Nina gari langu dogo la mizunguko ya kazini na watoto shule, gari hii muda wote na hasa kipindi cha Desemba na Januari lilikuwa linaendeshwa na mimi au mke wangu.
Wiki ya kwanza ya Januari na hasa tarehe 3 na 4 hatukutoka na gari kabisa, kutokana na kuwa katika likizo ya mwaka mpya. Leo baada ya kugundua kuwa kuna website ya police, TMS CHECK - Tanzania Police Force, ambayo unaweza kuangalia kama gari lako linadaiwa au la
Nikaona ngoja niangalie na gari langu, lahaula nakuta system inasoma kuwa gari lilipigwa faini Tarehe 4 Januari 2019 kwa kosa la kutozingatia kivuko cha waenda kwa miguu.
Leseni ambayo inayoambatana na kosa si yangu wala ya mke wangu lakini zaidi sana kama nilivyosema katika tarehe hii, gari haikutoka ndani kabisa .
Je katika mazingira kama haya napeleka wapi malalamiko yangu kuhusu faini hii ya kubambikiwa kimakosa au kwa makusudi kabisa?
Na je kuna uthibitisho wowote naoweza kuutumia katika mazingira kama haya ?
Naomba msaada wenu.
Natanguliza Shukrani