je vipi kuhusu wale wananchi wanaopiga kelele maisha bora kila siku, wanaogombea maji safi kila siku na hawaishi kupata ajali, je unalo lolote la kusema pale hawa waungwana wanapopata ajali pia ??
__________________
Kama unafuatilia kwa makini utabaini kwamba humu JF watu walijadili sana masuala ya ajali za barabarani ambazo watu wamekua wakipoteza maisha. Lakini pili Zitto ni kiongozi kama alivyo Marehemu Sokoine, Merehemu Kombe, marehemu Salome Mbatia, kwa hiyo suala la ajali ni suala la kujadiliwa na inaotokea gari la kiongozi mjadala unanoga zaidi na ndio maana magazeti yameandika. Lakini pia Zitto ni mtu maarufu na muhimu na ndio maana Rais amemteua katika Kamati ya Madini, kama alivyo Jaji Mark Bomani, Dr Mwakyembe, John Cheyo na Ezekiel Maige, kwa hiyo kwa kuwa maarufu na kuwa yeye ndiye aliyeibua mjadala huu, jambo linalomhusu lazima lijadiliwe. Leo kama hiyo gari isingepata ajali, tukasikia gari la Zitto limefyatuliwa risasi na polisi baada ya kukutwa likifanya ujambazi katika maneo fulani katikati ya jiji, ingekuaje? Halafu ingesikika kwamba gari hilo limekutwa limechomwa moto mahali fulani na Zitto hajulikani aliko, tungesemaje?
Kwa mantiki hiyo, bila kujali itikadi za vyama, kama alivyosema mjumbe mmoja ni kwamba uchunguzi na mjadala wa kina usiwekewe vikwazo, bali hoja iwe wazi ili UKWELI UJULIKANE KAMA NI TUKIO LA KAWAIDA ITAJULIKANA KAMA KUNA ZIADA PIA IJULIKANE NA SI KUZIBA MIDOMO YA WATU, ili watu waendelee kujadili UPUUZI WA KASHFA ZA KIJINGA ZA VIONGOZI (wa pande zote).. Hili lina msingi kuliko kile kinachoitwa kashfa ya Slaa, Mbowe, JK etc.
MWISHO NASEMA USALAMA WA ZITTO KWA SASA SI USALAMA WA CHADEMA WALA CCM NI USALAMA WA TAIFA.. KUMBUKA UMATI WA WATU ULIONYESHEWA NA MVUA JANGWANI, LEO ZITTO ADHURIKE BILA KUWAPO MAELEZO YA KUTOSHA, ITAKUA NI KUHATARISHA USALAMA WA TAIFA. TUSITIZAME VYAMA TUTIZAME TAIFA LETU