Kuna siku nilileta thread humu kuomba ni namna gani naweza kupata msaada wa rufaa yangu ya bodi ikapita na mimi nikaongezewa chochote kitu maana to be honestly napata mkopo kidogo sana napata asilimia 40 tu na hapo ada ilobaki najilipia mwenyewe,kodi, kila kitu ni mimi tu .
Kiukweli Jf ina watu wazuri sana, wema na wakarimu ila pia na matapeli wapo! Baada ya kuona nimepost hiyo thread kuna mtu humu ni maarufu kiasi japo sio sana alifata pm na kunambia yupo tayari kunisaidia
Na siwezi kuficha chochote kile na kama jf wangeruhusu ningeweka pm zake zote hapa na humu jf anajiita
Focustz
Huyu jamaa
Focustz anilifata pm akinambia anataka kunisaidia na kwamba ana kaka yake anafanya kazi bodi ya mikopo
Alinambia mara nyingi sio rahisi mtu kushinda rufaa za bodi lakini kwa kua alinambia ana ndugu yake anafanya kazi huko basi akanambia atanisaidia
Mwisho akaniachie namba nimtafute, nikampigia simu tukawa tunawasiliana, kadri siku zilivyokua zikienda alikua akinishawishi na kuniahidi atanisaidia
Akaongea na kaka yake anavyodai alivyomwambia kaka yake alisema hawezi kumsaidia mtu bure bila kumpa chochote kitu na akanitolea mfano alishasaidia watu wengi lakini wakishapata wanakua hawana Shukran na hawashukuru hivyo anataka.chochote kitu
Mimi nilikubali kwakweli, kusema kweli wenyewe mnajua hali zetu tz zilivyo watu wengi wanapenda chochote kitu wanasema mkono mtupu haulambwi japo hii inatengeneza mazingira mabaya ya rushwa, haya mambo nayachukia sana lakini kuna wakati unalazimika tu
Alisema et anataka elfu 50! Mimi nilimwambia hiyo elfu 50 kisa tu nataka kuongezewa mkopo asilimia walau 80, 90 au 100 naitoa wapi wakati mimi hata hela ya kula ni tabu?
Tukaongea sana, nikamwambia aniamini kama akinisaidia ikikubali ndo nitampa,akakataa akasema ashawahi kumsaidia mtu hivyo hivyo hadi huyo mtu akapewa na refund na bodi lakini hakumpa jamaa asante wala nini
Basi akanambia nimtumie elfu 30 kwanza, wakati huo nilikua na elfu 20 tu nikamuomba anifanyie kwa elfu 20 nikija kupata nitampa elfu 30 ilobaki
Nikamtumia elfu 22 ili apate na ya kutolea, baada ya kupata akaniambia nimtumie na form index namba na taarifa nyingine nikafanya hivyo
Tuliendelea kuwasiliana km week hv baadae akawa hapatkani hata ukipiga inaita hapokei wala hajibu msg ukimtumia msg hata humu jf anajikausha km sio yeye
Bahati nzuri nina msg zake zote, Hadi simu zake zote nilirekodi, huyu ni mshenzi na ni tapeli, alitumia matatizo yangu kujinufaisha mungu akulaani popote ulipo na jf wangeniruhusu ningeanika pm zake zote hapa maana nilisikia kuanika pm hadharani ni kinyume na sheria za jf
Focustz nakuita mara 3 hichi ulichokifanya kitakutokea puani siku moja, ulitumia shida zangu kujinufaisha hela zenyewe nilikopa halafu ukanifanyia hivyo, kuweni makini na huyu mtu hata mkitaka niweke simu zote nilizorekodi ninazo,message zake na pm zake, ila nakuahidi utavuna ulichopanda
Anatumiaga namba hizi hapa 0717026364
0789391493 japo kila nikipiga naambiwa hazipatikani......
View attachment 2196311View attachment 2196312View attachment 2196313