Lilinukuta hili janga nikitokea musoma kwenda mwanza na ist na nikadhani ni coil spark, nilipochukua nyingine nzima na kuiweka nikaona bado na nikawa na uhakika kabisa kuwa coil mpya ni nzima.
Nilipofungua sparkplug nikagundua kale kakichuma cha chini ya ule mkunjo wa plug kalikuwa hakapo yane kameungua kabisa na kutoka. Nilipoweka sparkplug nyingine nikakuta kumbe coil yangu ni nzim kabisa nikasave 45k yangu ya ile coil mpya.
Nawakilisha.