Kiturilo
JF-Expert Member
- Sep 27, 2021
- 708
- 2,859
Inasikitisha! Usiku wa kuamkia leo gari la mbunge wa jimbo la Songwe Mhe. George Mwenisongole aina ya Brevis limechomwa moto na watu wasiojulikana.
Imehisiwa kuwa hizo ni siasa za chuki zinazoendekezwa na Chadema nchini kote.
Gumzo!! Gari la Mbunge lachomwa moto na watu wasiojulikana.
===
Usiku wa kuamkia leo 29/09/2021 gari la mbunge wa jimbo la Mbozi Mh.George Mwenisongole aina ya Brevis T 231 DDZ imechomwa moto na watu wasio julikana nyumbani kwake Ichenjezya Vwawa Mbozi Songwe .
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Songwe Omary Mgumba ambae ni Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama Mkoa amesama chanzo cha tukio hilo hakijajulikana na waliofanya tukio hilo bado hawajajulikana hivyo wameviachia vyombo husika kufanya upelelezi na utakapokamilika waliohusika watawajibishwa.
Chanzo: Millard Ayo
Pia soma
~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia
- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana