Gari la kustaajabisha aina ya porsche 550

Gari la kustaajabisha aina ya porsche 550

Military Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2019
Posts
761
Reaction score
1,464
Majanga yanaanzia Septemba 23, 1955, ambapo James Dean raia wa Los Angeles US alinunua gari yake ya michezo aina ya Porsche 550 kwa muuzaji George Barris na akaenda kuiboresha zaidi ionekane vile alivyokuwa anapenda yeye iwe.

James aliweka siti mpya nzuri mpya za tartan, akaandika namba 130 ubavuni, na kwenye injini alikuta yameandikwa maneno 'Little Bastard', haya yaliandikwa na George mwenyewe aliyekuwa mmiliki wa kwanza wa gari hilo kabla James hajanunua. Akayafuta.

Siku hiyo hiyo Septemba 23, 1955, wakati James akiendesha gari lake karibu na Los Angeles, alikutana na muigizaji wa Alec Guinness nje ya mgahawa mmoja, akaombwa apande lakini Alec alikataa huku akionyesha hofu na uwoga mkubwa. Siku iliyofuata ikabidi amwandikie barua James kueleza ni kwanini alikuwa akionyesha hofu kupanda kwenye gari lake.

"Gari lako lilionekana kuwa baya sana kwangu, lilinipa shida, hasira, nikahisi kuumia sana. licha ya fadhili zako lakini nilijisikia mwenyewe nikisema kwa sauti ambayo sikuweza kabisa kuitambua kama ni sauti yangu, iliniambia 'tafadhali usiingie kamwe ndani ya gari, utakua maiti ndani ya wiki"

Baada ya James kusoma barua hii ya Alec, akacheka tuu kwa dharau.

Wiki moja baadaye Septemba 30, James na wenzake walikuwa wakifanya mazoezi ya kukimbiza magari kwani gari lake pia ilibidi likatumike katika mashindano ya mbio za magari huko Salinas California mwishoni mwa juma hilo.

Ni kweli mazoezi yalianza kufanyika, lakini kwa bahati mbaya James alipata ajali mbaya kwa gari lake kugongana na gari jingine na kufariki papo hapo, yule muuzaji wa gari George akaja tena kununua 'skrepa' za gari hilo baada ya kutokuwa na uwezo wa kutengenezeka tena, ukizingatia na mmiliki wake James kafariki tayari.

George akalinunua gari hilo chakavu kwa $ 2,500 zaidi ya milioni 5.5 za Kitanzania akiwa na dhamira ya kuuza tiketi kwa watu watakaotaka kuja kuliangalia gari hilo katika gereji yake, maana shauku ya watu kuliangalia gari alilopatiwa nalo ajali James ilikuwa ni kubwa.

Baadaye akachomoa injini na akaiuza kwa Troy McHenry aliyekuwa dereva wa treni, na vifaa vingine vilivyokuwa vizima akamuuzia William Eschrid. Hawa wote walienda kuvitumia kuundia magari yao binafsi.

Ajabu ni kuwa siku chache tuu mbele McHenry akiwa na gari lake lenye injini hiyo aliyoinunua alipata ajali kwa kugonga mti na kufa, Willium yeye akiwa na gari lake pia taili zilijilock ghafla bila hata sababu akiwa kwenye speed kali, akapata ajali na kuumia vibaya sana.

Taili mbili za mbele katika gari la James ziliharibika vibaya katika ajali, lakini mbili za nyuma hazikuharibika, ziliwekwa tuu katika garage ya bwana George bila kuguswa kwa miezi mingi tangu ajali iliyoondoka na maisha ya Jamesi itokee.

Baadaye taili hizi mbili George aliziuza kwa watu wawili tofauti waliokuwa na magari yao ambapo walizifunga katika magari yao, siku chache mbele wote wawili walijirusha nje ya magari yao yakiwa kwenye mwendo mkali barabarani, wakafa.

Watu walishuku kua inawezekana George alikuwa anajua kila kitu kuihusu gari hiyo, kwani yeye ndiye aliyemuuzia James wiki chache nyuma, na yeye huyo huyo ndiye aliyeichukua na kuanza kuuza spea. Hii ilipelekea gari hili chakavu kuwa la ajabu na kutakiwa liwepo katika maonyesho ya usalama barabarani yaliyotakiwa kufanyika mjini California siku chache mbeleni.

Jaribio la kwanza la kulipepeka gari hilo kwenye maonyesho lilifeli, ilikuwa ni baada ya kuzuka moto wa ajabu ulioiteketeza gereji yote ya George, lakini baada ya moto kuishi gari hiyo ikaonekana kama hakuna moto wowote ulioligusa wakati magari mengine yote yameteketea, na ilikua humo humo pia. Iliwashangaza.

Jaribio la pili la kuipelekeka gari hiyo chakavu katika maonyesho lilifaulu, lakini wakati maonyesho yakiendelea, gari likiwa limenyanyuliwa juu na kifaa maalumu, ghafla likafyatuka, likaanguka na kumuuwa mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari pale pale. Maishindano yakaisha.

Baadaye George akawa anaipakia kwenye Lori gari hiyo chakavu ili airudishe kwake, ghafla tena ikateleza kutoka kwenye Lori na kumuuwa pale pale naye baada ya kumuangukia.

Mambo yakatulia kiasi hadi mwaka 1960 wakati gari hilo chakavu lilipohitajika kupelekwa katika maonyesho ya usalama barabarani mjini Miami. Kufuatia maonyesho hayo Lori kubwa pamoja na gari jingine ndizo zilienda kulichukua gari hilo California ili liletwe kwenye maonyesho.

Ajabu ni kuwa Lori hizi mbili wakati zinarudi na gari hilo zilipotea njiani kimaajabu na hazijawahi kuonekana tangu hapo hadi leo hii.

Written by Military Genius

IMG-20200522-WA0047.jpg
 
"Gari lako lilionekana kuwa baya sana kwangu, lilinipa shida, hasira, nikahisi kuumia sana. licha ya fadhili zako lakini nilijisikia mwenyewe nikisema kwa sauti ambayo sikuweza kabisa kuitambua kama ni sauti yangu, iliniambia 'tafadhali usiingie kamwe ndani ya gari, utakua maiti ndani ya wiki"

Tatizo lilianzia hapa.
 
Mkuu naona unaijua hii story maana itakuwa mjerumani kausika kuiunda jamaa yako aliyeileta kama kaishia njiani.
"Gari lako lilionekana kuwa baya sana kwangu, lilinipa shida, hasira, nikahisi kuumia sana. licha ya fadhili zako lakini nilijisikia mwenyewe nikisema kwa sauti ambayo sikuweza kabisa kuitambua kama ni sauti yangu, iliniambia 'tafadhali usiingie kamwe ndani ya gari, utakua maiti ndani ya wiki"

Tatizo lilianzia hapa.
 
"Gari lako lilionekana kuwa baya sana kwangu, lilinipa shida, hasira, nikahisi kuumia sana. licha ya fadhili zako lakini nilijisikia mwenyewe nikisema kwa sauti ambayo sikuweza kabisa kuitambua kama ni sauti yangu, iliniambia 'tafadhali usiingie kamwe ndani ya gari, utakua maiti ndani ya wiki"

Tatizo lilianzia hapa.
Mjumbe akachukulia poa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom