Hii nchi sasa ishakuwa ngumu kila mtu anatumia nguvu yake aliyokuwa nao.
Sasa hii gari unayoiona kwenye video ni gari inadaiwa ni ya mfanyabiashara Muarabu amezua gari ya taka ya kiwanda cha AI kinachomilikiwa na kampuni ya Mohammed Enterprises lisipite na gari hilo limezuiwa mbele na nyuma.
Yani nguvu ya pesa imefanya mambo ya kijinga sana. Na haya mambo ni ushindani wao kwenye biashara na inavyoonyesha ni kama wanabifu lao kubwa tu kwahiyo kila mmoja kaamua kufanya jeuri ya kuonyesha yeye ni mbabe mbele ya mwezie.
Huyo dereva wa roli nae mstaarabu tu,
Angekuta ni mvuta bangi mmoja angeweza kugonga hiyo gari mbele na akaipeleka nje ya njia kabisa MO atalipa.
Shenzy
Mbona unaweza kusaidia tu mkuu 'Imho' kwenye swala dogo kama hili.
Naamini ukiwasilisha hii taarifa mahali maalum mambo yatanyooka tu haraka.
Kwa nini tupigishhane kilele kwenye mambo madogo kama haya. Mama hahitaji kulaumiwa kwenye maswala kama haya wakati watu mpo kushughulikia vitu vya namna hii haraka.