Teknolojia ni Yetu sote
JF-Expert Member
- Apr 28, 2020
- 1,386
- 2,833
๐ญ Naam sio filamu za kuigiza Tena ni maisha Halisi, kwa miaka mingi Teknolojia ya Magari ya kupaa iliweza kugunduliwa toka mwaka 2015 kupitia kwa jamaa mmoja anaitwa Tim Draper.
๐ญ Kampuni ya Alef toka Sam Mateo imeingia ubia na kampuni ya Hollister na half Bay Moon airport toka bonde la silicon kwa kuanza majaribio ya kurusha magari yanayopaa.
๐ญ Gari hilo linaitwa Model A ikiwa ni la kuchaji completely , lenye uwezo wa kwenda umbali Mpaka wa Miles 200 kwa kuendesha kawaida na kwa kupaa umbali wa mile 111. Gharama yake ni Dola $300,000 ambapo watu zaidi ya 3,300 wameshaweka oda zao.
๐ญ Gari hiyo inatambuliwa kama ndege hivyo hauhitaji mkataba madhubuti wa kisheria ila kwenye utumiaji Kuna mipaka inaruhusiwa kupaa juu nyakati za mchana tu na sio kwenye maeneo ya watu wengi.
๐ญ Kampuni hiyo ya Alef inasema model A inatumia kiwango kidogo cha nishati kuliko magari mengine ya umeme kama vile Tesla EV. Baada ya zaidi ya miaka 10 ya maendeleo, majaribio yajayo yataangalia jinsi gari linavyofaa katika mifumo ya air traffic system katika viwanja vyote vya ndege.