Gari la lulu laibua mazito

Gari la lulu laibua mazito

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
MAKUBWA!
Mambo yamekuwa mambo, kadi ya gari jipya la staa wa sinema za Bongo, Elizabeth Michael Kimemeta ' Lulu' imeibua mazito kufuatia Jeshi la Polisi Dar es Salaam kubaini kuwa namba ya Sanduku La Posta ( SLP) iliyoandikwa kwenye kadi hiyo ni Wizara ya Mambo ya Ndani Tanzania.

IMEVUJAJE?
Lulu alipewa shavu kwa vile alinunua gari aina ya Toyota Rav 4 New Model kwa pesa zake mwenyewe tofauti na baadhi ya mastaa wa Bongo ambao huhongwa magari na wanaume.

SIMU YAPIGWA
Wakati gazeti hilo likiwa mitaani, mtu mmoja aliyedai kuwa ni afisa wa jeshi la polisi jijini Dar es Salaam alipiga simu kwenye chumba cha habari cha Global Publishers na kusema kuwa S .L. P ya 9140 iliyotumika kwenye kadi ya gari la Lulu ni ya jeshi hilo.

NI KOSA LA JINAI
Ofisa huyo aliliambia gazeti hili kuwa raia wa kawaida haruhusiwi kutumia sanduku la barua la jeshi kitu alichodai kinaonesha jinai ilifanyika wakati wa usajili ya gari hilo. "Haiwezekani Lulu atumie Postal Office Box ( P. O . Box au S . L.P ) ya jeshi kwenye kadi ya gari lake ikizingatiwa kuwa yeye ni raia wa kawaida . "Ukiachana na hilo hata sisi maofisa wa jeshi la polisi hatuwezi kuitumia hiyo anuani kwa shughuli zetu binafsi labda kuwe na kibali maalum," alisema afisa huyo ambaye aliomba hifadhi ya jina lake kwa vile yeye si msemaji wa jeshi hilo.

LULU ANASEMAJE?
Baada ya kupata maelezo hayo, gazeti hili lilimtafuta Lulu ili kujibu madai hayo yenye utata ambapo alisema kuna mtu alimtengenezea namba yake ya TIN ( Taxpayer Identification Number ) ndiye aliyemwekea anuani hiyo bila yeye kujua. Huku akisita kumtaja kwa jina mtu huyo lakini akimtaja kwa cheo ambacho kiko wazi na mapaparazi wetu wakamjua, Lulu alifunguka hivi : "Namiliki gari langu kihalali kabisa na nina kila kitu , niko tayari kwenda kokote kuonesha uhalali wa umiliki wangu . Kuhusu hiyo anuani, mtu aliyenitengenezea TIN Number ili nipate leseni ya udereva ndiye aliyetumia hiyo anuani , mimi sijui chochote jamani ."
AOMBA AHIFADHIWE SIRI
Katika hali ya kushangaza, Lulu aliwaambia mapaparazi wetu wasimtaje jina gazetini mtu huyo aliyemsajilia TIN akisema asitiriwe siri yake.

POLISI NAO WANENA
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke , ambako ndiko usajili wa gari hili ulifanyika katika ofisi za TRA , Zakaria Sebastian, alisema jeshi lake halina taarifa za kuwepo kwa jambo hilo lakini watalifuatilia kwa karibu . "Huenda ni mke wa askari au mwanafamilia . Unajua kuna baadhi ya maofisa wana msamaha, huenda alitumia hivyo , lakini tutafuatilia, " alisema kamanda huyo ambaye alielezwa kuwa , Lulu hajawahi kuwa mke wala mwanafamilia ya mwajiriwa wa jeshi la polisi . "Kama hajawahi kuwa mwenye kustahili kutumia anuani hii , basi tutafuatilia ili kujua wakati akiitumia , je alikuwa anakusudia kufanya jinai ? Tukijiridhisha hivyo bila shaka sheria itafuata mkondo wake."
 
Attachments

  • 1409121318410.jpg
    1409121318410.jpg
    75.4 KB · Views: 1,214
hizi sifa hizi sasa kuonyesha haya makadi hadharani ndo matokeo yake. kuna lile lenzao cjui wolper nae kwa misifa likaleta kadi hivi hivi kumbe gumashi wakalikamata gari pumbavu zao
 
Sifa zinawaponza sana hawa super nyota wetu sasa mbwe2 za kuonyesha kadi uko IG zitakuja kumponza na kuibua mapya kipuuzi tu duh sijui nani kaingia mkenge.
 
hizi sifa hizi sasa kuonyesha haya makadi hadharani ndo matokeo yake. kuna lile lenzao cjui wolper nae kwa misifa likaleta kadi hivi hivi kumbe gumashi wakalikamata gari pumbavu zao

Ahahaha ahaha kweli mkuu wolper nae ili mcost ivi ivi, da unakumbukumbu nzuri kweli, lenyewe lilijishaua kuonyesha kadi madai awazibe mdomo maadui zake matokeo yake kumbe gari la magumashi imem cost, nasikia mpaka leo ipo inaoza tu hela ya kulipia hamna
 
Sifa zinawaponza sana hawa super nyota wetu sasa mbwe2 za kuonyesha kadi uko IG zitakuja kumponza na kuibua mapya kipuuzi tu duh sijui nani kaingia mkenge.

Na ndicho kitakachotokea watu wataanza kuichunguza hiyo kadi kwa umakini kabisa na watakuta kasoro we ngoja yamkute maana hawa wasanii mambo yao ya kisanii tu
 
Na ndicho kitakachotokea watu wataanza kuichunguza hiyo kadi kwa umakini kabisa na watakuta kasoro we ngoja yamkute maana hawa wasanii mambo yao ya kisanii tu

Naona umerudi kwa kasi sana
 
Na ndicho kitakachotokea watu wataanza kuichunguza hiyo kadi kwa umakini kabisa na watakuta kasoro we ngoja yamkute maana hawa wasanii mambo yao ya kisanii tu

Hii episode nyinginee ngoja ntafute popcorn
 
Ukitaka heshima kwa gharama, utaambulia dharau na matatizo kwa bei rahisi sana kama sio bure kabisa. Sio lazima kujibu kila tuhuma unazopewa. Angekaa tu kimya as long as ana hati za gari lake.
 
Ukitaka heshima kwa gharama, utaambulia dharau na matatizo kwa bei rahisi sana kama sio bure kabisa. Sio lazima kujibu kila tuhuma unazopewa. Angekaa tu kimya as long as ana hati za gari lake.

Umeongea point, mtu anajijua yeye ni maarufu na kila kukicha anaandamwa na scandal na hili kwa lulu sio geni, sasa atashindana na wangapi? Kwani angenyamaza kimya angepasuka? Mbona mambo mengine wanayomwambia atoagi vithibitisho kama anajifanya mkwel sana
 
umeona binamu eeh, yeye angepiga tu kimya. Sisi mapovu yangetutoka weeee but tungenyamaza tu siku moja. Kukaa kimya ni jibu la mjinga. So angetupuuzia tu na wala asingepungukiwa chochote
 
Ukitaka heshima kwa gharama, utaambulia dharau na matatizo kwa bei rahisi sana kama sio bure kabisa. Sio lazima kujibu kila tuhuma unazopewa. Angekaa tu kimya as long as ana hati za gari lake.

Tatizo bongo movie wanapendaga sifa za kijinga sijui waonekane wana vitu sana na kuringishiana kusiko na maana ukute mwenyewe kapewa sometimes kunyamaza na kuwa kimya huwa ni jibu tosha
 
Tatizo bongo movie wanapendaga sifa za kijinga sijui waonekane wana vitu sana na kuringishiana kusiko na maana ukute mwenyewe kapewa sometimes kunyamaza na kuwa kimya huwa ni jibu tosha

Shauri zao na ulimbukeni wao. Mbona wanashutumiwaga mambo mengi tu na wanapiga kimya, au ndo tuamini kuwa wanayafanyaga kweli coz hawakanushagi wala kutoa vidhibiti. As long as wewe ni celebrity, jifunze tu kupotezea baadhi ya mambo coz wewe kusemwa ni inevitable.
 
Kwan lazima uonyesheee kadi ya gari jamaniiii.mi nilijua kamekuwa kumbe bado utoto mwingi
 
Back
Top Bottom