Sina nia ya kukuharibia biashara ila nataka kukusaidia uuze haraka,
Ushauri wangu bei iko juu ya market price ya gari yenyewe.
Nissan X-Trail ukinunua toka Japan ni kati ya $2300 hadi $2500 kwa mwaka huo na hata mwaka 2004 ambazo zina sifa ya kuwa na leather seats na gear knob yake ni tofauti na older versions.
Gharama ya TT ni about 59$ that makes a maximum total of 2600$ hiyo ni CIF with inspection ukizidisha kwa prevailing exchange rate unapata jibu.
Ushuru wa hiyo gari ni less than 4.5mil tzs
Gharama nyingine ni;
Delivery order about 200,000tzs
Wharfage + port charges about 400,000tzs
Agency fees about 250,000tzs
Plate number about 30,000tzs
Bima ndogo ni 118,000tzs
Jumla kuu ni kama mil 11,361,000tzs kwa gari ya mwaka 2004 na yenye mileage below 100k kms
Back to the point utaona umeweka bei juu sana.
Kuhusu ubora wa gari ni nzuri inataka kuzingatia service ya uhakika na huwa haitaki kuoshwa engine ukifanya hivyo mara kwa mara itaathiri kompyuta yake na kuwasha taa ya check engine na nyinginezo so ushauri puliza na pressure air na kufuta tu engine.
Kuhusu fuel consumption kuwa makini na selection ya 4wd au AWD ikiwa kwenye auto au kwenye 4wd lazima consumption ya mafuta itakuwa juu hasa ikiwa automatic kwa vile inajichagulia gear so kama kwenye foleni inakuwa gear kubwa i.e 1 au 2 halafu iko 4wd halafu unatumia AC lazima itacucost.
Otherwise ni gari nzuri sana rekebisha bei iwe within market price utauza tu.
I stand to be corrected but I thought I could share this knowledge and expertise so JF members can be aware.
All the best