Gari lilikuwa nyumbani siku 2, mfumo wa Trafiki Polisi unaonesha ilipigwa faini

Pia inawezekana kuna gari ipo barabarani inatembea yenye plate number kama yako au trafiki walikosea wakati wa kusoma plate namba.

Maendeleo hayana chama

Huu ni wizi unaofanya na traffic ,hizi kesi zimekua nyingi saana toka waanze kutwmbea na hizo mashine mkononi.weww sio wa kwanza kulalamika.

Upuuzi huu naona unazidi kushika kasi tu,nakushauri komaa mpk mwisho.nenda kalalamike ikishindikana nenda mahakamani tu utawasaidia wengi.
 
Wana taabu na wenye magari. Nia yao ni kuwakandamiza na kuwakamua wenye magari. Wenye leseni tu watatoa wapi bil. 29 za faini ndani ya mwezi mmoja.

Ama kweli maendeleo yana chama!
Pamoja na kuwa na gari huwezi kuendesha bila leseni, na ukiwa na leseni waweza hata kuazima gari na ukaendesha. Huwezi kuazima leseni ya kuendeshea. Hivyo ipo haja ya huu utaratibu kubadilishwa.
Mbona dereva akiwa na matatizo anafungiwa leseni?

"To expect bad man not to do wrong is madness"
 
Mkuu kwa hakika ili kutenda haki mhusika wa adhabu alikuwa dereva. Tatizo lilopo na faini wanataka pesa tena nyingi. Ndiyo maana hawanayo haja na madereva wana haja na wenye uwezo wa kukamuliwa vilivyo na hao sasa ni wamiliki. Ndiyo nia ovu iliyofichika kwenye utaratibu uliopo.
 
Wana taabu na wenye magari. Nia yao ni kuwakandamiza na kuwakamua wenye magari. Wenye leseni tu watatoa wapi bil. 29 za faini ndani ya mwezi mmoja.

Ama kweli maendeleo yana chama!
Walisema lazma muishi kama mashetani, sasa nani waliolengwa kama sio wenye magari? Je, wote wenye magari wameyapata kifisadi!
 
hayo ni makosa ya kibinadamu, nenda traffic ukalalamike. wataitafuta hiyo lessen ipo mkoa gani ova
Hii dharau kubwa sana, kosa la kibinadamu unamaanisha kuwa wanajaza taarifa bila kuangalia number za gari au inakuwaje.
Inawezekana kwa namna moja au nyingine gari yake imetoka anachoweza ni kuwabana tu traffic juu ya hiyo leseni ilotumika. Huenda funguo za gari unaacha nyumbani halafu unasema gari haijatoka.
Pili kuna kesi za namba za gari kufanana hasa hizi gari zinaingizwa kwa dili au zimeibiwa wataalam wa mambo wanazibatiza namba za usajiri wakijua kabisa usajiri huo upo na gari na mmiliki mwingine.
Kesi ya kufanana usajiri tulishuhudia mwaka jana baada ya hizi gari mbili kupaki sehemu moja na kugundulika kuwa zinafanana kwa kila kitu
 
Umuhimu wa Dash Cams umefika sasa. ...
Sijui kisheria zinaruhusiwa?
Kesi nyingi zitakuwa na ushahidi....
 
TrafficCcm walichotumwa wao ni pesa tu ukiona hivyo alikuwa anamuandikia mtu akakosea no za gari.hakuna msaada mahari utapata hapo
 
Walisema lazma muishi kama mashetani, sasa nani waliolengwa kama sio wenye magari? Je, wote wenye magari wameyapata kifisadi!

Wenye magari kama wao wanavyowaita 'matajiri' ni kada inayoonelewa sana awamu hii.

Wenye magari na hasa wenye mabasi na wenye malori wamekuwa ni maadui kwa awamu hii.

Angalia wizi wa mafuta Na biashara ya mafuta njiani unaofanywa na madereva wa malori. Serikali imefunga macho kama haioni. Yote ma SGR na hata madege yanayonunuliwa. Nyuma ya pazia believe ni kuwa fanya wanaolengwa wenye malori na mabasi cynically kuishi kama mashetani.

Pana barabara kama ya nyakanazi nyabugombe km 80 tu hivi katika njia kuu kwenda Rwanda wilaya ya biharamulo. Wakuu wameamua kuwa hawaioni.

Hiviv zile bilioni 29 za faini au zile za watorosha dhahabu si zingeboresha au kuimaliza kabisa barabara vyeti yenye kupitishwa malori mengi zaidi kwa siku kama hii? Vipi pesa za bei za dege moja la Airbus? si kipande hiki cha barabara kingeisha kabisa?

Pana haja ya wadau wahusika na ulengwaji huu kuunganisha nguvu kuwatia adabu mafedhuli hawa ambao wamejawa na roho za husika, chuki, visasi nk yaani roho kamili za kishetani.
 
ukienda izo ofisi utasikilizwa?litatatuliwa na hautaambiwa lazima ulipe?
 
Hili linawezekana. Wakati anaingiza namba kupiga faini...badala ya 356 akaingiza 365 au DNA akaingiza DAN
Sawa kabisa usemacho, nilisimamishwa karibu na Msimbazi center ya kwamba nadaiwa elf 30 kwa kosa la speed kwenye eneo la 30kph leseni inayosoma sio yangu,gari ikazuiwa nikaenda kulipa baada ya hapo nilienda trafiki makao makuu kuonana na RTO wakaangalia wakanishauli niende kitengo cha tehama makao makuu mtaa wa ghana na ohio, mwisho wa siku trafiki aliyeko Songea ndo aliyeandika faini hiyo na alikosea kusoma namba za gari nikapewa namba yake tukawasiliana akanirudishia pesa yangu na kuomba radhi kwa usumbufu nilioupata.
 
  • Thanks
Reactions: Dyf
Nina gari langu dogo la mizunguko ya kazini na watoto shule, gari hii muda wote na hasa kipindi cha Desemba na Januari lilikuwa linaendeshwa na mimi au mke wangu.

Wiki ya kwanza ya Januari na hasa tarehe 3 na 4 hatukutoka na gari kabisa, kutokana na kuwa katika likizo ya mwaka mpya. Leo baada ya kugundua kuwa kuna website ya police, TMS CHECK - Tanzania Police Force, ambayo unaweza kuangalia kama gari lako linadaiwa au la

Nikaona ngoja niangalie na gari langu, lahaula nakuta system inasoma kuwa gari lilipigwa faini Tarehe 4 Januari 2019 kwa kosa la kutozingatia kivuko cha waenda kwa miguu.

Leseni ambayo inayoambatana na kosa si yangu wala ya mke wangu lakini zaidi sana kama nilivyosema katika tarehe hii, gari haikutoka ndani kabisa .

Je katika mazingira kama haya napeleka wapi malalamiko yangu kuhusu faini hii ya kubambikiwa kimakosa au kwa makusudi kabisa?

Na je kuna uthibitisho wowote naoweza kuutumia katika mazingira kama haya ?

Naomba msaada wenu.

Natanguliza Shukrani
Anza kwa kumbana mkeo alipotoka na gari siku hiyo na ni aliendesha, mbane kisawasawa ukiwa na kalamu na karatasi mkononi, atasema.
 
Mchunguze mkeo vizuri huenda alitoka na kibenteni chake hiyo tarehe wewe unalaumu polisi bure [emoji23]

Chunguza hiyo leseni iliyohusika kwenye makosa unaweza kuta ni mume mwenzako [emoji125][emoji125][emoji125]
Hili linawezekana sana tu,tena sana tu
 
Mimi nilishapata tatizo kama lako nikaenda polisi makao makuu ghorofa ya nne kuna kitengo kinachoshughulikia nenda na leseni yako na mkeo watakusaidia na utajua fine iliandikwa wapi na nani aliandika ref. Ni leseni hivyo sio rahisi kubambikiwa.
Nina gari langu dogo la mizunguko ya kazini na watoto shule, gari hii muda wote na hasa kipindi cha Desemba na Januari lilikuwa linaendeshwa na mimi au mke wangu.

Wiki ya kwanza ya Januari na hasa tarehe 3 na 4 hatukutoka na gari kabisa, kutokana na kuwa katika likizo ya mwaka mpya. Leo baada ya kugundua kuwa kuna website ya police, TMS CHECK - Tanzania Police Force, ambayo unaweza kuangalia kama gari lako linadaiwa au la

Nikaona ngoja niangalie na gari langu, lahaula nakuta system inasoma kuwa gari lilipigwa faini Tarehe 4 Januari 2019 kwa kosa la kutozingatia kivuko cha waenda kwa miguu.

Leseni ambayo inayoambatana na kosa si yangu wala ya mke wangu lakini zaidi sana kama nilivyosema katika tarehe hii, gari haikutoka ndani kabisa .

Je katika mazingira kama haya napeleka wapi malalamiko yangu kuhusu faini hii ya kubambikiwa kimakosa au kwa makusudi kabisa?

Na je kuna uthibitisho wowote naoweza kuutumia katika mazingira kama haya ?

Naomba msaada wenu.

Natanguliza Shukrani
 
Nina gari langu dogo la mizunguko ya kazini na watoto shule, gari hii muda wote na hasa kipindi cha Desemba na Januari lilikuwa linaendeshwa na mimi au mke wangu.

Wiki ya kwanza ya Januari na hasa tarehe 3 na 4 hatukutoka na gari kabisa, kutokana na kuwa katika likizo ya mwaka mpya. Leo baada ya kugundua kuwa kuna website ya police, TMS CHECK - Tanzania Police Force, ambayo unaweza kuangalia kama gari lako linadaiwa au la

Nikaona ngoja niangalie na gari langu, lahaula nakuta system inasoma kuwa gari lilipigwa faini Tarehe 4 Januari 2019 kwa kosa la kutozingatia kivuko cha waenda kwa miguu.

Leseni ambayo inayoambatana na kosa si yangu wala ya mke wangu lakini zaidi sana kama nilivyosema katika tarehe hii, gari haikutoka ndani kabisa .

Je katika mazingira kama haya napeleka wapi malalamiko yangu kuhusu faini hii ya kubambikiwa kimakosa au kwa makusudi kabisa?

Na je kuna uthibitisho wowote naoweza kuutumia katika mazingira kama haya ?

Naomba msaada wenu.

Natanguliza Shukrani

Inawezekana wasiojulikana wanakutafuta kwa kupitia ID ya JF
 
Porojo hizi, leseni si yako wala ya mke wako, ni ya nani? Kalipe finee wacha kulialia
 
Back
Top Bottom