Gari la Tesla limeua watu wanne

Gari la Tesla limeua watu wanne

𝗚𝗮𝗿𝗶 𝗹𝗮 𝗧𝗲𝘀𝗹𝗮 𝗹𝗶𝗺𝗲𝘂𝗮 𝘄𝗮𝘁𝘂 𝘄𝗮𝗻𝗻𝗲 😔

View attachment 3152687

Watu wa nne wenye umri kati ya miaka 26 mpaka 32 waliweza kupoteza maisha kwenye jiji la Toronto nchi ya Italian Baada ya gari aina ya Tesla kuwaka moto baada ya kugonga nguzo wakiwa ndani na kushindwa kutoka.

View attachment 3152689

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 20 yeye alikua Abiria wa tano aliyeweza kunusulika chupuchupu baada ya mtu mmoja kuvunja Kioo cha karibu na kumtoa nje.

View attachment 3152690

Gari za Tesla zinatumia mifumo ya electronic kujiendesha mpaka kujifungua sasa watu hao walikufa baada ya milango kujiloki wakati watu hao walipopata ajali kwa kugonga nguzo ya umeme iliyopeleka gari kuwaka moto wakiwa ndani na kufanya milango kujifunga kusababisha watu kuungulia ndani ya gari mpaka kufa😞.

View attachment 3152692

Gari za Tesla zinalalamikiwa sana kwenye kusababisha watu kufa huku wakijitahidi kujinasua maana wengi wanajikuta wanakufa wakiwa kwenye mazingira magumu baada mitambo ya kieletroniki kushindwa kufanya kazi.
hii lugha ya "waliweza" haijakaa poa sana

waliweza kupata ajali

waliweza kufugwa goli 2

mtuhumiwa aliweza kuhukumiwa
 
Habari umeandika ni kama vile tesla self driving ndio imesababisha ajali wakati uchunguzi unafanyika na taarifa za awali zinaonyesha gari ilikuwa kwenye kasi kubwa na kumbuka kabla ya software update ya fsd 12.5.4.1, max spidi ya self drivingi ilikuwa na 40kph, habari kama hizi zilete kama zinavyoripotiwa punguza maoni binafsi utajikuta unakuwa bias
 
hii lugha ya "waliweza" haijakaa poa sana

waliweza kupata ajali

waliweza kufugwa goli 2

mtuhumiwa aliweza kuhukumiwa
Yeah! Wanaotumia hilo neno hawana tofauti na wale wanaopenda kusema wahanga wa vita,
Wahanga wa ajali, badala ya kusema
Waathirika wa vita,
Waathirika wa ajali.
Wahanga ni wale watu waliopata tatizo Kwa kujitoa (kujitoa muhanga) wakati waathirika ni wale waliopata tatizo bila kupenda.

Vichwa maji kabisa.
 
Ulivyoisagia kunguni tafkiri una hata bajaji ya kutembelea Kenge wewe...ivi ubajua Auto druve inalimit ya speed kati ya 30-50 mwisho? ..Unless kujiendehsha sio sababu kuna sababu nyingine
 
ndio maana langu nililiuza.

stori ya kikanjanja, na mchango wangu wa kibwege
 
Back
Top Bottom