Gari la mbunge wa Songwe lachomwa moto na watu wasiojulikana

Gari la mbunge wa Songwe lachomwa moto na watu wasiojulikana

Ndo huyu aliyetaka aongezewe posho? tena alipwe kwa dola, au ni mwingine....
 
Acheni ujinga wa kuingiza siasa kwenye kila eneo! Hao chadema wakimchomea gari ndo wanapata nn? Huyo mbunge ndo kazuia katiba mpya kuwepo?

Wengine wanatembea na wake za watu, wamedhulumu wengine mali zao, wakilipizwa kisasi mnaishia chadema!

Muwe mara nyingine mnafikiria nje ya box siyo kila kitu siasa tu
Nchi hii siasa zishatuharibu mzee

Ova
 
Mbunge kapiga hesabu kaona kalipia bima kubwa (comprehensive) kiasi cha kununua gari nyingine. Halafu ya kwake imechoka, kaona isiwe tabu. Kalichoma, halafu mleta mada anawaangushia zigo chadema.
Sidhani kama bima ni wajinga kiasi hicho....
 
Sidhani kama bima ni wajinga kiasi hicho....
Hawana namna mkuu lazima wamlipe. Unawasha njiti ya kiberiti unatupia ndani ya gari karibu na kibanda cha kuchomea chips halafu unawaambia bima cheche ya moto wa chips ndiyo chanzo. Unavuta mkwanja
 
Hawana namna mkuu lazima wamlipe. Unawasha njiti ya kiberiti unatupia ndani ya gari karibu na kibanda cha kuchomea chips halafu unawaambia bima cheche ya moto wa chips ndiyo chanzo. Unavuta mkwanja
Sasa bima ndo watakuwa wamekuagiza kupeleka gari karibu na jiko la chipsi? itabidi ujipange sana kuwaelewesha vinginevyo hesabu maumivu.
 
Inasikitisha! Usiku wa kuamkia leo gari la mbunge wa jimbo la Songwe mh George aina ya brevis limechomwa moto na watu wasiojulikana.
Imehisiwa kuwa hizo ni siasa za chuki zinazoendekezwa na chadema nchini kote.

Gumzo!! Gari la Mbunge lachomwa moto na watu wasiojulikana Gumzo!! Gari la Mbunge lachomwa moto na watu wasiojulikana – Millard Ayo TV
Moderator Ni vyema hizi habari za kutuhumu na kuhisi bila ushahid ziwe banned manake ni kinyume na ethics za JF zilizoainishwa kwenye guidelines.
 
Tuangalie tulipojikwaa kama Taifa. CCM , CHADEMA na wenzi wao wote sio muhimu wala wakubwa kama Tanzania. Tukumbuke hivyo kila wakati na tutende accordingly. Mwenye masikio na asikie.
 
Back
Top Bottom