Gari langu limekua na tatizo la kuzima wakati naendesha

UWOGA=UMASKINI

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2013
Posts
2,399
Reaction score
1,014
Kwanza nitangulize shukrani zangu za pekee kwa wanajukwa hili kwa kuwa nimejifunza mengi

Naombeni msaada hapa gari yangu ni spacio new model 1zz imekuwa na tatizo la kuzima nikiwa naendesha haswa nikiwa naendesha sehemu ambayo situmii/sikanyagi mafuta huzima na nikijaribu kuwasha inagoma mpaka nibust betri na baada ya hapo huwaka .Tafadhali ni mambo gani huchangia tatizo hili .Silence iko sawa kabisa
 
Tafuta fundi akague mfumo wako wa ufuaji umeme, maana kwa haraka haraka hapo inaonekana gari yako haijaji betri ndo maana inapelekea gari kuzima kwa kuwa betri inakuwa imeisha chaji kabisa.
 
Je gari ikishawaka inatumia betri tena kwa kuwa nataka labda ninunue betri itakuwa imekufa ndo inapelekea kuzima kwa kuwa pia betri yangu ikikaa zaidi ya SAA tano gari ikiwa off inakuwa imenyonya pia
 
Kabla ya kununua betri jirizishe kwanza na mfumo wako wa kufua umeme. Unapo washa gari kuna baddhi ya vitu vinatumia umeme kutoka kwenye betri kama vle taa, honi n.k, ndo maana gari hata ikiwa imezima ikiwasha taa zitawaka na ukipiga honi itapiga vile vile, pia gari kama haichji vizuri au betri ikiwa mbovu hata muungurumo hubadilika vile vile pamoja na kukosa nguvu.
 
Asante sana nitayafanyia kazi soon
 
Asante sana nitayafanyia kazi soon
Ina naiman kuwa betri yako ndo mbovu, ukitaka kuthitisha hilo azima betri hata kwa mtu halafu utembelee kidogo, ukiona haizim ujue shida n betri yako, unajua hata gari ukiqasha halafu utoe betri haizimi ila ukikanyaga mafuta hala ukaachia basi lazima izime, vinginevyo uendeshe na miguu miwili ili mmoja uwe kwenye brake na mwingine kwenye mafuta,

Hivyo bac, inaonekana betti lako linaporeza kabisa moto ndo maana ukiachia mafuta gari inazima.
 
Niliwahi kupata tatizo hilo, Kwa uoande wangu ilikuwa radiator ya maji ina tundu, maji yalikuwa hayamo,

Jaribu kucheki kama kuna maji kwenye radiator
 
Tafuta fundi akague mfumo wako wa ufuaji umeme, maana kwa haraka haraka hapo inaonekana gari yako haijaji betri ndo maana inapelekea gari kuzima kwa kuwa betri inakuwa imeisha chaji kabisa.
Asante kiongozi nitalifanyia kazi soon
 
Niliwahi kupata tatizo hilo, Kwa uoande wangu ilikuwa radiator ya maji ina tundu, maji yalikuwa hayamo,

Jaribu kucheki kama kuna maji kwenye radiator
Maji husababisha pia kiongozi gari kuzima mbona langu huzima wakati situmii mafuta nikiwa napanda mlima halizimi ?

Kuna siku moja ilichemsha mpaka ikazima yenyewe
 
Ina naiman kuwa betri yako ndo mbovu, ukitaka kuthitisha hilo azima betri hata kwa mtu halafu utembelee kidogo, ukiona haizim ujue shida n betri yako, unajua hata gari ukiqasha halafu utoe betri haizimi ila ukikanyaga mafuta hala ukaachia basi lazima izime, vinginevyo uendeshe na miguu miwili ili mmoja uwe kwenye brake na mwingine kwenye mafuta,

Hivyo bac, inaonekana betti lako linaporeza kabisa moto ndo maana ukiachia mafuta gari inazima.

Umenipa mwanga mkubwa sana hivyo wale wanaosema Betri kazi yake ni kuwasha gari pekee kwamba gari ikishawaka haitumii tena betri inakuwaje hapo kaka mkubwab ??
 
Back
Top Bottom